Balozi Seif Ally Iddi; Leo kutakuwa na tamasha la taarabu kwa wageni waalikwa wa sherehe za mapinduzi.

Balozi Seif Ally Iddi; Leo kutakuwa na tamasha la taarabu kwa wageni waalikwa wa sherehe za mapinduzi.

Ahaa ! Kumchamba mtu ni pale wanawake hasa wa pwani kuenda kumsema mwenzao ambaye ni muongo au mfitini ili akome! Tendo hili hufanywa mbele ya halaiki au kadamnasi ya watu. Wakati mwingine wachambaji hupendelea kuvaa nguo aina ya dira sare sare na kibwebwe kiunoni ili kukoleza mambo ! Mchambwaji Hua hapewi hata nafasi ya kujitetea na anaweza kusingwa vile vile. Inasemekana kabila la wazaramo ndio wataalam wa kuchamba maana huweza kumchamba mwenzao mpaka akazimia bila hata kuguswa! 😁 Nadhani nimefafanua vya kutosha.😎
Doh, nimecheka sana asee,
Mkuu inaonekana hayo mambo unayajua vizuri Sana hayo
 
Huu ni ushahidi tosha kuwa watu Wazanzibar wana asili isiyokuwa ya Kitanganyika kama wengi wenu humu munavojidanganya. Siku ya sherehe za Mapinduzi ni siku adhimu ya kusheherekea ukombozi na kupiga vita mila za kikoloni. Ikiwa wanasheherekea kwa Taarabu na sio Mdundiko au Sindimba hiyo ni kuonesha kuwa Taarabu ni utamaduni wa Wazanzibar weusi tokea asili na si kitu kilichokuwa imported kutoka nje!

Suala ni jee Watanganyika waliokuja Zanzibar ku settle kabla ya Waarabu ( kama inavojidaiwa) waliweka pembeni ngoma zao za asili na kuifata Taarabu iliyokuja baadae au walipokuja waliwakuta watu wako na tamaduni zao na ikabidi wafuate tu!
 
Back
Top Bottom