Balozi wa Tanzania nchini Korea akanusha upotoshaji Tanzania kutoa sehemu ya Bahari na Madini

Balozi wa Tanzania nchini Korea (Jamhuri ya Korea), Balozi Togolani Mavura amekanusha taarifa iliyosambazwa na chombo kimoja cha habari kuwa Tanzania imepokea mkopo toka Jamhuri ya Korea na kutoa sehemu ya bahari na madini.

Kupitia ukurasa wake rasmi wa Mtandao wa X (zamani Twitter), Balozi Mavura amesema taarifa hiyo ina mapungufu makubwa ya kiuandishi, kiuweledi na haiakisi ukweli kwani Tanzania haijasaini Mkataba wowote na Jamhuri ya Korea unaohusu Bahari wala Madini katika ziara ya Rais Samia Suluhu nchini Korea.

“Taarifa hii ina mapungufu makubwa ya kiuandishi, kiuweledi na haiakisi ukweli kwa sababu:

  1. Tanzania haijasaini Mkataba wowote na Jamhuri ya Korea unaohusu Bahari wala Madini katika ziara ya Mheshimiwa Rais Samia Suluhu nchini Korea. Katika ziara hiyo, Rais ameshuhudia utiwaji saini wa Mkataba MMOJA tu ambao ni mkataba wa mkopo wa masharti nafuu wa dola za kimarekani bilioni 2.5 kwa ajili ya miradi ya miundombinu.
Mbali na mkataba huo, Mheshimiwa Rais alishuhudia utiwaji saini wa Hati ya Maelewano (Memorandum of Understanding-MOU) mbili za Ushirikiano katika sekta za Uchumi wa Bluu na Madini ya Kimkakati. Aidha, alishuhudia pia kusainiwa kwa Tamko la Utayari wa Kuanza Majadiliano ya Ushirikiano wa Kiuchumi (Joint Statement on the launch of Negotiation on Economic Partnership Agreement-EPA).

Hivyo, Tanzania na Korea wametiliana saini Mkataba mmoja; MOUs mbili, na Tamko moja.

  1. Tanzania haijagawa chochote kubadilishana na mkopo nafuu kutoka Korea kama ilivyoandika.
    Tanzania inapata mkopo wa masharti nafuu kupitia Mfuko wa Ushirikiano wa Maendeleo (EDCF) kwa mara ya tatu. Mara ya kwanza dola za kimarekani milioni 733 (2014-2020); mara ya pili dola bilioni 1 (2021-2025) na huu mkopo wa tatu ni dola bilioni 2.5 (2024-2028).
Nchi 59 zilizoko barani Afrika, Asia na Ulaya zinafaidika na mkopo wa aina hii kutoka EDCF edcfkorea.go.kr/he/HPHYFE043M01

  1. Tofauti na mlivyoandika, mkopo huu wa masharti nafuu una riba ya asilimia 0.01, unalipwa kwa miaka 40, na una fungate (grace period) ya miaka 25. Yaani unaanza kulipa baada ya mwaka wa 26. Hivyo si kweli kwamba mkopo huo utalipwa kwa miaka 5.
Ni mategemeo yangu kuwa mtakuwa na uungwana wa kurekebisha taarifa hii.”

====

Pia soma:

Ziara ya Rais Samia Korea Kusini atasaini Mkopo wa Tsh. Trilioni 6.51

Mimi swali langu ni ... Kwa nini wanataka tuwaamini wao wakati hawajawahi kuwa wakeli hata siku moja....!!?
 
Ngoja nkija tulia ntambana classmate wangu huyu balozi
😄

Ova
 
Angetoa ufafanuzi wa tofauti ya MoU na mkataba. Na angefafanua zaidi, nchi hizi mbili Tanzania na Korea ya Kusini zinafaidikaje na MoU?
====
Ufafanuzi huu utarahisisha uelewa mpana wa mambo haya na kuondoa hisia mbaya ya mashirikiano baina ya nchi hizi mbili. Kwa ufupi MoU ingewekwa wazi. Asante.
Unampangia sio?
 
Binafsi sioni shida kuwapa watu kibali cha kuvua as far as commercial fishing is concerned.

Uvuvi wenyewe wa mitumbwi wakati samaki wamejazana baharini wacha wengine wachukue, kwa usingizi wetu.

Shida ni huko mbele watanzania wakiamka na kuanza commercial fishing, hapo sasa ndio inaweza kuwa mgogoro.

Kwa sasa tuwe wakweli tu we are not exploiting the ocean kwa mipaka yetu, wacha wenye uwezo wajibebe tu kama kuna utaratibu mzuri wa ukaguzi.
Ingieni kwenye commercial fishing
Jamani 😄
Au watanzania mnaishia kwenye uwekezaji wa biashara za maframe,bar,miziki

Ova
 
Balozi wa Tanzania nchini Korea (Jamhuri ya Korea), Balozi Togolani Mavura amekanusha taarifa iliyosambazwa na chombo kimoja cha habari kuwa Tanzania imepokea mkopo toka Jamhuri ya Korea na kutoa sehemu ya bahari na madini.

Kupitia ukurasa wake rasmi wa Mtandao wa X (zamani Twitter), Balozi Mavura amesema taarifa hiyo ina mapungufu makubwa ya kiuandishi, kiuweledi na haiakisi ukweli kwani Tanzania haijasaini Mkataba wowote na Jamhuri ya Korea unaohusu Bahari wala Madini katika ziara ya Rais Samia Suluhu nchini Korea.

“Taarifa hii ina mapungufu makubwa ya kiuandishi, kiuweledi na haiakisi ukweli kwa sababu:

  1. Tanzania haijasaini Mkataba wowote na Jamhuri ya Korea unaohusu Bahari wala Madini katika ziara ya Mheshimiwa Rais Samia Suluhu nchini Korea. Katika ziara hiyo, Rais ameshuhudia utiwaji saini wa Mkataba MMOJA tu ambao ni mkataba wa mkopo wa masharti nafuu wa dola za kimarekani bilioni 2.5 kwa ajili ya miradi ya miundombinu.
Mbali na mkataba huo, Mheshimiwa Rais alishuhudia utiwaji saini wa Hati ya Maelewano (Memorandum of Understanding-MOU) mbili za Ushirikiano katika sekta za Uchumi wa Bluu na Madini ya Kimkakati. Aidha, alishuhudia pia kusainiwa kwa Tamko la Utayari wa Kuanza Majadiliano ya Ushirikiano wa Kiuchumi (Joint Statement on the launch of Negotiation on Economic Partnership Agreement-EPA).

Hivyo, Tanzania na Korea wametiliana saini Mkataba mmoja; MOUs mbili, na Tamko moja.

  1. Tanzania haijagawa chochote kubadilishana na mkopo nafuu kutoka Korea kama ilivyoandika.
    Tanzania inapata mkopo wa masharti nafuu kupitia Mfuko wa Ushirikiano wa Maendeleo (EDCF) kwa mara ya tatu. Mara ya kwanza dola za kimarekani milioni 733 (2014-2020); mara ya pili dola bilioni 1 (2021-2025) na huu mkopo wa tatu ni dola bilioni 2.5 (2024-2028).
Nchi 59 zilizoko barani Afrika, Asia na Ulaya zinafaidika na mkopo wa aina hii kutoka EDCF edcfkorea.go.kr/he/HPHYFE043M01

  1. Tofauti na mlivyoandika, mkopo huu wa masharti nafuu una riba ya asilimia 0.01, unalipwa kwa miaka 40, na una fungate (grace period) ya miaka 25. Yaani unaanza kulipa baada ya mwaka wa 26. Hivyo si kweli kwamba mkopo huo utalipwa kwa miaka 5.
Ni mategemeo yangu kuwa mtakuwa na uungwana wa kurekebisha taarifa hii.”

====

Pia soma:

Ziara ya Rais Samia Korea Kusini atasaini Mkopo wa Tsh. Trilioni 6.51
Kelele kibao hakuna la maana alilosema huyu Balozi. Samia anauza nchi huyu.mtu.
 
Ingieni kwenye commercial fishing
Jamani 😄
Au watanzania mnaishia kwenye uwekezaji wa biashara za maframe,bar,miziki

Ova
Ndio mambo tunayoyaweza imagine vyuo vyote hivi wanafunzi soko kubwa sana jumlisha na bachelors wa mtaa. Huku Tuna wamejaa baharini hakuna wavuvi.

Watanzania wenye akili ya kuvua samaki wenye stake na kuweka kwenye makopo na ku-target ilo soko. Huo muda hawana vijana huko vyuo wanashindia zege.

Bado huko kwenye mboga mboga, mbaazi mpaka India anunue wakati machine ndogo (pressure cooker) ya kuchemshia vitu kama maharage na jamii zingine za kunde haizidi hata $20,000 AliBaba. Unawachemshia mboga unawawekea kwenye makopo wanafunzi na ma-bachelor wanaunga mboga kwa dakika tano tu.

Watanzania wanachojua ni mabasi, bar, maduka, kujenga na kufanya kazi na serikali wakati nchi ina fursa kibao za kutengeneza hela nyingi tu kwenye sector ya uzalishaji.

Wacha wengine watumie tu hizo fursa mradi kuna usimamizi mzuri.
 
Balozi wa Tanzania nchini Korea (Jamhuri ya Korea), Balozi Togolani Mavura amekanusha taarifa iliyosambazwa na chombo kimoja cha habari kuwa Tanzania imepokea mkopo toka Jamhuri ya Korea na kutoa sehemu ya bahari na madini.

Kupitia ukurasa wake rasmi wa Mtandao wa X (zamani Twitter), Balozi Mavura amesema taarifa hiyo ina mapungufu makubwa ya kiuandishi, kiuweledi na haiakisi ukweli kwani Tanzania haijasaini Mkataba wowote na Jamhuri ya Korea unaohusu Bahari wala Madini katika ziara ya Rais Samia Suluhu nchini Korea.

“Taarifa hii ina mapungufu makubwa ya kiuandishi, kiuweledi na haiakisi ukweli kwa sababu:

  1. Tanzania haijasaini Mkataba wowote na Jamhuri ya Korea unaohusu Bahari wala Madini katika ziara ya Mheshimiwa Rais Samia Suluhu nchini Korea. Katika ziara hiyo, Rais ameshuhudia utiwaji saini wa Mkataba MMOJA tu ambao ni mkataba wa mkopo wa masharti nafuu wa dola za kimarekani bilioni 2.5 kwa ajili ya miradi ya miundombinu.
Mbali na mkataba huo, Mheshimiwa Rais alishuhudia utiwaji saini wa Hati ya Maelewano (Memorandum of Understanding-MOU) mbili za Ushirikiano katika sekta za Uchumi wa Bluu na Madini ya Kimkakati. Aidha, alishuhudia pia kusainiwa kwa Tamko la Utayari wa Kuanza Majadiliano ya Ushirikiano wa Kiuchumi (Joint Statement on the launch of Negotiation on Economic Partnership Agreement-EPA).

Hivyo, Tanzania na Korea wametiliana saini Mkataba mmoja; MOUs mbili, na Tamko moja.

  1. Tanzania haijagawa chochote kubadilishana na mkopo nafuu kutoka Korea kama ilivyoandika.
    Tanzania inapata mkopo wa masharti nafuu kupitia Mfuko wa Ushirikiano wa Maendeleo (EDCF) kwa mara ya tatu. Mara ya kwanza dola za kimarekani milioni 733 (2014-2020); mara ya pili dola bilioni 1 (2021-2025) na huu mkopo wa tatu ni dola bilioni 2.5 (2024-2028).
Nchi 59 zilizoko barani Afrika, Asia na Ulaya zinafaidika na mkopo wa aina hii kutoka EDCF edcfkorea.go.kr/he/HPHYFE043M01

  1. Tofauti na mlivyoandika, mkopo huu wa masharti nafuu una riba ya asilimia 0.01, unalipwa kwa miaka 40, na una fungate (grace period) ya miaka 25. Yaani unaanza kulipa baada ya mwaka wa 26. Hivyo si kweli kwamba mkopo huo utalipwa kwa miaka 5.
Ni mategemeo yangu kuwa mtakuwa na uungwana wa kurekebisha taarifa hii.”

====

Pia soma:

Ziara ya Rais Samia Korea Kusini atasaini Mkopo wa Tsh. Trilioni 6.51
Sawa
 
Back
Top Bottom