Habari za Zanzibar
JF-Expert Member
- Dec 18, 2024
- 651
- 433
BALOZI YAKUBU: USHIRIKI WA MATAIFA 16 WAONESHA KUKUA KWA HADHI YA KISWAHILI DUNIANI
Balozi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Daudi Yakubu, amesema ushiriki wa mataifa 16 katika Kongamano la Pili la Kimataifa la Kiswahili unaonesha kuongezeka kwa hadhi na umuhimu wa lugha ya Kiswahili katika medani za kimataifa.
Balozi Yakubu alitoa kauli hiyo wakati wa ufunguzi wa Kongamano hilo lililofanyika jijini Paris, Ufaransa, Julai 7, 2026, akieleza kuwa idadi kubwa ya nchi zinazoshiriki ni ishara ya kutambuliwa kwa mchango wa Kiswahili katika kuimarisha diplomasia, elimu, utamaduni na mawasiliano ya kimataifa.
Amesema kongamano hilo limewakutanisha viongozi wa serikali, wanadiplomasia, wasomi, wataalamu wa lugha pamoja na wadau mbalimbali wa Kiswahili kutoka sehemu tofauti duniani, kwa lengo la kujadili mikakati ya kuendeleza matumizi, ufundishaji na ukuzaji wa lugha hiyo katika ngazi ya kimataifa.
Balozi Yakubu amesisitiza kuwa Kiswahili kimeendelea kuwa daraja la kuunganisha jamii mbalimbali, kukuza uelewa wa tamaduni na kuimarisha ushirikiano miongoni mwa mataifa.
Ameongeza kuwa Tanzania itaendelea kushirikiana na wadau wa ndani na wa kimataifa kuhakikisha Kiswahili kinapata nafasi stahiki duniani, huku kikitumika kama chombo cha kukuza mshikamano, amani na mahusiano mazuri kati ya mataifa.