Ngoja tuone hayo matamko ya CHADEMA na CCM yatakuja na kitu gani!
====
Your browser is not able to display this video.
Rais na Mtendaji Mkuu wa Kituo cha Sera za Kimataifa-Afrika (CIP-AFRICA), Mheshimiwa Balozi Omar Mjenga, amepongeza jinsi zoezi la uchaguzi mdogo limeendeshwa kwa utulivu na amani. Katika mazungumzo yake, amewapongeza wale waliochaguliwa kushika nafasi mbalimbali, akisisitiza umuhimu wa kushirikiana kwa maslahi ya taifa.
Aidha, Mheshimiwa Balozi Mjenga amewataka wanasiasa kuepuka kutoa taarifa za uongo kwa umma, akieleza kuwa taarifa za aina hiyo husababisha taharuki, jambo ambalo si desturi ya Watanzania. Ametoa wito wa kuendeleza maadili mema na mshikamano ili kulinda amani ya nchi yetu.