Zanzibar-ASP
JF-Expert Member
- Nov 28, 2013
- 11,550
- 40,697
Siku ya jana nimemsikia Balozi Mulamula akitoa onyo na vitisho dhidi ya mabalozi, maafisa wa kidiplomasia wanaoziwakilisha nchi zao na taasisi za kimataifa hapa Tanzania kuhusu hatua yao kuhudhuria mahakamani kusikiliza kesi ya ugaidi inayomkabili mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe.
Balozi Mulamula alianza kwa kutoa kauli ya jumla jumla ya kusema wafate sheria za kidiplomasia bila kusema ni sheria zipi za kidiplomasia zinazotakiwa kufuatwa au zilizovunjwa au kuelekea kuvunjwa na maafisa hao.
Baadaye alipohojiwa na waandishi wa habari Balozi Mulamula alifafanua kauli yake kwa kusema kuwa, Balozi au afisa Diplomasia anayekwenda mahakamani kuhudhuria kesi ya Mbowe anajihatarishia maisha yake na pia yuko hatarini kuambukizwa Corona!
Kupitia andiko hili ninapenda kumwambia Balozi Mulamula na wapambe wake kuwa.
Mosi, kikatiba mahakama ni mhimili unaojitegemea, hauhitaji kusemewa na mhimili mwingine(serikali), kama kuna tatizo lolote katika mazingira ya mahakama basi watendaji wa mahakama watasema wenyewe. Mulamula sio sehemu ya mhimili wa mahakama, kauli yake imelenga kuingilia utendaji wa shughuli za kila siku za kimahakama. Ametoa kauli ya upotoshaji kwa chombo asichohusika nacho.
Pili, mahakama ni eneo huru la umma, salama zaidi kiraia, lenye ulinzi madhubuti. Mtu yoyote yule anayo haki na uhuru kufika mahakamani kufuatilia mwenendo wa kesi mbalimbali, pasipo kubughudhiwa, kuomba kibali cha mamlaka yoyote au kumtaarifu mtu mwingine yoyote. Maafisa wa balozi mbalimbali na wanadiplomasia hawajaanza leo wala jana kufika kwenye mahakama zetu kufuatilia mienendo ya kesi mbalimbali. Utaratibu huo ulikuwepo toka Nyerere aliposhtakiwa na serikali ya kikoloni kabla ya uhuru na uliendelea pia hata Nyerere alipokuwa rais wa Tanzania wakati wa mashtaka dhidi ya watuhumiwa wa uhaini.
Tatu, balozi Mulamula kwa malengo yake binafsi amelenga kuichafua nchi yetu mbele ya macho ya kitaifa kwa kutaka kuonyesha eneo la mahakama za Tanzania ni mahali pa hatari. Mahakama za Tanzania hazijawahi kuwa eneo la hatari kwa kipindi chote cha uhai wa taifa letu na tusilazimishe mahakama zetu kuwa maeneo ya hatari.
Balozi Mulamula umekosea, umetokusea na umewakosea maafisa wa kibalozi. Tuombe radhi, waombe radhi na jisahihishe.
PIA, SOMA:
- Mabalozi wa kigeni wanaohudhuria kesi ya Mbowe waonywa