William J. Malecela
R I P
- Apr 27, 2006
- 26,584
- 10,400
- Wakuu JF, tuna habari za huzuni kwamba Mwanasiasa wa siku nyingi sana toka enzi za Mwalimu, amefariki dunia leo asubuhi sana. Tutawaletea habari zaidi za msiba na matayarisho ya mazishi.
- Mungu amuweke mahali pema peponi na poleni sana kwa familia na hasa Mkulu Oscar, tupo pamoja sana mkuu katika maombolezo.
Respect.
Field Marshall Es.
sasa mbona unatoa habari roborobo? ngaiza gani? amewahi kuwa ktk nafasi gani. kama ulimlenga oscar si unemPM ingetosha?
kama umeleta jamvini basi sema japo kidogo na wengne tujue tunamuongelea nani?
- Marehemu alifahamika kwa jina la Christopher Ngaiza, aliwahi kuwemo kwenye uongozi vyama vya ushirika kwa mkoa wa Bukoba, pia aliwahi kuwa Balozi wetu Egypt, aliporudi nyumbani akawa mshauri wa Mwalimu katika mambo ya siasa, kabla ya kwenda kwua muwakilishi wetu kwenye Great Lake Zone.
- Mwaka 1980, alipatikana na kesi ya uhaini ambayo baadaye aliachiwa na alijaribu kugombea ubunge wa Muleba Kusini, kupitia chama cha CCM, lakini hakufanikiwa hivyo akajiunga na Chadema mpaka leo asubuhi alipofariki.
- Amefariki hospitali ya mjini Nairobi na mipango ya kusaifirisha mwili kwa ajili ya mazishi yatakayofanyika nyumbani kwa marehemu mkoani Kagera, tutaendeelea kufahamishana zaidi yatakayojiri juu ya huu msiba.
- Mungu Amuweke Pema Peponi.
Respect.
FMEs!
Atakwenda tu baba wa watu. Habagui wala hachagui kwa kuwa yeye hajui atajazikwa na nani. Kwa matatizo ya watu, JK wetu hana mfano.JK anakwenda msibani?
RIP - CN: Mungu akipenda tutaonana tena.