Bambo aomba msaada

Bambo aomba msaada

Siamini kama kweli EAT wameshindwa kumsaidia labda mabosi hawajapata taarifa rasmi,duuuh.
Pole bambo yooote wamesahau.
 
sidhani kama Bambo amekurupuka kwenda kulisema hili ktk radio tena live, maana huenda alishapeleka taarifa kwa uongizi husika kilio chake hakikusikilizwa, maana mpaka mtu mzima unajitokeza hadharani basi mambo yamebana kweli, so tujitahidi kumsaidia mwenzetu, lakini hata umoja wa wasanii nao wamekosa fungu la kumtoa mwenzao Muhimbili? au wameshindwa kuchangishana hela kumtoa mwenzao hospital? ok Mr. Bambo tupe A/C # yako au ur phone # lakini uwe ni wewe kweli siyo tunakupigia simu harafu anapokea msaidizi tena hatutatoa hela, maana Bongo hii kuna namna nyingi za kujitafutia kipato,
 
Tusikimbilie kumlaumu Mengi!..Mnajua mahusiano yao currently(Bambo na EATV) yalivyo?
Kama ni mwajiriwa ni lazima angekuwa na haki ya matibabu!...
BILI HIYO ya kumshinda Mengi ni shiing ngapi..inafika 500K?
Acheni hizo!
 
Mambo si anafanya kazi EATV hiyo bill ni kubwa kiasi gani mpaka mwajiri kama EATV atembeze bakuli?
 
Bosi masifa mengi.akitoa hata shilingi kumi atajitangaza mpaka kwenye taarifa ya habari.ila haiingi kichwani sidhani kama jamaa kashindwa kulipa.
 
Alisema kawekwa chuma mguuni na atakuwa on wheel chair kwa miezi 6.
muhimbili wamemruhusu akaugulie home.Likini mpaka alipe deni lote.
Mtanga alikuwa naye alipo hojiwa akasema watu wajitokeze kumsaidia.
 
Kwani mkataba wake wa kazi hauhusiani na masuala ya afya ya mfanyakazi?
 
Du ukiona mtoto wako anajifanya anataka kuwa msanii mkataze kwa nguvu zote usanii bongo haulipi, hata wapiga debe wanaweza kukichanga hadi laki kwa siku.
 
Kuna kampuni moja binafsi hujifanya kuajiri watu kama vibarua ili kukwepa gharama kama hizi,inabidi kutizama vyema..pole mzee wa magumashi tutakumic
 
mmmh! mbona kama siamini vile,
kweli EATV wameshindwa kumlipia bambo bill yake????,
au kuna mahali sijaelewa vizuri? hiyo bill ni sh ngapi hasa mpaka EATV iwashinde?
 
Jamani, Zembwela ni msanii mchekeshaji aliyegeukia tasnia ya utangazaji na Bambo bado ni full time msanii mchekeshaji.

Isije ikawa wanaendeleza uchekeshaji.

Ila, kama kweli kashindwa kulipa bill ya utabibu, hapa pana tatizo. Mkataba wake pale EATV ni full time employment au vinginevyo?

Hapa ndo mantiki ya Mh. Mbilinyi ya kupiga marufuku fiesta kwake Mbeya ina click - wasanii hawafaidiki na kazi zao, wananyonywa.

Bambo hauko covered na bima yoyote ya afya?
Hulipwi kazi zako unazofanya? Hii sasa ina maana hata wasanii hawako kwenye mfuko wowote wa pensheni. Nawashauri wamfuate Mh. Sugu ka ushauri.
 
Haikuwa uchekeshaji,Mtanga,Bambo alikuwepo pia.Na jana (jumatano )Kibonde alizungumzia 12.40 jioni akasema,pls Bambo ana itaji msaada
mwenye nafasi aende muhimbili kwa nia ya kumsaidia sio kumkejeli.
Mara ya kwanza huyo bin adam kaongea upendo na ukweli (Plssss simfagilii kibonde ila kajitahidi kuwa na hisia kama wana jamii)
Utavua gamba au?
 
Wasanii wa kibongo wakati wanapata ela wanakimbilia kutakasa nyota (kunywa mipombe kwa fuso na kushindilia vitimoto visivopimwa na TBS) na kusahau kuna ya kesho na kesho kutwa.
 
eatv wahuni tu hao, mwenyewe anajifanya kuwapenda yatima, masikini nk halafu anashindwa kumtibia huyo Bambo? shame on you unajijua mwenyewe.
 
Duuuh! kweli kama ni fani muulize BISHANGA BISHAIJA
sanaa ya bongo kwa wasanii haina faida!!!!!
 
msiniambie wiki hii mzee wa magumashi hatakuwepo hewani bana,
lakini kwani kwenye mshahara au posho wanayopewa huwa haitoshi ikabaki ya kuhifadhi kwa dharula kama hizi?
pia watanzania tujifunze na tuaze kujiandikisha kwenye mifuko ya hifadhi za jamii ambayo huwa inatoa msaada wa matibabu, kwa mfano mfuko wa bima ya afya,nssf,na mingine,unachangia mara moja tu kwa mwaka,inakuja kukufaa siku umeugua na mfukoni huna kitu.
 
Leo asubuhi alikuwa live kwenye east africa radio,akihojiwa na zembwela.
Alsema muhimbili wamemzuia kutoka hospitali kwa sababu anadaiwa hela
nyingi kwa ajili ya oparesheni ya mguu.kwa hiyo anaomba jamii kumsaidia.
Mimi nilidhani ni mwajiriwa wa etv au nipo wrong?

Na mashaka na hili na kama kweli mahojiano hayo yamefanyika EATV Radio haya ni matusi ya nguoni kwa mzee Mengi, alivyo mahiri na karima kwa kusaidia watanzania. Hawa jamaa watakuwa wamemkosea sana kama wamefanya hivyo. Siamini kama wamemkonsult na amekataa kuwasaidia.
 
Back
Top Bottom