Waufukweni
JF-Expert Member
- May 16, 2024
- 5,383
- 18,776
Katibu wa Siasa na Uenezi wa CCM Mkoa wa Dar es Salaam, Ally Bananga, amesema CHADEMA ya Freeman Mbowe ilikuwa bora zaidi kuliko ilivyo sasa, akimtaja Mbowe kuwa kiongozi mwenye uwezo wa kupunguza presha za kisiasa na kuweka maslahi ya taifa mbele.
Akizungumza katika mahojiano na East Africa Radio Juni 19, 2026, Bananga amesema: "The man is humble. Freeman anajua kupunguza presha. Mwaka 2015, baada ya Mheshimiwa Lowassa kugombea urais, kila mmoja alijua watu wataenda barabarani, but the man was a resistor. Aliweka mambo chini. Hata 2020, hata 2010, Freeman amekuwa mtu wa mwisho kuongea kauli ngumu. Na ukimwona anazungumza jambo gumu, ujue limefika mwisho. That's the type of leader tunatamani kuona. Anaibeba nchi zaidi kuliko mhemko."
Bananga aliongeza kuwa viongozi wanapaswa kuwa waangalifu na kauli wanazozitoa kwa kuwa zina uzito mkubwa kwa umma. "Na ninarudia; kauli zetu sisi hata kama unaongea umelewa, watu wanazinukuu zilivyo. Tuogope kutumia midomo yetu kuligawa taifa," alisema.