Pre GE2025 Balozi Nchimbi: Wizara ya Kilimo ishughulikie changamoto zilizojitokeza msimu uliopita ili zisijirudie kwenye ugawaji wa pembejeo msimu ujao

Pre GE2025 Balozi Nchimbi: Wizara ya Kilimo ishughulikie changamoto zilizojitokeza msimu uliopita ili zisijirudie kwenye ugawaji wa pembejeo msimu ujao

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla, wakati na baada)

Ojuolegbha

JF-Expert Member
Joined
Sep 6, 2020
Posts
1,278
Reaction score
797
Katibu Mkuu wa Chama cha Mapinduzi Balozi Dkt Emmanuel Nchimbi leo tarehe 09 Oktoba 2024 akiwa Tinde Shinyanga Vijijini amezungumza na Wananchi na moja ya kero ilikuwa ni Changamoto ya Mfumo Katika ugawaji pembejeo kwani mkulima inamlazimu mtu kutoka asubuhi sana kuwahi lakini akakosa pia .

Akielezea Jambo hilo ametoa maelekezo kwa wizara ya kilimo kuhakikisha zile Changamoto zilizojitokeza Msimu uliopita basi msimu zinakwisha na Watu wanapata pembejeo kwa urahisi.

"Nimekuwa na mazungumzo na Mbunge wenu pamoja na mafanikio aliyaongelea kero ya kwanza aliyosema ni Changamoto ya Mfumo Jinsi ya upatikanaji wa Mbegu na amesema Kwakweli watu wanakwenda wanaamka asubuhi kuwahi kwenye Vituo na wakati mwingine mfumo unakuwa chini mpaka wanaondoka jioni".

 
Back
Top Bottom