LGE2024 Balozi Nchimbi Ahitimisha Kampeni Akihamasisha Watanzania Kujitokeza Kupiga Kura

LGE2024 Balozi Nchimbi Ahitimisha Kampeni Akihamasisha Watanzania Kujitokeza Kupiga Kura

Uchaguzi wa Serikali za Mitaa 2024

Stephano Mgendanyi

JF-Expert Member
Joined
May 16, 2020
Posts
2,833
Reaction score
1,301
Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Balozi Emmanuel John Nchimbi, amehitimisha kampeni za uchaguzi wa Serikali za Mitaa za CCM mkoani Dar es Salaam kwa kutoa wito kwa Watanzania kujitokeza kwa wingi kupiga kura siku ya Jumatano, tarehe 27 Novemba 2024, kuchagua viongozi, hususan wanaotokana na chama hicho.​

Akihutubia mkutano mkubwa wa hadhara katika Uwanja wa Kwamnyani, Mtaa wa Kingugi, Kata ya Kiburugwa, Mbagala, wilayani Temeke leo, tarehe 26 Novemba 2024, Balozi Nchimbi amesisitiza Watanzania kutumia haki yao ya kidemokrasia kuchagua viongozi wenye maono ya maendeleo, amani na utulivu, watakaosimamia vijiji, mitaa na vitongoji kwa miaka mitano ijayo.

Balozi Nchimbi pia amewakumbusha viongozi wa CCM watakaochaguliwa kuwa watumishi wa watu, akisisitiza kwamba Chama hakitasita kuchukua hatua kali dhidi ya viongozi wake watakaotumia madaraka yao vibaya, kwa kuminya haki za wananchi au kuwadhulumu.

WhatsApp Image 2024-11-26 at 19.57.47 (1).jpeg
WhatsApp Image 2024-11-26 at 19.57.48.jpeg
WhatsApp Image 2024-11-26 at 19.57.48 (1).jpeg
WhatsApp Image 2024-11-26 at 19.57.49.jpeg
WhatsApp Image 2024-11-26 at 19.57.50.jpeg
WhatsApp Image 2024-11-26 at 19.57.50 (1).jpeg
WhatsApp Image 2024-11-26 at 19.57.51.jpeg
WhatsApp Image 2024-11-26 at 19.57.51 (1).jpeg
WhatsApp Image 2024-11-26 at 19.57.52.jpeg
WhatsApp Image 2024-11-26 at 19.57.52 (1).jpeg
WhatsApp Image 2024-11-26 at 19.57.53.jpeg
 
Back
Top Bottom