Securelens
JF-Expert Member
- Sep 28, 2020
- 316
- 541
Katika taarifa ya habari ya Channel 10 ya usiku wa jana tarehe 20 Novemba 2020, Balozi wa Tanzania nchini Ubelgiji na Mwakilishi wa Tanzania kwenye Umoja wa Ulaya Mhe Jestas Abuok Nyamanga ameeleza kuwa siku ya tarehe 19 Nov alimwandikia barua Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Mambo ya Nje ya Umoja wa Ulaya Mhe David Mc Allister kumwomba apewe nafasi ya kutoa ufafanuzi kwa Mwenyekiti huyo na Kamati yake dhidi ya taarifa mbalimbali za upotoshaji. Ameeleza kwenye mahojiano hayo na Channel 10 kuwa jana tarehe 20 Nov, Mwenyekiti huyo alimjibu na kukubali kukutana naye na kwamba atampangia tarehe.
My take:
Kila uongo wanaotengeneza na wana Ufipa unazidi kubainika ndani na nje ya nchi. Ama kweli njia ya mwongo ni fupi
My take:
Kila uongo wanaotengeneza na wana Ufipa unazidi kubainika ndani na nje ya nchi. Ama kweli njia ya mwongo ni fupi