PreGE2025 Balozi Nchimbi apiga marufuku wimbo unaochochea chuki dhidi ya wapinzani

PreGE2025 Balozi Nchimbi apiga marufuku wimbo unaochochea chuki dhidi ya wapinzani

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla)
BALOZI NCHIMBI APIGA MARUFUKU WIMBO UNAOCHOCHEA CHUKI DHIDI YA WAPINZANI





KATIBU Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Balozi Emmanuel John Nchimbi amepiga marufuku wimbo unaobeza na kuchochea chuki dhidi ya vyama vya upinzani, akiagiza usitumiwe na wanaCCM popote, kwani wao wanapaswa kuwa mfano wa kuigwa kuhamasisha upendo, umoja na mshikamano nchini.

Balozi Nchimbi alichukua hatua hiyo alipokuwa akihutubia umati mkubwa wa maelfu ya wananchi wa Mji wa Shirati, wilayani Rorya, kwenye mkutano wa hadhara uliofanyika katika Uwanja wa Obwele, leo Ijumaa tarehe 25 Aprili 2025, akiwa katika siku ya nne ya ziara yake ya kikazi mkoani Mara.

Kabla ya kutoa kauli hiyo, kwanza Balozi Nchimbi aliwakumbusha wananchi waliokuwa wakimsikiliza wimbo maarufu uliokuwa unatumiwa na wanajeshi wa Tanzania kwenye Vita vya Kagera, wakati wa kumtoa na kumpiga Nduli Idi Amin Dada, aliyekuwa Rais wa Uganda, baada ya kuvamia mipaka ya Tanzania.

“Mnaukumbuka ule wimbo ulikuwa unaimbwa wakati wa Vita vya Kagera…Idi Amin akifa, mimi siwezi kulia, nitamtupa Kagera, awe chakula cha mamba…sasa naomba msikilize wimbo mwingine hapa, kisha niseme ninachotaka kukitolea kauli hapa,” alisema Balozi Nchimbi.

Akitumia simu yake kuucheza wimbo huo na kuwasikilizisha wananchi kupitia kipaza sauti alichokuwa anatumia kuhutubia, walisikika watu wakiimba wimbo unaofanana na ule wa dhidi ya Nduli Amin, huku wakiwa wamebadili maneno na kuweka mengine yanayolenga kubeza na kuchochea chuki dhidi ya vyama vya siasa vya upinzani nchini.

“Natumia nafasi hii kuendelea kusisitiza amani, umoja, mshikamano. Mwaka huu ni uchaguzi mkuu. Ni mwaka wenye vishawishi vingi. Ni lazima sana watu, hasa wanasiasa wapime kauli zao. Wawe wanasiasa wa CCM au vyama vingine, muhimu sana watoe kauli zenye kulenga kuimarisha utaifa wetu. Lazima tuulinde utaifa wetu kwa wivu mkubwa.

“Maneno haya katika wimbo huu ni maneno yanayojenga chuki. Hayajengi upendo. Napiga marufuku wimbo huu. Sisi wanaCCM tuna dhamana kubwa katika nchi hii. Lazima tuongoze kwa mfano. Tuunganishe watu. Tusiwe chanzo cha vurugu. CCM ndiyo baba na mama wa demokrasia nchini,” alisema Balozi Nchimbi kwa msisitizo.

Aidha, Balozi Nchimbi, mbali ya kutoa wito huo kwa wanaCCM, pia alitoa rai kwa viongozi na wanachama wa vyama vya upinzani: “Wote, wanaCCM na vyama vya upinzani tujiepushe na kauli zinazochochea chuki na shari na vurugu. Hata tukimsikia kiongozi wa upinzani anatoa kauli za kuchochea, tuwatafute ndugu zake huko Singida, kuwa mshaurini ndugu yenu huko anakotupeleka siko.”

Kupata matukio na taarifa zote kwa kila mkoa kuelekea Uchaguzi Mkuu 2025 ingia hapa: Special Thread: Mijadala na Matukio ya Uchaguzi Mikoa yote Tanzania Bara na Zanzibar kuelekea Uchaguzi Mkuu 2025

Kabla ya hapo, Balozi Nchimbi alitoa maelekezo kwa Waziri wa Ujenzi, Mhe. Abdalla Ulega, kuwahakikishia wananchi wa Rorya kwenye mkutano huo, kwa njia ya simu, kuhusu utekelezaji wa ujenzi wa mradi wa Barabara ya Mika – Utegi – Shirati – Kirongwe yenye kilometa 56, ambayo tayari imeshatangazwa na itaanza kujengwa mwisho wa mwezi huu, mara tu baada ya mkandarasi kupatikana.

View attachment 3315336View attachment 3315338View attachment 3315340
Mnafiq mkubwa huyu, na Samia amebugi kweli kumteua kuwa mgombea mwenza.
 
Mnafiq mkubwa huyu, na Samia amebugi kweli kumteua kuwa mgombea mwenza.
Kama anajua tuna hitaji amani na utulivu nchini kwanini hakemei yaliyo fanywa na polisi kupiga na kuumiza watu ambao walienda mahakamani bila fujo? Je? Ni sahihi kupiga watu na kuwa telekeza porini? Ni hatua gani serikali ime wachukuliia walio fanya huu unyama? Ccm mnapo lipeleka hili Taifa mta kuja kujuta
 
Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Balozi Emmanuel John Nchimbi, amepiga marufuku matumizi ya wimbo unaochochea chuki dhidi ya vyama vya upinzani, akieleza kuwa haupaswi kuimbwa wala kutumiwa na wanachama wa CCM popote nchini. Ametoa agizo hilo Aprili 25, 2025, alipohutubia maelfu ya wananchi katika Uwanja wa Obwele, Shirati, wilayani Rorya, akiwa katika ziara ya kikazi mkoani Mara.

Balozi Nchimbi alikemea vikali matumizi ya wimbo huo ambao umebadilishwa kutoka ule wa kihistoria wa Vita vya Kagera dhidi ya Nduli Idi Amin na kupewa maneno mapya yenye dhihaka kwa vyama vya siasa vya upinzani. Akiucheza hadharani kupitia simu yake, alisema wimbo huo unakiuka maadili ya kisiasa na unaweza kuathiri mshikamano wa kitaifa.

“Nasisitiza, CCM hatuwezi kuwa chanzo cha mfarakano. Tunapaswa kuwa mfano wa kuigwa wa kuhubiri upendo, mshikamano na umoja wa kitaifa, hasa katika mwaka huu wa uchaguzi mkuu,” alisema Nchimbi.

Ameongeza kuwa ni wajibu wa kila mwanasiasa, bila kujali chama chake, kuhakikisha anatoa kauli zinazojenga utaifa badala ya kuvunja umoja, akisema Tanzania imejengwa juu ya misingi ya amani inayopaswa kulindwa kwa gharama yoyote.
 
Kidogo Chimbi na Dr Mpango wanajielewa na siyo kama Samia alivyo anaye waachia polisi kufanya vitu vya ajabu
 
Dkt Nchimbi alishindwa hata kukemea na kulaani Speech ya Amos Makala kuhusu virusi vya M.pox na Ebola alivyodai vinasambazwa na kupitia TONE TONE la CHADEMA.
 
Back
Top Bottom