Amesema hivyo ili kushusha pressure ya wachangiaji wa mitandaoni, lakini pressure ikishuka na wao watapotezea. Ni kama ule utapeli wa tume ya waziri mkuu kuhusu ajali ya moto wa mafuta kule Morogoro. Ni bahati mbaya hamna mpinzani anayeweza kuitisha vyombo vya habari na kupandisha utambi kwenye hiyo ripoti.
Balozi Mahiga ana uwezo mkubwa wa kuwa mzimamoto wa serikali.
Kuna wakati Balozi wa Tanzania Burundi alishiriki kwenye biashara ya silaha. Membe alikuwa Waziri wa Mambo ya Nje. Siku hizo Balozi Mahiga alikuwa Balozi wa Tanzania UN.
Basi Membe alihojiwa akachemka kitoto. Akakataa katakata kwamba Wafanyakazi wa Serikali ya Tanzania wamehusika kwenye biashara ya silaha Mashariki ya Congo.
Kumbe BBC wamemfanyia maswali ya mtego, wanauliza maswali kama hawajui, wakati wananushahidi wite moaka text nessages za Balozi.
Kikwete alikasirika sana Membe alivyozidiwa kete na waandishi wa habari, akampigia simu Balozi Mahiga New York. Akamwambia hii kazi ya kutuliza scandal nakupa wewe.
Siku chache baadaye nikasikia BBC wanamuhoji balozi Mahiga.
Wamemuuliza seali, kwanza anaanza kujibu na historia ndefu ya Tanzania na inavyojishughulisha kupatikanankwa amani eneo la maziwa makuu, akaongea misingi ya tangu siku za Nyerere, akafundisha darasa kama enzi zake Profesa wa Chuo Kikuu. Kisha akacheza sarakasi za kidiplomasia, akasema serikali ya Tanzania haihusiki na biashara chafu ya silaha, ila hawezi kusema kama wafanyakazi wa serikali wanehusika kama watu binafsi. Anachofanya ni kaanzisha uchunguzi wa kimataifa kuangalia jambo hili, na hatua zitachukuliwa kulingana na uchunguzi utakavyoona.
Nikajua mzee mzima kashamaliza kazi.
Sikuisikia tena ile scandal wala sijui uchunguzi uliishaje. Kitu muhimu Dr. Mahiga alizima moto kidiplomasia kwa jinsi ambayo Membe alishindwa.
Baadaye kidogo nikasikia balozi wa Tanzania Burundi karudishwa nyumbani.
Nikajua mule muleee.