Nyakijooga
JF-Expert Member
- Dec 9, 2018
- 524
- 829
Wakili Massawe: Huwezi kuwa na uhuru kamili kama vyombo vya habari havipati uhuru huo
Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu (LHRC), Wakili Fulgence Massawe amesema kuwa ilitarajiwa katika kipindi hiki cha kuelekea uchaguzi Mkuu vyombo vya habari vitakuwa huru zaidi kuliko kipindi chochote kile.
Amesema kwamba uhuru vyombo vya habari ni eneo muhimu ambalo utazamwa katikati hatua za kidemokrasia, ambapo amesema kuwa LHRC itaendelea kuwa mstari wa mbele kupigania uhuru wa vyombo vya habari pamoja na waandishi wa habari ikiwemo Sheria ambazo ni mwiba.
Akitolea mfano, Sheria inayotoa mamlaka kwa TCRA kusajili na kuratibu vyombo vya Mtandao, kwamba inatumika kuwapa nguvu ya kutuhumu, kusikiliza na kutoa adhabu jambo ambalo anasema kuwa sio sawa katika kuleta haki.
Amesema kwamba utaratibu huo unakiuka haki asili, huku akipendekeza kwamba mamlaka mengine ni vyema yangepelekwa kwenye mikono ya chombo kingine kama Mahakama ili kuwezesha mazingira ya haki.
Hayo ameyasema September 8, 2025 wakati LHRC wakisaini rasmi mkataba mpya wa makubaliano wa miaka mitatu na Norway wenye thamani ya NOK milioni 19 (takribani dola milioni 2 za Kimarekani). Ubalenga kusaidia utekelezaji wa mpango mkakati mpya wa LHRC wa 2025–2030.
Ameongeza kuwa,Mkataba unatarajiwa kuongeza tija kwenye maeneo mbalimbali, ikiwemo mashauri ya kimkakati, msaada wa kisheria, mabadiliko ya sheria pamoja na kuimarisha sauti za wananchi katika mchakato wa uwajibikaji kitaifa na kimataifa ikiwa ni pamoja kustawisha uhuru wa kujieleza.
Balozi wa Norway nchini Tanzania anasisitiza kuhusu uhuru wa kujieleza katika kustawisha demokrasia
Akizungumza katika hafla hiyo ya utiaji saini, Balozi wa Norway nchini Tanzania, Tone Tinnes, amesisitiza umuhimu wa ushirikiano huu akisema: “Mkataba huu unaakisi dhamira ya muda mrefu ya Norway katika haki za binadamu nchini Tanzania. Kwa kuunga mkono LHRC, tunachangia jamii katika haki za kisiasa, maridhiano, uwezeshaji wa wanawake na uhuru wa kujieleza vinakuwa msingi wa maendeleo ya kijamii na kiuchumi.”
Pia kwa msisitizo ameongeza kuwa: “Haki za kisiasa na maridhiano ni msingi wa kujenga imani na utulivu. Demokrasia imara inategemea uhuru wa kujieleza na sauti huru, na Norway inajivunia kuunga mkono kazi ya LHRC ya kulinda maadili haya.”
Imeelezwa kwamba Mkataba uliosainiwa
utadumu kipindi cha 2025-2027, ikiwa ni mwendelezo wa ushirikiano wa muda mrefu tangia mwaka 2013.