Habari za Zanzibar
JF-Expert Member
- Dec 18, 2024
- 651
- 433
Balozi Kombo azungumza na Watumishi Ubalozi wa Tanzania
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Mahmoud Thabit Kombo, amekutana na kuzungumza na watumishi wa Ubalozi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania nchini Ufaransa,
Mhe. Kombo aliwasihi watumishi hao kuendelea kudumisha ushirikiano, umoja na kufanya kazi kwa pamoja ili kuleta tija na ufanisi katika utekelezaji wa majukumu yao.
Kikao hicho kilifanyika katika Ofisi za Ubalozi wa Tanzania jijini Paris, Julai 7, 2026 Balozi Kombo alisema mafanikio ya utekelezaji wa diplomasia ya uchumi yanategemea mshikamano wa watumishi na ari ya kufanya kazi kama timu moja yenye malengo ya pamoja ya kulitumikia Taifa.
Aidha, Balozi Kombo aliwahakikishia watumishi hao kuwa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki itaendelea kushirikiana kwa karibu na ubalozi huo pamoja na kutoa ushirikiano unaohitajika ili kuwezesha utekelezaji wa majukumu kwa ufanisi zaidi, hatua itakayochangia kuendelea kuiletea Tanzania manufaa kupitia diplomasia na ushirikiano wa kimataifa.
Akizungumza kwa niaba ya watumishi hao, Balozi wa Tanzania nchini Ufaransa Mhe. Said Yakubu alimshukuru Waziri Kombo kwa kutenga muda na kukutana na kuzungumza nao na kuahidi kuendelea kutekeleza majukumu yao kwa weledi, uzalendo na kujituma, sambamba na kuendeleza ushirikiano unaolenga kuimarisha maslahi ya Tanzania nchini Ufaransa na katika eneo la uwakilishi wao.
Balozi Kombo alikuwa nchini Ufaransa kushiriki Kongamano la Kimataifa la Kiswahili na Maadhimisho ya Pili ya Siku ya Kiswahili Duniani yaliyofanyika jijini Paris Ufaransa Julai 7,2026.