Ojuolegbha
JF-Expert Member
- Sep 6, 2020
- 1,278
- 797
Waziri wa Mambo ya nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mheshimiwa Balozi Mahmoud Thabit Kombo (Mb.) amekutana na Mwakilishi Mkazi mpya wa Shirika la Kimataifa la Maendeleo ya Kilimo (IFAD), Bw. Sakphouseth Meng aliyefika kujitambulisha katika ofisi ndogo za Wizara jijini Dar es Salaam baada ya kuteuliwa kuiwakilisha IFAD nchini.
Katika mazungumzo yao, wameangazia kukuza ushirikiano wa karibu baina ya Tanzania na IFAD ili kuweza kuinufaisha sekta ya kilimo kwa kukuza na kuongeza ubora wa bidhaa za kilimo za Tanzania.
Katika mazungumzo yao, wameangazia kukuza ushirikiano wa karibu baina ya Tanzania na IFAD ili kuweza kuinufaisha sekta ya kilimo kwa kukuza na kuongeza ubora wa bidhaa za kilimo za Tanzania.