Balozi wa Marekani nchini Tanzania atembelea Ofisi za JamiiForums

Ni wazi JF inaheshimika na kutambulika zaidi ya media nyingi hapa Tanzania, sasa JF waangalie uwezekano wa kuanzisha magazeti, luninga, na radio station yao.

Hizi ziara za hawa mabalozi zinaonesha vile kizuri kinavyojiuza...
Swadakta
 
Ni jambo jema sana kwa mabalozi mbalimbali wanapotembelea ofisi za JF. Hii inatoa taswira moja muhimu sana. Na pia inatoa ujumbe muhimu sana ndani ya jamii yetu.

Mchango wa JF ni wenye kuthaminika mno ndani na nje ya mipaka ya Tanzania.

Kazi kubwa inayofanywa na ofisi hii katika kusimamia maudhui ya habari, kusimamia "privacy" ya watoa habari, na hata kutoa habari za uhakika na zenye kuaminika kwa wakati ni alama pekee ambayo wana jukwaa tunajivunia.

Nichukue nafasi hii kuupongeza uongozi mzima wa JF na wanajukwaa wote kwa ujumla. Natoa ofa ya kinywaji kwa wanajukwaa wote, ila angalizo tu kila mmoja anywe kwa gharama zake mwenyewe.
 
Hongera sana Maxence Melo and Team JF.

Kutembelewa na ujumbe huu mzito ni kutambulika kwa kazi nzuri ya JF katika kutoa maoni yanayozingatiwa na viongozi wa nchi.
Hii ni medium ya ukweli, haraka, na kupima joto la wananchi kwa haraka haraka.

Hongereni sana.
 
Binafsi nimemdharau na.kumpuuza huyu jamaa. Achana nae tu.
 
Aisee mpaka wazungu itakuwa wananijua wamenisoma soma ndege John ndani ya JF.
 
Mainzi YANAUMIA sana kuona hii kitu

Jamiiforums hoyeeeee......
 
Kuna watu huwa nawaona wanacomment sana ujinga ila nafikiri ikitokea siku moja JAMII FORUM imepotea itawaacha na kovu la uchizi wa akili. Jamii forum ni kisiwa cha maarifa yeyote

Watanzania wengi waliopo nnje ya nchi mtandao huu ni sehemu ya familia zao

LonG live
 

Hebu fafanua kidogo, baraka za nini.
 
Hebu fafanua kidogo, baraka za nini.
Kwani Baraka ni nini?

But again mzungu hafanyi kitu bila sababu/malengo.

Hawa watu wanakuwaga na malengo ya muda mrefu😄😄juzi Sweden leo American
 
Huyo balozi hajaniulizia huko ,,,,kwamba yule member wenu April26 hajambo!!
 
Hongera Melo, kutokusaliti jukwaa Zama za Giza za Meco. Asante Mh.Balozi Ni heshima na joto kwa wapigania Haki na Uhuru wa habari.
 
Kaka MM na team nzima ya JF, kwa mara nyingine tena Hongereeni sana!!

Hizi ni dalili za wazi kabisa kwamba katika ule muundo wa Kikao cha Mabalozi walio na balozi au uwakilishi wa Nchi zao hapa Tanzania, agenda ya JF imetua mezani kwao na ikaongelewa kwa umahiri na umakini mkubwa.

Kwa hayo tuyaonayo, kwa hakika JF muda si mrefu mtakuwa ktk anga (level) nyingine kabisa kwa yale mnayoyafanya kwa niaba ya Watanzania tulio wengi. Tegemeeni ushauri mkubwa sana wa Teknolojia na wa Uendeshaji wa shughuri zenu.

Nimesema hayo pia baada ya kuwaona wajumbe walioambatana na Balozi.

Hongereeni Sana JF. Pigeni Kazi.
 
Mkuu Nyani Ngabu sasa unaizalilisha nchi yetu, huyo sio balozi wa nyumba kumi
 
Bwahahahahahahaa, hii sasa ni kumi bila, KNOCK-OUT kabisa.
Aisee, Maxence Melo hongera sana braza, nuru imekuzukia.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…