Balozi wa Tanzania nchini Korea akanusha upotoshaji Tanzania kutoa sehemu ya Bahari na Madini

Balozi wa Tanzania nchini Korea akanusha upotoshaji Tanzania kutoa sehemu ya Bahari na Madini

Roving Journalist

JF Roving Journalist
Joined
Apr 18, 2017
Posts
3,984
Reaction score
13,760
balozi.jpg

Balozi wa Tanzania nchini Korea (Jamhuri ya Korea), Balozi Togolani Mavura amekanusha taarifa iliyosambazwa na chombo kimoja cha habari kuwa Tanzania imepokea mkopo toka Jamhuri ya Korea na kutoa sehemu ya bahari na madini.

Kupitia ukurasa wake rasmi wa Mtandao wa X (zamani Twitter), Balozi Mavura amesema taarifa hiyo ina mapungufu makubwa ya kiuandishi, kiuweledi na haiakisi ukweli kwani Tanzania haijasaini Mkataba wowote na Jamhuri ya Korea unaohusu Bahari wala Madini katika ziara ya Rais Samia Suluhu nchini Korea.

“Taarifa hii ina mapungufu makubwa ya kiuandishi, kiuweledi na haiakisi ukweli kwa sababu:

  1. Tanzania haijasaini Mkataba wowote na Jamhuri ya Korea unaohusu Bahari wala Madini katika ziara ya Mheshimiwa Rais Samia Suluhu nchini Korea. Katika ziara hiyo, Rais ameshuhudia utiwaji saini wa Mkataba MMOJA tu ambao ni mkataba wa mkopo wa masharti nafuu wa dola za kimarekani bilioni 2.5 kwa ajili ya miradi ya miundombinu.
Mbali na mkataba huo, Mheshimiwa Rais alishuhudia utiwaji saini wa Hati ya Maelewano (Memorandum of Understanding-MOU) mbili za Ushirikiano katika sekta za Uchumi wa Bluu na Madini ya Kimkakati. Aidha, alishuhudia pia kusainiwa kwa Tamko la Utayari wa Kuanza Majadiliano ya Ushirikiano wa Kiuchumi (Joint Statement on the launch of Negotiation on Economic Partnership Agreement-EPA).

Hivyo, Tanzania na Korea wametiliana saini Mkataba mmoja; MOUs mbili, na Tamko moja.

  1. Tanzania haijagawa chochote kubadilishana na mkopo nafuu kutoka Korea kama ilivyoandika.
    Tanzania inapata mkopo wa masharti nafuu kupitia Mfuko wa Ushirikiano wa Maendeleo (EDCF) kwa mara ya tatu. Mara ya kwanza dola za kimarekani milioni 733 (2014-2020); mara ya pili dola bilioni 1 (2021-2025) na huu mkopo wa tatu ni dola bilioni 2.5 (2024-2028).
Nchi 59 zilizoko barani Afrika, Asia na Ulaya zinafaidika na mkopo wa aina hii kutoka EDCF edcfkorea.go.kr/he/HPHYFE043M01

  1. Tofauti na mlivyoandika, mkopo huu wa masharti nafuu una riba ya asilimia 0.01, unalipwa kwa miaka 40, na una fungate (grace period) ya miaka 25. Yaani unaanza kulipa baada ya mwaka wa 26. Hivyo si kweli kwamba mkopo huo utalipwa kwa miaka 5.
Ni mategemeo yangu kuwa mtakuwa na uungwana wa kurekebisha taarifa hii.”

====

Pia soma:

Ziara ya Rais Samia Korea Kusini atasaini Mkopo wa Tsh. Trilioni 6.51
 
....utiwaji saini wa Hati ya Maelewano (Memorandum of Understanding-MOU) mbili za Ushirikiano katika sekta za Uchumi wa Bluu na Madini ya Kimkakati....
Angetoa ufafanuzi wa tofauti ya MoU na mkataba. Na angefafanua zaidi, nchi hizi mbili Tanzania na Korea ya Kusini zinafaidikaje na MoU?
====
Ufafanuzi huu utarahisisha uelewa mpana wa mambo haya na kuondoa hisia mbaya ya mashirikiano baina ya nchi hizi mbili. Kwa ufupi MoU ingewekwa wazi. Asante.
 
Shida ni moja, Nyinyi mnaficha lakini Wakorea wanayaanika hadharani,, Kwao hawana sera kama yenu ya kufichaficha mambo, Mtu pekee atakayeaminiwa na Wadau ni Serikali ya Korea, ikijitokeza kukanusha kwamba hawajapewa Bahari tutaamini, lakini vinginevyo zitakuwa porojo zilezile za DP WORLD.

Hivi VOA wawasingizie nyinyi ili iweje, kwanza mna nini nyie cha kusingiziwa nacho kipya wakati KIA mmeuza na Ngorongoro nayo mmeuza ?

MUNGU WABARIKI WAZUNGU
 
Hivi hii mikataba ina siri gani? Mtu anajitokeza kukanusha kuwa hauhusiani na madini wala bandari bali ni mkataba wa MASHARTI NAFUU halafu hayo masharti hayataji ni yapi.

Huu upuuzi utaendelea mpaka lini? Wanaficha nini mbona hayo masharti nafuu hawayaweki wazi?
 
"Mara ya kwanza dola za kimarekani milioni 733 (2014-2020); mara ya pili dola bilioni 1 (2021-2025) na huu mkopo wa tatu ni dola bilioni 2.5 (2024-2028)"

Swali: Kwanini tusaini awamu ya tatu ikiwa ya pili bado haijaisha?
😆😆😆😆😆
 
Balozi wa Tanzania nchini Korea (Jamhuri ya Korea), Balozi Togolani Mavura amekanusha taarifa iliyosambazwa na chombo kimoja cha habari kuwa Tanzania imepokea mkopo toka Jamhuri ya Korea na kutoa sehemu ya bahari na madini.

Kupitia ukurasa wake rasmi wa Mtandao wa X (zamani Twitter), Balozi Mavura amesema taarifa hiyo ina mapungufu makubwa ya kiuandishi, kiuweledi na haiakisi ukweli kwani Tanzania haijasaini Mkataba wowote na Jamhuri ya Korea unaohusu Bahari wala Madini katika ziara ya Rais Samia Suluhu nchini Korea.

“Taarifa hii ina mapungufu makubwa ya kiuandishi, kiuweledi na haiakisi ukweli kwa sababu:

  1. Tanzania haijasaini Mkataba wowote na Jamhuri ya Korea unaohusu Bahari wala Madini katika ziara ya Mheshimiwa Rais Samia Suluhu nchini Korea. Katika ziara hiyo, Rais ameshuhudia utiwaji saini wa Mkataba MMOJA tu ambao ni mkataba wa mkopo wa masharti nafuu wa dola za kimarekani bilioni 2.5 kwa ajili ya miradi ya miundombinu.
Mbali na mkataba huo, Mheshimiwa Rais alishuhudia utiwaji saini wa Hati ya Maelewano (Memorandum of Understanding-MOU) mbili za Ushirikiano katika sekta za Uchumi wa Bluu na Madini ya Kimkakati. Aidha, alishuhudia pia kusainiwa kwa Tamko la Utayari wa Kuanza Majadiliano ya Ushirikiano wa Kiuchumi (Joint Statement on the launch of Negotiation on Economic Partnership Agreement-EPA).

Hivyo, Tanzania na Korea wametiliana saini Mkataba mmoja; MOUs mbili, na Tamko moja.

  1. Tanzania haijagawa chochote kubadilishana na mkopo nafuu kutoka Korea kama ilivyoandika.
    Tanzania inapata mkopo wa masharti nafuu kupitia Mfuko wa Ushirikiano wa Maendeleo (EDCF) kwa mara ya tatu. Mara ya kwanza dola za kimarekani milioni 733 (2014-2020); mara ya pili dola bilioni 1 (2021-2025) na huu mkopo wa tatu ni dola bilioni 2.5 (2024-2028).
Nchi 59 zilizoko barani Afrika, Asia na Ulaya zinafaidika na mkopo wa aina hii kutoka EDCF edcfkorea.go.kr/he/HPHYFE043M01

  1. Tofauti na mlivyoandika, mkopo huu wa masharti nafuu una riba ya asilimia 0.01, unalipwa kwa miaka 40, na una fungate (grace period) ya miaka 25. Yaani unaanza kulipa baada ya mwaka wa 26. Hivyo si kweli kwamba mkopo huo utalipwa kwa miaka 5.
Ni mategemeo yangu kuwa mtakuwa na uungwana wa kurekebisha taarifa hii.”

Kama ni WAKWELI watuwekee mkataba hadharani.

Sheria ya JPM inawataka wapeleke mikataba Bungeni lakini wao wameamua kupindisha sheria wanajifanyia yao kinyume cha sheria.
 
Hatujaingia mkataba serikali imesaini MoU mbili tu.

Sasa MoU na yenyewe si mkataba ukijitoa unaweza shitakiwa.

Huko baharini nani anakagua hizo meli, zikija wanavua hao wanaondoka juu kwa juu.

Billioni 2.5 kitu gani kama na wao labda wanajivulia wanavyotaka kwa miaka 25 bila ya kukaguliwa.

Kwa sasa ukweli wenyewe kupewa kibali cha kuvua maana samaki wanajifia kama nchi hatuvuni samaki commercially kama wenzetu wacha wachukue tu.

Shida ni pale watanzania wakiamka na kuanza kuitumia bahari vilivyo na kuanza kugombania kitowoe na wakorea.
 
Hivi tunayojeuri ya kumsimanga Ndugu yetu wa wakati huo wa " Msovero" kweli?
Binafsi sioni shida kuwapa watu kibali cha kuvua as far as commercial fishing is concerned.

Uvuvi wenyewe wa mitumbwi wakati samaki wamejazana baharini wacha wengine wachukue, kwa usingizi wetu.

Shida ni huko mbele watanzania wakiamka na kuanza commercial fishing, hapo sasa ndio inaweza kuwa mgogoro.

Kwa sasa tuwe wakweli tu we are not exploiting the ocean kwa mipaka yetu, wacha wenye uwezo wajibebe tu kama kuna utaratibu mzuri wa ukaguzi.
 
Wa Tanzania humu ukiwasikiliza utasema hii nchi tajiri sana haina shida na mikopo wakati sisi majumbani mwetu tumejawa na mikopo mpaka Vicoba na sasa tumehamia kausha damu. Tanzania bila mikopo haiwezekani na sababu nyepesi tu, makusanyo yetu hayatoshi kuongeza mishahara tu hatuwezi uwezo mdogo sembuse kujenga miundo mbinu? au miradi ya maendeleo. Kama hutaki mkopo ni kuishi kwa uwezo wako na huko ina maana miradi mingi itakufa na uchumi ndio bye bye.

Nchi inahitaji kuzalisha sana, uza sana lakini hatuongelei mambo kama haya tuko busy mikopo, mikopo iko kisheria na wala haijaanza leo toka tunapata uhuru tunakopa tu, kiujumla nchi zote za Africa. Juzi juzi tu Egypt waliokolewa na UAE kupewa billion 35 Billion$ nasema tena 35 sio 2.5 tuyaopiga kelele.
 
Back
Top Bottom