Balozi wa REDDS 2008 arejesha Taji na Zawadi

Jamani inashangaza watu wengi wanazungumzia shinikizo la wazazi, kwa tukio lenyewe lilivyokwenda sioni dalili za shinikizo la mzazi/wazazi, pengine shinikizo la waumini/muumini katika kanisa lao, hapo yawezekana. nasema hivyo kutokana na kwamba wazazi wote walikuwepo kwenye kutunukiwa na kumpongeza sasa hilo shinikizo limekuja lini??? baada ya kufika nyumbani ama wapi?, mimi sioni hata mmoja kati ya wazazi wake kuwa ni muumini wa kweli katika imani za dhati ya kuabudu.
 
...

Susuviri,
Tunawekana sawa mazee sioni kama kuna jazba au matusi kukosa busara au hekima kupo na watu wa aina hiyo wapo so sorry mkuu kama imekukwaza. Lakini narudi katika hoja zako 3 yaani imani Angela, Investment kwa waandaji na Mikataba. Mtu ana haki ya kuamini vile anavyoamini na kwa ukweli bado sioni mantiki ya Angela kurudisha taji na zawadi kwa kigezo cha imani yake. Kama ulivyosema mwenyewe Redd's wamekuwa na hili shindano kwa karibu mwaka wa 3 au 4 that means hata yeye alijua wazi kuwa akishiriki mashindano ya urembo wa Tanzania lazima kipengele cha kumtafuta mrembo wa Redd's hawezi kukiepuka so alikuwa na muda wa kuamua haikuwa ghafla kama moto umelipuka. Alipanda ndege toka Dar mpaka Mwanza alielewa kinachoenda kufanyika huko na imani yake ilikuwa iko vizuri tu wakati huo so again alitakiwa kuamua mapema kushiriki au kutoshiriki.

Investment kwa waandaji.. Ni kweli waliandaa hafla moja ya kumvisha taji Angela kwa kuwa amerudisha taji na zawadi. Sasa mrembo atakayechaguliwa tena na TBL (sijui kwa style ipi) atavishwa taji mbele ya waandishi wa habari au kwenye ofisi za TBL??? au naye itabidi afanyiwe hafla???

Mikataba; Kwa hili sina uhakika na uendeshaji wa mashindano kama washiriki husaini mikataba yoyote may be Bw. Lundenga au yeyote anayefahamu atufahamishe lakini suala ni kuwa kama kuna makubaliano baina ya pande mbili nadhani ni wajibu kwa kila upande kuheshimu unless kuna sababu za maana sana. Mimi si mwanasheria lakini kwa mtazamo wa kawaida tu Angela alikosea, kwa mfano warembo walielezwa mapema kuwa mshindi wa Redd's atapata zawadi ya Sh. 2.5ml na mambo mengine then ikawa Angela ameshinda na TBL hawakumpa zawadi kama walivyoahidi ungeichukuliaje wewe????
 
Mambo matata na utatanishi mkubwa... Sikujua kama kuna makanisa yanakubaliana na mchakato mzima wa mashindano ya Ulimbwende lakini yanagomea suala zima la kuhusiana na Pombe...

Kweli kuna utata katika dini zetu.!

Mkuu Mzozo

Hapo umeongea, hivi inaingia akilini kweli mtu kushiriki mashindano ya ulimbwende halafu ukatae zawadi za pombe?, maana nafikiri kushiriki tu ni mbaya zaidi ya pombe, mavazi ya kuogelea kupita mbele za watu, na je angeshinda kwenda Miss World ambako vichupi vinatawala angesemaje?. Mi nafikiri huyu binti huenda aliingia bila kuwataarifu waumini wenzake kuhusu ushiriki. Au ameombewa baada ya kupotea na sasa anarudi kundini. Huu ni upuuzi mkubwa sasa kambania mtu zawadi hiyo?. Next time kina Lundenga watoe form za hawa kujaza kama wanafungamana na imani yoyote kali kabla ya kuwa shortlist.
 

Sipingi kama Redds au kina lundenga wamekwazwa na angela wachukue hatua za kisheria lakini navojua mambo yetu yanavofanywa kienyeji sidhani kuna mkataba unaombana angela,tusubiri tuone au waanze 2009
 
kwani ulipokuwa unagombania hukujua unagombania kuwa nani!!! hii kali alafu umekaa baada ya wiki eti unarudisha pesa umeambiwa utatengwa nini kanisani!!!!!!!!!
 

Bint amechanganyikiwa!!

Hebu nenda hapa

http://dailynews.habarileo.co.tz/st...ador2008AngelaLubalaTalksOnHerTitle.flv&id=46
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…