PostGE2025 Balozi Msuya: Idadi ya vifo 518 imepatikana kwenye vyanzo rasmi kama Wizara ya Afya na wafiwa wenyewe

Conversations and stories after Tanzania's 2025 General Elections

Lexuss

Member
Joined
Mar 24, 2026
Posts
24
Reaction score
28

Mjumbe wa Tume ya Uchunguzi wa Matukio ya Oktoba 29, Balozi Radhia Msuya, ametoa ufafanuzi kuhusu idadi ya vifo iliyobainishwa katika ripoti ya tume hiyo.

Akizungumza na waandishi wa habari leo Dar es Salaam, Balozi Msuya amesema idadi hiyo imezingatia taarifa kutoka kwenye vyanzo rasmi kama vile Wizara ya Afya pamoja na ushahidi uliotolewa na mashuhuda waliojitokeza mbele ya tume wakati wa uchunguzi.

Balozi Msuya ameeleza kuwa takwimu hizo zinawakilisha hali halisi hadi wakati tume inakamilisha uchunguzi wake, na kwamba zinaweza kubadilika endapo kutapatikana taarifa nyingine mpya na sahihi kutoka kwa mamlaka husika.
 
Tufanye ni hao 500 ndio walio kufa
Nani amewajibishwa mpaka sasa?
Roho 500 zimepotea
Miguu 1000 umepotea
Mikono 1000 umepotea
Familia 500 zimeathirika Moja kwa Moja

Na Kuna watu bado wanalipana posho ofisini
 
Naam, mia tano kweli waliuwawa, nani ana paswa kuwajibika kwa vifo hivyo? hata kama angekuwa mmoja , uhai hauna mbadala!
 
Amka wewe ajuza , wajinga waliisha .

Hizo namba zenu mlizopika kwa siku 153 na hiyo mnayoita wizara ya afya msifikiri watanganyika hawaujui ukweli.

Mnaua hadi watoto wa miaka 2 mnasema walipewa mafunzo ya kuandamana.?

Watu wanapotea hadi balozi halafu mnasema sababu ya madeni, mapenzi , na kujiteka.

Msichokifahamu hadi sasa ndio kwanza mmetonesha vidonda vya watu na ukweli unajulikana na watu hawajazika ndugu zao hivyo mmetengeneza ombwe la visasi huko mbeleni msije kuanza kutafuta chanzo ni nini.
 
H
View attachment 3581535

Mjumbe wa Tume ya Uchunguzi wa Matukio ya Oktoba 29, Balozi Radhia Msuya, ametoa ufafanuzi kuhusu idadi ya vifo iliyobainishwa katika ripoti ya tume hiyo.

Akizungumza na waandishi wa habari leo Dar es Salaam, Balozi Msuya amesema idadi hiyo imezingatia taarifa kutoka kwenye vyanzo rasmi kama vile Wizara ya Afya pamoja na ushahidi uliotolewa na mashuhuda waliojitokeza mbele ya tume wakati wa uchunguzi.

Balozi Msuya ameeleza kuwa takwimu hizo zinawakilisha hali halisi hadi wakati tume inakamilisha uchunguzi wake, na kwamba zinaweza kubadilika endapo kutapatikana taarifa nyingine mpya na sahihi kutoka kwa mamlaka husika.
Hawa wazee si walishakabidhi ripoti yao? Kwanini wanaipigia promo ripoti wakati washamkabidhi alowatuma?
HIvyo vyanzo rasmi bila shaka ni Polisi, mochwari za umma na hospitali za serikali. Wote hao wakiwa watuhumiwa kuua na kupoteza taarifa kwa makusudi!
Anyways, ngoja waendelee kuwaamsha WaTanganyika!
Polisi na taasisi hizo kwa sehemu wanatuhumiwa
 
View attachment 3581535

Mjumbe wa Tume ya Uchunguzi wa Matukio ya Oktoba 29, Balozi Radhia Msuya, ametoa ufafanuzi kuhusu idadi ya vifo iliyobainishwa katika ripoti ya tume hiyo.

Akizungumza na waandishi wa habari leo Dar es Salaam, Balozi Msuya amesema idadi hiyo imezingatia taarifa kutoka kwenye vyanzo rasmi kama vile Wizara ya Afya pamoja na ushahidi uliotolewa na mashuhuda waliojitokeza mbele ya tume wakati wa uchunguzi.

Balozi Msuya ameeleza kuwa takwimu hizo zinawakilisha hali halisi hadi wakati tume inakamilisha uchunguzi wake, na kwamba zinaweza kubadilika endapo kutapatikana taarifa nyingine mpya na sahihi kutoka kwa mamlaka husika.
These mazafakas are sick in the head. Wizara ya Afya ni kwa son-in-law. Walitarajia son-in-law aunguze picha ya mother-in-law?
 
Back
Top Bottom