TANZIA Balozi wa Saudia afa katikati ya hotuba akimsifia Rais Al Sisi

TANZIA Balozi wa Saudia afa katikati ya hotuba akimsifia Rais Al Sisi

Webabu

JF-Expert Member
Joined
Apr 29, 2010
Posts
8,870
Reaction score
14,258
Balozi maarufu wa Saudia na tajiri mkubwa bwana Mohamed Al qahtan, amefariki huko jijini Cairo nchini Misri wakati akitoa hotuba yake. Mara baada ya kumsifia Rais Alsisi kwa kuashiria picha yake iliyokuwa nyuma yake kwa kusema huyu ni kiongozi wa watu wote mpaka siku ya mwisho ghafla alianguka kwa kishindo kinyume nyume na kudakwa na wenzake waliokuwa karibu naye. Alipata huduma ya mwanzo na kutolewa kupelekwa hospitali. Hata hivyo muda mfupi baadae alifariki dunia

Imeelezwa ya kuwa balozi huyu wa muda mrefu nchini humo kwa mara ya mwanzo aliugua maradhi ya moyo mwaka 2013 mara baada ya uchaguzi uliompa ushindi Mohammed Morsi.



1660228153192.png
 
Mmh yan kakata moto ghafla...itakua heart attack by the way. RIP bwana balozi
 
Huku kwetu kibongobongo tunasema kapigwa kipapai
 
Maradhi ya moyo unakufa huku unajiona.yaani ghafla
Yule sio moyo.Pembeni yake palikuwa na jamaa anamsubiri saa ifike,bahati mbaya imefika na huku anazungumza mambo ya kijinga.Sijui alipoingizwa kwenye gari aliendelea na kauli ile au alibadili nia.
 
Back
Top Bottom