Miss Zomboko
JF-Expert Member
- May 18, 2014
- 4,599
- 9,532
Maafisa nchini Myanmar awamemkamata balozi wa zamani wa Uingereza nchini humo na mumewe, mchoraji maarufu ambaye wakati mmoja aliwahi kuwa mfungwa wa kisiasa. Utawala wa kijeshi wa Myanamr umesema wanatuhumiwa kwa kukiuka sheria za uhamiaji.
Vicky Bowman, ambaye alihudumu kama balozi kuanzia mwaka wa 2002 hadi 2006, alikamatwa kwa kushindwa kuzifahamisha mamlaka kuwa anaishi sehemu tofauti na iliyoorodheshwa kwenye cheti chake cha usajili wa wageni.
Taarifa hiyo ya jeshi imeongeza kuwa mumewe balozi huyo wa zamani, Htein Lin alikamatwa kwa kumsaidia mkewe kuishi katika makazi tofauti na yaliyosajiliwa katika mji wa kibiashara wa Yangon. Msemaji wa ubalozi wa Uingereza mjini Yangon amesema wana wasiwasi na kukamatwa kwa mwanamke wa Uingereza nchini Myanmar, bila kulitaja jina la Bowman.