Balozi Sirro amshukuru Rais kwa kumuamini

mkuu mambo ya kijeshi ni magumu sana,msione watu wanapewa pewa vi favour fulani mkadhani ni hivi hivi.

acha twende taratibu.
wewe ukiongea na rais mama samia,unaongea na rais wako uliyemchagua au aliyechaguliwa na wenzako.
ila sirro anaongea na boss wake,kinga yake kiutendaji,mshauri wake na msemaji wake wa mwisho.
wewe unadhani kuua mke ni amri ngumu hiyo??kuna watu wako vitani huko au oparesheni wanasubiri amri ya rais tu kuua kijiji kizima cha watu au kundi fulani la watu,akisema ndio wamekwenda.kwa sababu gani???maslahi ya wengine.

amri isiyo halali haitoki kwa rais,inatoka kwa watu na viongozi wengine.
 
Mtu anapewa amri ya kuua mke na mganga na anaua itakuwa Rais
 
Ewe Dunia ebu simama nishuke, kama mkuu unafikiri kwa kiwango hiki basi Tanzania yetu itachukua generation nyingi kubadilika, vyombo vya usalama vipo kwa ajili yetu sio politicians na madikiteta uchwara, bila shaka wewe ni mmoja you can't even question kuhusu matumizi ya fedha yetu kwa vyombo hivi, nakuona hata ukipotea njia huwezi kwenda kumuuliza mwanajeshi akuonyeshe njia!,karibu huku lingusenguse, ukilewa polisi anakuendesha kukupeleka nyumbani!
 
Mkuu ni katiba ndio inasema hivyo sio mimi
 

Atafute gunia ya kubebea pesa Zimbabwe. Yaani Raisi anajua atakuwa mharibifu mpaka kumpeleka huko
 
Sirro ni mtu mwema sana, mcha Mungu, mwenye huruma na Kiongozi kweli. Changamoto ya Sasa ni kuwa ili uongoze lazima vyama vya upinzani wakusifie pasi. Mwenyezi Mungu amjalie utulivu wa Moyo. Sadaka yake ya ujenzi wa Kanisa itaenziwa. Namuona Kingai nae akifuata uelekeo huo huo na mwisho nchi itapoteza viongozi wema kwa sababu binafsi za baadhi ya vyama vya siasa.
 
Wakatoliki tunajidhalilisha sana!! Huyu muuaji alitubu lini? Na fedha zake mmechukua siyo? Huyu mseminari aligeuka shetani na kuua zaidi ya shetani mwenyewe!
 
Ni kazi ile mkuu.Ina kiapo cha utii kwa Rais na nchi.Usimlaumu sana.Moyoni na yeye hapendi uonevu.Hatujazaliwa wakatili.Ni maisha,mazingira na ugali.πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚
Mazingira na ugali!! Kwa miaka yote amechukua pochi za walipa kodi bado amekuwa tegemezi wa ugali!???? Ni kiazi tu!!
Hivi Said Mwema yuko wapi??
 
Huwezi ukafanya kazi Polisi ama jeshi na ukajikuta mchamungu,izo kazi kupata uchamungu ni ngumu sana elewa ilo,
 
Huwezi ukafanya kazi Polisi ama jeshi na ukajikuta mchamungu,izo kazi kupata uchamungu ni ngumu sana elewa ilo,
Wacha Mungu wapo wengi kwenye majeshi yetu hasa kwenye level za uafisa. Mfano CDF mstaafu. Ni Myth tuu kuwa ukiwa Mwanajeshi huwezi kuwa mchamungu. Hata vitani watu wanasali.
 
Wacha Mungu wapo wengi kwenye majeshi yetu hasa kwenye level za uafisa. Mfano CDF mstaafu. Ni Myth tuu kuwa ukiwa Mwanajeshi huwezi kuwa mchamungu. Hata vitani watu wanasali.
Stori za vijiweni hizi. Sio majeshi ya kiafrika
 
Tuishi kwa kujitahudi kutenda haki. Mali na madaraka ni vitu vya kupita.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…