Ojuolegbha
JF-Expert Member
- Sep 6, 2020
- 1,773
- 1,174
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. Balozi Mahmoud Thabit Kombo (Mb.) ameipongeza Msumbiji kwa kuadhimisha miaka 50 ya Uhuru.
Pongezi hizo amezitoa kwenye hafla iliyoandaliwa na Ubalozi wa Msumbiji nchini Tanzania na kufanyika katika Ukumbi wa Polisi uliopo Masaki jijini Dar es Salaam tarehe 3 Julai, 2025.
Balozi Kombo alieleza kuwa Tanzania na Msumbiji zimekuwa na uhusiano mzuri na wa kihistoria, ukizingatia nchi hizo zina vitu vingi vinavyofanana kama vile makabila na vyakula.
Hafla hiyo imehudhuriwa na viongozi mbalimbali wa Serikali na Chama na wanadiplomasia wakiwemo, Makamu wa Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi, Mhe, Stephen Wasira, Makamu mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi mstaafu Mhe. Abrahaman Kinana, aliyekuwa Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. Balozi Liberata Mulamula (Mb.), Mkurugenzi, Idara ya Afrika katika Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Sakila Bujiku pamoja na mabalozi wanao ziwakilisha nchi zao hapa nchini.