Balozi wa kudumu wa Tanzania Umoja wa Mataifa, Dkt. Abdallah Possi, akihojiwa katika kipindi cha Jana na Leo cha Wasafi Media jana, Agosti 19, 2026, amezua mjadala mzito kuhusu vigezo na malengo yanayotumiwa na taasisi za kimataifa kutoa tuzo kwa waandishi wa habari wanaoripoti matukio ya kisiasa na haki za binadamu nchini.
Ameeleza kuwa utoaji wa tuzo hizo mara nyingi unagubikwa na mtazamo wa kiharakati badala ya umahiri na upeledi wa kazi ya uandishi wa habari.
Kauli hiyo imekuja baada ya Makala ya CNN, iliyotengenezwa na Mwandishi Larry Madowo kuhusu Mauaji ya Waandamanaji yaliyotokea wakati wa uchaguzi Oktoba 29, 2025, kupata Tuzo
Soma Makala ya kiuchunguzi ya CNN iliyotengenezwa na Larry Madowo kuhusu mauaji ya Watanzania Oktoba 29, yashinda tuzo huko Atlanta, GA, Marekani.
Akitofautisha misingi ya utoaji wa tuzo hizo, Balozi Possi amebainisha kuwa masuala ya haki za binadamu na uandishi yanaweza kutazamwa kupitia pembe kuu tatu:

- Angle ya Sheria: Mfumo usio na upande (neutral) unaofuata misingi na mikondo ya kisheria.
- Angle ya Kiharakati: Mtazamo unaofungamana na malengo mahsusi yanayotakiwa kufikiwa na kikundi au taasisi fulani.
- Angle ya Kisiasa: Mtazamo unaotafsiri haki kulingana na mazingira au eneo husika.