Balozi Lumbanga: Suala la Katiba mpya haliepukiki, Tunajaribu kucheza na akili za watu

BARD AI

JF-Expert Member
Joined
Jul 24, 2018
Posts
3,591
Reaction score
8,826
Katibu Mkuu Kiongozi mstaafu, Balozi Marten Lumbanga amesema mabadiliko ya Katiba hayakwepeki, huku akiwataka viongozi wa Serikali na CCM kutopuuza madai hayo.

Balozi Lumbanga aliyekuwa Katibu Mkuu Kiongozi wakati wa Rais mstaafu Ally Hassan Mwinyi na baadaye Rais mstaafu Benjamin Mkapa kabla ya kuwa Balozi nchini Uswisi, aliyasema hayo katika mahojiano na Mwananchi nyumbani kwake Masaki jijini Dar es Salaam.

“Kwanza niseme its very unfortunate (ni bahati mbaya) kwamba Kikwete aliyeanzisha hili jambo hakuli carry through (hakulifikisha) mpaka mwisho naye kastaafu, ndiyo kwanza linayumba. Laiti angelisukuma lile wakati bado yuko madarakani tungefika tamati tukawa huru.

“Ukweli nji kwamba tunajaribu kucheza na akili za watu. Suala la marekebisho ya Katiba ni suala ambalo haliepukiki. Tukilikwepa tunajaribu kulikwepa kwa muda tu, lakini halitazuilika,” alisema.

Alisema kwa kuwa tayari kuna wananchi na viongozi wenye maoni tofauti, lazima ifike mahali maoni yao yachukuliwe na yafanyiwe kazi.

“Sasa tatizo letu tunasema tu kwamba, aah! Marekani imekuwa huru zaidi ya miaka 200 wamefanya marekebisho ya Katiba mara ngapi? Sasa wenzako walianzia pazuri, wewe ulianzia kule chini unatakiwa uwe na spidi ya haraka kama wenzako? Haiwezekani.

“Tulikuwa na mfumo wa chama kimoja, wenzetu hawakuwa na kitu kama hicho. Mahitaji yanatofautiana sana,” alisema.

Huku akifafanua mabadiliko yaliyotokea kwa miaka 60 ya uhuru wa Tanzania, Balozi Lumbanga alisema, viongozi wa Serikali wanafanya makosa kuwafananisha Watanzania wa sasa na wa miaka 60 iliyopita.

“Jinsi elimu ya wananchi wetu wetu inavyozidi kupanuka, watu wamekuwa na PhD, hata mimi sikuwa na PhD lakini nimekwenda ubalozini nimejiendeleza kule mpaka nimepata. Sasa huwezi ukawachukulia kama watu wa miaka ya 1960.

Pia alisema mabadiliko ya Katiba yanakwamishwa na viongozi wanaotetea masilahi yao binafsi na kutojali masilahi ya wananchi

“Kuna watu wenye ushawishi ukiwagusa hili, wanatetea masilahi yao. Tunazungumzia future (mnustakabali) ya nchi, siyo masilahi yako, tukiyaahirisha haya leo kesho watakuja kuuliza tena,” alisema.

Akirejea mabadiliko ya mfumo wa chama kimoja kwenda vyama viwili, Lumbanga alisema baadhi ya wana CCM walimlaani.

“Huko tunakokwenda huwezi kutegemea kila mtu anaimba wimbo wa CCM, CCM, CCM imara, uimara wa CCM uko wapi?

“Mimi huwa nasema kila siku, Kama siyo Magufuli (hayati Rais John) kuamua kugombea wakati ule, CCM ilikuwa inapoteza. Tulishafanya analysis zetu kabisa tukaona CCM haiendi mbali. Magufuli kuja kugombea ndiyo ime rejuvenate (imeifufua) CCM.

“Leo ukizungumza na viongozi wengine wa CCM ambao wamelala usingizi, mimi huwa nawaambia, ninyi mmebweteka sana, mnadhani leo ni sawa na juzi, lazima mfanye mageuzi ndani ya chama....alieleza.

Chanzo: Mwananchi
 
Inashangaza kwamba kila mtu anataka katiba mpya sasa lakini viongozi wa serikali ambao ni wa kuchaguliwa kwa kura wanalipuuza.
 
Katibu Mkuu Kiongozi mstaafu, Balozi Marten Lumbanga amesema mabadiliko ya Katiba hayakwepeki, huku akiwataka viongozi wa Serikali na CCM kutopuuza madai hayo...
Kwa nini wakistaafu ndo wanajua unuhimu wa katiba? Wamekosa asali Tu hao zero brain
 
Katibu Mkuu Kiongozi mstaafu, Balozi Marten Lumbanga amesema mabadiliko ya Katiba hayakwepeki, huku akiwataka viongozi wa Serikali na CCM kutopuuza madai hayo.

Balozi Lumbanga aliyekuwa Katibu Mkuu Kiongozi wakati wa Rais mstaafu Ally Hassan Mwinyi na baadaye Rais mstaafu Benjamin Mkapa kabla ya kuwa Balozi nchini Uswisi, aliyasema hayo katika mahojiano na Mwananchi nyumbani kwake Masaki jijini Dar es Salaam.

“Kwanza niseme its very unfortunate (ni bahati mbaya) kwamba Kikwete aliyeanzisha hili jambo hakuli carry through (hakulifikisha) mpaka mwisho naye kastaafu, ndiyo kwanza linayumba. Laiti angelisukuma lile wakati bado yuko madarakani tungefika tamati tukawa huru.

“Ukweli nji kwamba tunajaribu kucheza na akili za watu. Suala la marekebisho ya Katiba ni suala ambalo haliepukiki. Tukilikwepa tunajaribu kulikwepa kwa muda tu, lakini halitazuilika,” alisema.

Alisema kwa kuwa tayari kuna wananchi na viongozi wenye maoni tofauti, lazima ifike mahali maoni yao yachukuliwe na yafanyiwe kazi.

“Sasa tatizo letu tunasema tu kwamba, aah! Marekani imekuwa huru zaidi ya miaka 200 wamefanya marekebisho ya Katiba mara ngapi? Sasa wenzako walianzia pazuri, wewe ulianzia kule chini unatakiwa uwe na spidi ya haraka kama wenzako? Haiwezekani.

“Tulikuwa na mfumo wa chama kimoja, wenzetu hawakuwa na kitu kama hicho. Mahitaji yanatofautiana sana,” alisema.

Huku akifafanua mabadiliko yaliyotokea kwa miaka 60 ya uhuru wa Tanzania, Balozi Lumbanga alisema, viongozi wa Serikali wanafanya makosa kuwafananisha Watanzania wa sasa na wa miaka 60 iliyopita.

“Jinsi elimu ya wananchi wetu wetu inavyozidi kupanuka, watu wamekuwa na PhD, hata mimi sikuwa na PhD lakini nimekwenda ubalozini nimejiendeleza kule mpaka nimepata. Sasa huwezi ukawachukulia kama watu wa miaka ya 1960.

Pia alisema mabadiliko ya Katiba yanakwamishwa na viongozi wanaotetea masilahi yao binafsi na kutojali masilahi ya wananchi

“Kuna watu wenye ushawishi ukiwagusa hili, wanatetea masilahi yao. Tunazungumzia future (mnustakabali) ya nchi, siyo masilahi yako, tukiyaahirisha haya leo kesho watakuja kuuliza tena,” alisema.

Akirejea mabadiliko ya mfumo wa chama kimoja kwenda vyama viwili, Lumbanga alisema baadhi ya wana CCM walimlaani.

“Huko tunakokwenda huwezi kutegemea kila mtu anaimba wimbo wa CCM, CCM, CCM imara, uimara wa CCM uko wapi?

“Mimi huwa nasema kila siku, Kama siyo Magufuli (hayati Rais John) kuamua kugombea wakati ule, CCM ilikuwa inapoteza. Tulishafanya analysis zetu kabisa tukaona CCM haiendi mbali. Magufuli kuja kugombea ndiyo ime rejuvenate (imeifufua) CCM.

“Leo ukizungumza na viongozi wengine wa CCM ambao wamelala usingizi, mimi huwa nawaambia, ninyi mmebweteka sana, mnadhani leo ni sawa na juzi, lazima mfanye mageuzi ndani ya chama....alieleza.

Chanzo: Mwananchi
Mzee Lumbanga Mwenyenzi Mungu azidi kukupigania na kukuepusha yule mwovu asiyependa msema kweli kuwepo huru.
Amina
 
Ameshajua kuna watu wanatetea maslahi yao,ndio hao wakisikia katiba mpya wanawashwa masikio
 
Hata Jiwe alikuwa hataki kusikia kuhusu katiba mpya kwani naye alikuwa mnufaika,unajua Bongo ukiwa Rais unakuwa zaidi ya Mfalme na kwa vile Jiwe alipenda kutukuzwa na kufanya anavyotaka kiasi cha baadhi ya chawa wake kufikia hatua ya kumuita mh.Mungu.
 
Huyu mzee inabidi apewe cheo ili astaafu nacho vizuri ama hata mshauri wa diplomasia huko Tanzania embassy in USA kidogo atanyamaza Ni akili tu za ccm jamani sio mie
Ah kabisa,maana wakiwaga ndani hawazungumzi haya
Kwanza hawa wazee washakula sana mama ya nchi hii

Ova
 
Hao wazee tunawaheshimu ila kauli zao zina utata.

Wakiwa madarakani hawakumbuki mambo kama haya kwakua walikua wanafaidi.

Ila sasa wapo nje wanaanza kutuletea maneno maneno.

Yeye alipokua katika mfumo atuambie alifanya initiative gani kuhakikisha katiba inapatikana.
 
Sasa pointi yako ni nini? Tatizo lako ni kwamba ni kwa vile hayuko madarakani au tatizo lako ni nini? Kwani wewe upo madarakani? Mbona hutaki?
 
“Mimi huwa nasema kila siku, Kama siyo Magufuli (hayati Rais John) kuamua kugombea wakati ule, CCM ilikuwa inapoteza. Tulishafanya analysis zetu kabisa tukaona CCM haiendi mbali. Magufuli kuja kugombea ndiyo ime rejuvenate (imeifufua) CCM.

“Leo ukizungumza na viongozi wengine wa CCM ambao wamelala usingizi, mimi huwa nawaambia, ninyi mmebweteka sana, mnadhani leo ni sawa na juzi, lazima mfanye mageuzi ndani ya chama....alieleza.
Anayasema haya akiwa na rangi gani ili tuamini anayosema yanatoka rohoni na yanamuuma!
 
Mzee kaongea facts ambazo Lumumba wengi hawapendi zisemwe wazi. Kiukweli kama kuna alama Mh Mbowe ataacha kwenye Taifa hili ni jinsi alivyosimama kwenye swala la Katiba.

Binafsi siamini Katiba kama mwarobaini lakini ni msingi wa kupunguza matatizo mengi.
 
IMG_20211218_014906.jpg
 
Back
Top Bottom