GE2025 Balozi Nchimbi: Mgombea aliyeshinda kura za maoni apewe kipaumbele cha kuteuliwa au kupendekezwa na vikao

Matukio, Taarifa, Habari na Mijadala ya Wananchi WAKATI wa Mchakato wa Uchaguzi Mkuu 2025

The Watchman

JF-Expert Member
Joined
Nov 7, 2023
Posts
2,186
Reaction score
4,940
Chama Cha Mapinduzi (CCM) kimeelekeza kuwa katika mchakato wa uchujaji na uteuzi wa wagombea wa nafasi za ubunge, uwakilishi na udiwani kwa Uchaguzi Mkuu wa 2025, mgombea aliyeshinda kura za maoni apewe kipaumbele cha kuteuliwa au kupendekezwa na vikao husika ili mchakato uendelee.

Kwa mujibu wa barua iliyonaswa na Jambo TV ambayo inaonesha kuwa ya tarehe 9 Agosti 2025 ikiwa imeandikwa na Katibu Mkuu wa CCM, Balozi Dkt. Emmanuel John Nchimbi, imeelezwa kuwa iwapo vikao vitaamua kutomteua mgombea aliyeongoza kura za maoni, ni lazima viwasilishe ushahidi usio na shaka wa kukiuka maadili mbele ya Sekretarieti ya Halmashauri Kuu ya CCM Taifa.

Aidha imeelezwa kuwa mwongozo huo unazingatia Kanuni ya Uteuzi katika Vyombo vya Dola, Toleo la Machi 2025 Fungu la Kwanza (5) na Fungu la Tatu (9)(1)(a), ukiwataka watendaji wa chama kuhakikisha vikao vinatenda haki ili kuepusha migawanyiko na malalamiko ndani ya CCM.

Katibu Mkuu amesisitiza kuwa utekelezaji wa mwongozo huo ni muhimu kwa “mustakabali mwema, maendeleo na uhai wa chama,” akiwataka makatibu wa mikoa na watendaji wote kuzingatia Katiba, Kanuni na miongozo ya CCM wakati wa utekelezaji wa majukumu yao.

Jambo TV
 
Mgombea Urais wa CCM na makamu wake hawakufuata katiba ya chama, kanuni na desturi za kuwania uongozi ndani ya chama kwahiyo hawana uhalali wa kuwania nafasi hizo chaa ajabu msajili wa vyama mpaka sasa yupo kimya.
 
Chama Cha Mapinduzi (CCM) kimeelekeza kuwa katika mchakato wa uchujaji na uteuzi wa wagombea wa nafasi za ubunge, uwakilishi na udiwani kwa Uchaguzi Mkuu wa 2025, mgombea aliyeshinda kura za maoni apewe kipaumbele cha kuteuliwa au kupendekezwa na vikao husika ili mchakato uendelee.

Kwa mujibu wa barua iliyonaswa na Jambo TV ambayo inaonesha kuwa ya tarehe 9 Agosti 2025 ikiwa imeandikwa na Katibu Mkuu wa CCM, Balozi Dkt. Emmanuel John Nchimbi, imeelezwa kuwa iwapo vikao vitaamua kutomteua mgombea aliyeongoza kura za maoni, ni lazima viwasilishe ushahidi usio na shaka wa kukiuka maadili mbele ya Sekretarieti ya Halmashauri Kuu ya CCM Taifa.

Aidha imeelezwa kuwa mwongozo huo unazingatia Kanuni ya Uteuzi katika Vyombo vya Dola, Toleo la Machi 2025 Fungu la Kwanza (5) na Fungu la Tatu (9)(1)(a), ukiwataka watendaji wa chama kuhakikisha vikao vinatenda haki ili kuepusha migawanyiko na malalamiko ndani ya CCM.

Katibu Mkuu amesisitiza kuwa utekelezaji wa mwongozo huo ni muhimu kwa “mustakabali mwema, maendeleo na uhai wa chama,” akiwataka makatibu wa mikoa na watendaji wote kuzingatia Katiba, Kanuni na miongozo ya CCM wakati wa utekelezaji wa majukumu yao.

Jambo TV
Baada ya kujiridhisha kuwa wengi walioshinda ni wale waliowataka wao. Vi drama 🤣🤣🤣
 
Rushwa ilitawala karibu nchi nzima kwenye kura za maoni. Asilimia kubwa ya walioongoza kura za maoni waligawa pesa kwa wajumbe mpaka kwenye maeneo ya kupigia kura.

Kazi ya kuthibitisha vitendo vya uvunjifu wa maadili mfano vitendo vya rushwa inafanywa na TAKUKURU. Lakini kwenye Vituo vya kupigia kura hawakuonekana. Naongelea huku niliko Mimi maana wangekuwepo wangewakamata watoa rushwa na wapokea rushwa. Kwa mfumo huu tunaenda kupata viongozi waliopatikana kwa rushwa. Madiwani na Wabunge, ngoja tuone
 
Back
Top Bottom