Kipanga, I cannot invest so much emotion in beauty pageants, lakini naona ishu hii imekugusa sana, hivyo naomba bila jazba na matusi nikujibu kiutu uzima Kabla ya yote naomba nitofautishe mada hapa. Kuna suala la mrembo binafsi na imani yake ya dini. Kuna suala la investment kwa upande wa waandaji. Kuna suala la mikataba.
Sasa naomba tuanze na imani ya binti ambayo ni eneo nililotumia kumsifu binti huyu. Imani yake binti ni private matter. Anaweza akawa ameshindana na kutokana na factors mbalimbali akaona kwamba alichokifanya ni kinyume na imani yake. Hivyo akajitokeza hadharani na kusema hataki taji na kulirudisha. Mi namsifu kwa sababu ni kheri afanye hivyo kuliko kuanza kuwapiga chenga waandaji, kutafuta vijisababu vya kutoshiriki au kuleta vituko na kuzima simu eti hapatikani kwenye shughuli mbalimbali. [Nakumbuka Nancy Sumari aliwafanyia hivyo waandaji mpaka wakaandikana kwenye magazeti, Mrembo huyu wa mwaka jana, Radhia naye hajafanya shughuli zozote za kijamii] Like this it is straight forward na Angela anampatia nafasi mrembo mwingine ambaye atafanya kazi hiyo kwa moyo mkunjufu. Ndiyo maana nimemsifia dada, amekuwa mwazi na hajapindisha.
Investment kwa upande wa waandaji: Waandaji waliandaa hafla mbalimbali, lakni ni hafla moja tu ambayo iliandaliwa specific for Angela, ni ile iliyofanyika wiki iliyopita ya kupokea taji kutoka yule mshindi wa 2007. Gharama zingine za fainali ya Miss Tanzania walipomtangaza, fashion show ya Redds iliyofanyika Mwanza, haziwezi kuhesabika maana shughuli ingefanyika whether Angela angeshiriki au la. Kama wana mpango wa kumdai compensation, nadhani this is the only area wanaweza kumdai (kukabidhi taji). Zaidi ya hapo, alikuwa ni mmoja ya washiriki. So hakuna investment kubwa iliyofanyika kwa upande wa Redds.
Mikataba: Kama Redds na Lino wanafanya shughuli hizi bila mikataba basi nitawashangaa sana. Redds huu ni mwaka wao wa 3 au 4 wanatoa taji, Lino ni miaka 10 na kitu wanaandaa Miss Tz na hawajajifunza kusaini mikataba na warembo? Kwa kweli hii si fundisho tosha. Ndiyo maana kumbe wanashindwa hata kumvua taji washindi wao wanaoboronga? Maana hawana legal premise ya kufanya hivyo!? Sasa kama ni kweli hawana mikataba hii fundisho haijawagharimu vya kutosha. Maana wana bahati dada huyu alikuwa mstaarabu.