mwanamwana
JF-Expert Member
- Aug 1, 2011
- 1,309
- 4,798
Balozi wa Norway Nchini Tone Tinnes, akizungumza kwenye Maadhimisho ya Siku ya Demokrasia Duniani yanayofanyika Chuo Kikuu cha Dar Es Salaam amesema “Utafiti na masomo yanaonyesha kwamba hali ya demokrasia duniani inaporomoka. Ripoti ya Freedom House ya mwaka 2023 inaonyesha kwamba demokrasia duniani imeendelea kudorora kwa miaka 18 mfululizo, na Afrika inaongoza kwenye hili.
Mwaka ujao kutakuwa na uchaguzi nchini Tanzania kwa ajili ya serikali, na pia kutakuwa na uchaguzi nchini Norway kwa ajili ya bunge na serikali.
Ninawahimiza kila mtu kupiga kura, tumia haki yako ya kupiga kura, jiandikishe. Ni jukumu letu kuhamasisha na kuhakikisha kwamba tunakuwa viongozi katika nchi ambayo watu wanaamini kuna sababu ya kupiga kura kwa sababu sauti zao zinasikilizwa
Nilifika Tanzania mwaka 1999 na nikaona uchaguzi wa mitaa uliofanyika mwaka huo. Kisha nilikuwa sehemu ya shughuli za uchaguzi mkuu mwaka 2000 na sasa ninakuja tena na nitakuwa hapa kwa uchaguzi wa serikali za mitaa mwaka huu na kwa uchaguzi wa wabunge na urais mwaka ujao. Nimekuwa na uzoefu wa awali wa mfumo wa vyama vingi Tanzania na nimeona maendeleo ya vyama vya upinzani nchini Tanzania”