Bananga: CHADEMA ya Freeman Mbowe ni bora zaidi kuliko hii, Mbowe anajua kupunguza presha

Waufukweni

JF-Expert Member
Joined
May 16, 2024
Posts
5,383
Reaction score
18,776
Katibu wa Siasa na Uenezi wa CCM Mkoa wa Dar es Salaam, Ally Bananga, amesema CHADEMA ya Freeman Mbowe ilikuwa bora zaidi kuliko ilivyo sasa, akimtaja Mbowe kuwa kiongozi mwenye uwezo wa kupunguza presha za kisiasa na kuweka maslahi ya taifa mbele.

Akizungumza katika mahojiano na East Africa Radio Juni 19, 2026, Bananga amesema: "The man is humble. Freeman anajua kupunguza presha. Mwaka 2015, baada ya Mheshimiwa Lowassa kugombea urais, kila mmoja alijua watu wataenda barabarani, but the man was a resistor. Aliweka mambo chini. Hata 2020, hata 2010, Freeman amekuwa mtu wa mwisho kuongea kauli ngumu. Na ukimwona anazungumza jambo gumu, ujue limefika mwisho. That's the type of leader tunatamani kuona. Anaibeba nchi zaidi kuliko mhemko."

Bananga aliongeza kuwa viongozi wanapaswa kuwa waangalifu na kauli wanazozitoa kwa kuwa zina uzito mkubwa kwa umma. "Na ninarudia; kauli zetu sisi hata kama unaongea umelewa, watu wanazinukuu zilivyo. Tuogope kutumia midomo yetu kuligawa taifa," alisema.

Your browser is not able to display this video.
 
Mtu yuko ccm atasemaje,hata Msigwa angetetea tu kama bado angekuwa huko
 
Vipi mbona wako busy na Chadema ambayo sio bora unawezaje kupoteza mda kujadili kitu ambacho sio bora tuseme bora ni ACT au Chaumma kwanini hawajadili ivyo vyama ambavyo ni bora
 
"Ukiona umesifiwa jua umeumia" hvo Mbowe kisha umia..Kama Mbowe aliongoza vizuri mbona Hata Uwaziri Hakupewa? Hiyo danganya toto.
 
Si huyu huyu aliondoka kipindi Cha mbowe halafu analeta tantalila, machawa tukiwambia akili zenu kama nguruwe anayeweza kula mavi yake muwe mnatuelewa.
 
Jiwe limewapata sasa😅
 
Ninyi manyang'au wa CCM hadi lini mtaendelea kumlilia Mbowe? Kitendea kazi chenu mlichotumia kupoozesha mageuzi ya kweli kimekataliwa na wenye chama chao, kubalini kuwa Chadema ya sasa ndiye mkombozi wa kweli wa wana wa nchi hii, kama kusoma hamjui hata picha ya umma unaoiunga mkono Chadema hamuuoni?
 
Huyu wakuitwa bananga ametoka wapi tena! ?
Mzee wa kubananga akiwa Chadema alikuwa anafugwa na mkewe aliyekuwa mbunge wa CCM, baada ya watu kumgutukia kuwa anauza ramani ya vita ndiyo naye akajipeleka huko huko CCM.
 
Ukiona adui yako anakukosoa sana ujue anakuogopa hana aman anatengeneza taharuk

BANANGA WATANZANIA WA LEO SIYO WALE WA 1990< SI MLISEMA 29/10 HATAONEKANA MTU LEO VIPI?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…