PreGE2025 Balozi Nchimbi achangisha sh. 950 milioni kwa matibabu ya wagonjwa wa mguu kifundo

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla)

Ojuolegbha

JF-Expert Member
Joined
Sep 6, 2020
Posts
1,773
Reaction score
1,174
BALOZI NCHIMBI ACHANGISHA SH. 950 MILIONI KWA MATIBABU YA WAGONJWA WA MGUU KIFUNDO

KATIBU Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Balozi Dkt. Emmanuel John Nchimbi, amefanikisha uchangishaji wa shilingi milioni 950 kwa ajili ya matibabu ya watoto wapatao 400 wanaougua ugonjwa wa mguu kifundo.

Kiasi hicho cha fedha kimepatikana kupitia ahadi za wadau mbalimbali walioshiriki hafla ya futari maalum kwa harambee hiyo, iliyofanyika Machi 14, 2025, katika Ukumbi wa Super Dome, Dar es Salaam. Harambee hiyo ililenga kukusanya shilingi milioni 600 kwa ajili ya matibabu hayo.

Akifungua hafla hiyo kama mgeni rasmi, Balozi Nchimbi alisema tukio hilo ni sehemu ya kumuunga mkono Mwenyekiti wa CCM na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan, ambaye ameleta mafanikio makubwa katika sekta ya afya.

β€œSiku chache zilizopita, Rais Dkt. Samia alitangazwa mshindi wa tuzo ya kimataifa kwa juhudi zake za kupunguza vifo vya mama wajawazito na watoto, na kuwa Rais wa kwanza barani Afrika kupata nishani hiyo,” alisema Balozi Nchimbi.

β€œShughuli yetu ya leo ni ishara ya kuunga mkono kazi kubwa anayoifanya kwa taifa letu, ambayo imetambuliwa kimataifa,” aliongeza.

Kupata matukio na taarifa zote kwa kila mkoa kuelekea Uchaguzi Mkuu 2025 ingia hapa: Special Thread: Mijadala na Matukio ya Uchaguzi Mikoa yote Tanzania Bara na Zanzibar kuelekea Uchaguzi Mkuu 2025

Aidha, Balozi Nchimbi alifichua kuwa baada ya kumtaarifu Rais Dkt. Samia kuhusu harambee hiyoβ€”iliyodhaminiwa na Taasisi ya GSM kwa kushirikiana na Wizara ya Afya, Klabu ya Yanga, na Hospitali ya CCBRTβ€”Rais alielekeza CCM ichangie shilingi milioni 50 kwa ajili ya kusaidia matibabu hayo.

Your browser is not able to display this video.
 
well done Dr.Emmanuel Nchimbi, The County's Agenda, Come 2030,

Allah Akuzidishie comrade πŸ™πŸ’ͺπŸ‘Š
 
Fundraising yenye kuwagusa WAHITAJI moja kwa moja.....
 
Hela zote hizo ni kama yanga tu walichanga, credit anachukua nchimbi!!!


Big up Kwa ommy dimpoz, jamaa alitoa 45M nikawa najiuliza Hawa jamaa pesa wanapata vipi aisee
 
well done Dr.Emmanuel Nchimbi, The County's Agenda, Come 2030,

Allah Akuzidishie comrade πŸ™πŸ’ͺπŸ‘Š
Wakati huo huo, Tone Tone imeishachangisha sh. milioni 7 tu kwa zaidi ya wiki tatu sasa!😎😎😎😎
 
BALOZI NCHIMBI ACHANGISHA SH. 950 MILIONI KWA MATIBABU YA WAGONJWA WA MGUU KIFUNDO

KATIBU Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Balozi Dkt. Emmanuel John Nchimbi, amefanikisha uchangishaji wa shilingi milioni 950 kwa ajili ya matibabu ya watoto wapatao 400 wanaougua ugonjwa wa mguu kifundo.

Kiasi hicho cha fedha kimepatikana kupitia ahadi za wadau mbalimbali walioshiriki hafla ya futari maalum kwa harambee hiyo, iliyofanyika katika Ukumbi wa Super Dome, Dar es Salaam. Harambee hiyo ililenga kukusanya shilingi milioni 600 kwa ajili ya matibabu hayo.

Akifungua hafla hiyo kama mgeni rasmi, Balozi Nchimbi alisema tukio hilo ni sehemu ya kumuunga mkono Mwenyekiti wa CCM na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan, ambaye ameleta mafanikio makubwa katika sekta ya afya.

β€œSiku chache zilizopita, Rais Dkt. Samia alitangazwa mshindi wa tuzo ya kimataifa kwa juhudi zake za kupunguza vifo vya mama wajawazito na watoto, na kuwa Rais wa kwanza barani Afrika kupata nishani hiyo
 

Attachments

  • VID-20250316-WA1170.mp4
    4.6 MB
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…