Baltasar Engonga akabiliwa na kifungo cha miaka 18 kwa Ubadhirifu na Ufisadi, Equatorial Guinea

Baltasar Engonga akabiliwa na kifungo cha miaka 18 kwa Ubadhirifu na Ufisadi, Equatorial Guinea

Richer

JF-Expert Member
Joined
Jun 9, 2025
Posts
2,318
Reaction score
4,079
Aliyekuwa Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Kitaifa la Uchunguzi wa Fedha la Equatorial Guinea, Baltasar Engonga Ebang, amehukumiwa kifungo cha miaka 18 jela kwa ubadhirifu wa zaidi ya Sh milioni 230 za serikali

Kwa mujibu wa ripoti za vyombo vya habari nchini humo, Engonga alijipatia Sh milioni 209.3 ambazo nyingi zilidaiwa kutumika katika maisha ya kifahari, wakiwemo wanawake na anasa nyinginezo za kibinafsi

Kesi hiyo, iliyoanza siku ya Jumatatu, pia ilihusisha maafisa kadhaa wa zamani wa shirika la umma ambapo Waendesha mashitaka walisema mpango wa ubadhirifu uliratibiwa na Engonga wakati akiwa Mkurugenzi mkuu kati ya 2015 na 2020

Upande wa mashtaka ulitaka apewe adhabu kali ikiwemo miaka nane kwa ubadhirifu, miaka minne na miezi mitano kwa kujitajirisha na miaka sita na siku moja kwa matumizi mabaya ya mamlaka

Maafisa wengine sita wakuu, miongoni mwao Carmelo Julio Matogo Ndong, Ireneo Mangue Monsuy Afana, na Florentina Iganga Iñandji, pia wanakabiliwa na kesi kuhusiana na kile ambacho mamlaka imekielezea kuwa mtandao mkubwa wa ufisadi wa kifedha

Soma pia:


Mnamo Novemba 2024, Engonga alikumbwa na kashfa zaidi baada ya kanda nyingi za video chafu kusambaa mtandaoni, zikiripotiwa zikimuonyesha akifanya ngono na zaidi ya wanawake 40

Kanda hiyo, iliyosambazwa sana kwenye mitandao ya kijamii, ilifichua matukio yanayodaiwa kurekodiwa ofisini kwake, katika hoteli, vyoo, na hata kando ya mto

Wanawake wengi walitambuliwa kuwa wake za maafisa wakuu wa serikali, wanafamilia, na wasaidizi wake wa kibinafsi ambapo Engonga, anadaiwa kuwa baba wa watoto sita na anasemekana kurekodi zaidi ya video 400 za ngono

Kufuatia ufichuzi huo, Rais Teodoro Obiang Nguema Mbasogo alimteua Zenón Obiang Obiang Avomo kuwa Mkurugenzi Mkuu mpya wa wakala wa fedha Kisha serikali iliendelea kumfungulia mashtaka Engonga kwa utovu wa nidhamu unaohusiana na kashfa ya mkanda wa ngono, pamoja na uhalifu wa kifedha

===

Baltasar Engonga, the former director-general of Equatorial Guinea’s National Financial Investigation Agency (ANIF), has been held at Black Beach prison since September 2024, after being charged with embezzlement of public funds along with several other former senior officials. The prosecution on Monday outlined what they described as an elaborate scheme to siphon off public funds for personal use, allegedly orchestrated by Engonga in collusion with other top officials in the Directorate General of Insurance and Reinsurance (DGAR), which he led between 2015 and 2020

The national prosecutor has requested an exceptionally heavy sentence: 8 years in prison for embezzlement of public funds, 4 years and 5 months for illicit enrichment, and 6 years and 1 day for abuse of office. The charges also carry a proposed fine exceeding 910 million CFA francs (about 1.5 million USD) and a ban on holding public office for the duration of the sentence


1751539050384.jpeg

​
Source: LEBLEDPARLE.COM
 
P DIDY na unyama wake wote bado hamfikii huyu mwamba......hii ni habari nyingine duniani
 
Yaani ufisadi wa Tsh 230M? Mbona pesa ndogo sana hiyo? Bongo hapa hizo si ni sent tu? I'm sure, kashfa ni ile ile ya wale wanawake
 
Jamaa alipita nao wengi sana, watamfata mbaka gerezani sio bure
 
Back
Top Bottom