Bandari, ardhi, misitu na maliasili zetu, ni Mali ya URITHI, hazitauzwa wala kukodishwa kwa wageni, kataa wahuni

Bandari, ardhi, misitu na maliasili zetu, ni Mali ya URITHI, hazitauzwa wala kukodishwa kwa wageni, kataa wahuni

Rabbon

JF-Expert Member
Joined
Apr 16, 2022
Posts
21,625
Reaction score
33,688
Salaam, Shalom!!

Kuna uteuzi ulifanyika siku ya kusaini mkataba BATILI wa kukodisha URITHI wetu, Bandari Kwa wageni.

Uteuzi huo umekuja na wimbi la Matukio ya kutengeneza wenye Nia ya kutusahaulisha wanaukoo juu ya kilichofanyika.

Jambo muhimu juu ya nini Hasa kilisainiwa kwenye mkataba Ule kimebaki kuwa Siri, Viongozi wetu wa kiimani wamejaribu mara kadhaa kuomba mikataba hiyo Ili waisome na kujiridhisha ikiwa Issues zilizokuwa zikipigiwa kelele zimefanyiwa KAZI au la!!

Nyumisi amehoji kuwa, waziri Mbarawa na watetezi wa DP World,walidai kuwa DP World wakipewa mkataba, Serikali itapunguza utegemezi wa kukopa nje, kwamba DP World wataleta pesa nyingi, iweje tena Serikali ikope Trilion SITA kufadhili budget wakati DP World IPO?

Hadi sasa, hatujapata majibu, media zimechukuliwa na upepo wa uteuzi na maigizo ya kijana wa chama Fulani.

Tunataka kujua yafuatayo;

1. Je IGA ilifutwa au Bado IPO?

2. HGA zilipelekwa bungeni Ili kuangaliwa UPYA ikiwa zimekidhi SHERIA zetu kama nchi juu ya ulinzi wa Raslimali zetu?

3. Kwanini mgao wa umeme unaendelea ilhali mvua zimenyesha kubwa Nchi nzima?

4. Kwanini Mawaziri walioguswa na tuhuma mbalimbali mf Nishati, ujenzi, Fedha nknk hawajaondoshwa Hadi sasa?

5. Pesa zilozoibwa sawasawa na Ripoti ya CAG katika Halmashauri mbalimbali, zimesharudishwa kiasi Gani Hadi sasa?

6. Je ni sawa Rais kuendelea kuteua wahusika wa Tume ya Uchaguzi, I wapi Tume huru ya Uchaguzi?

7. Kwanini uchaguzi wa MITAA 2024 usisogezwe mbele 2025 Ili isimamiwe na Tume huru ya Uchaguzi na kupunguza gharama ya mara mbili?

8.Ikiwa DP World Wana manufaa katika Nchi yetu, kwanini Serikali ikope Trilion SITA kufadhili budget ijayo wakati DP world wapo? HOJA hii no. 8,imetolewa na Nyumisi memba wa JF.

Ndugu watanzani, tusikubali kuhamishwa kujadili issues muhimu , kamwe tusikubali kutekwa na maigizo ya chama chakavu kinachowaza uchaguzi bila kusema kimewatumikia wananchi Kwa kiwango Gani!!

Ni hayo Kwa sasa.

Karibuni.
 
Huyo aliyeteuliwa kama kweli hawezi kumsaliti Magufuli aanze kutuambia ukweli juu ya mambo haya
Kwanini hatwambii kwanini mkataba Ule fake ulilazimishwa namna Ile?

Nini Kiko nyuma ya mkataba huo BATILI, uliokataliwa na wananchi?

Elli
 
Salaam, Shalom!!

Kuna uteuzi ulifanyika siku ya kusaini mkataba BATILI wa kukodisha URITHI wetu, Bandari Kwa wageni.

Uteuzi huo umekuja na wimbi la Matukio ya kutengeneza wenye Nia ya kutusahaulisha wanaukoo juu ya kilichofanyika...
Duh aise hii nchi inapoeleke
 
Kwanini hatwambii kwanini mkataba Ule fake ulilazimishwa namna Ile?

Nini Kiko nyuma ya mkataba huo BATILI, uliokataliwa na wananchi?
Hii nchi inachezewa na familia zisizozidi 10 na mwasisi wa uchafu huu ni yule mzee mfitinishaji wa pale njiapanda, huyo ndiye kawafundisha viongozi wengine kuanza kuiuza nchi kidogokidogo
 
Hii nchi inachezewa na familia zisizozidi 10 na mwasisi wa uchafu huu ni yule mzee mfitinishaji wa pale njiapanda, huyo ndiye kawafundisha viongozi wengine kuanza kuiuza nchi kidogokidogo
Tusikubali kuhamishwa kujadili issue ya msingi.

Je IGA ilifutwa?

Professor shivji na manguli wengi wa SHERIA walisema haifai hata kidogo,
 
Huyo aliyeteuliwa kama kweli hawezi kumsaliti Magufuli aanze kutuambia ukweli juu ya mambo haya
Kijana Si mzalendo hata kidogo,

Hatujasahau, Mzigo wake ulikamatwa bandarini bila kulipa Kodi.

Mpango akiwa waziri wa Fedha, alizuia Mzigo wa kijana uliotaka kuingia pasi Kodi.

HATUDANGANYIKI.
 
Salaam, Shalom!!

Kuna uteuzi ulifanyika siku ya kusaini mkataba BATILI wa kukodisha URITHI wetu, Bandari Kwa wageni.

Uteuzi huo umekuja na wimbi la Matukio ya kutengeneza wenye Nia ya kutusahaulisha wanaukoo juu ya kilichofanyika...
Chama chakavu cha Matukio,mara kupanda farasi,mara ngamia,mara punda mwisho mwenezi wao atapanda juu ya mbuzi.
 
Salaam, Shalom!!

Kuna uteuzi ulifanyika siku ya kusaini mkataba BATILI wa kukodisha URITHI wetu, Bandari Kwa wageni.

Uteuzi huo umekuja na wimbi la Matukio ya kutengeneza wenye Nia ya kutusahaulisha wanaukoo juu ya kilichofanyika...
Mkuu

Mimi siwalaumu wananchi tena,Wala CCM Tena Wala Rais Tena !

Mimi nailaumu taaisisi za siri zinazoamua kesho ya taifa hili!!

Taasisi inayoamua kesho yetu ndio ya kulaumiwa!huwezi jiita DS halafu unaleta mtu anaiba rasilimali kama hivyo halafu ukamuacha akaendelea kupumua kama Leo tuonavyo!!

Mimi naandika na Chelsea kusema DS ya Tanzania ni taasisi Batili kwa haya yanayoendelea kama ni ya kweli!!!

Haiwezekani kuwaachia wafanye wanavyotaka!!

Mungu ibariki Tanzania yetu tuipendayo sana!
 
Mkuu

Mimi siwalaumu wananchi tena, Wala CCM Tena Wala Rais Tena !

Mimi nailaumu taaisisi za siri zinazoamua kesho ya taifa hili!...
Chief Mangungo na wenzie waliuza nchi na watu wake,

Wajukuu kina Nyerere, waliibuka na kudai uhuru na Nchi yetu na ilirudi.

Mali ya ukoo Huwa haiuzwi.

Kuhusu DS, usijali, wazalendo wa Kweli wanarudi Kwa Kasi, ingawa kijana Si mmoja wao,

Alitaka kumzunguka Magu Kwa kuingiza makontena bila kulipia, Mpango akamshika shati.

Tusubiri.
 
Vile vijana mnachakata kwenye kibod kama mna hasira kweli vileeee tiraaaliraaa nyingi kupongezana kwingii pointi nyiiiingi.

Wanaharakati uchwara wakiwa kwenye kibod hamasa za maandamano nyiiiingi wameshindwa hata na madereza hiace na bajaji.

Acheni kujazana upepo uchwaraa kelele nyiingii mkipewa muongoze hata Chama holaaa.

Leo eti bandari, ardhi, misitu blablaaaaa.
 
Miaka yoooote uchaguzi haupo huruuu na mnapiga kura bado.

Miaka yotee mnaibiwa kura.

Maandamano yakianzishwa hata na yule MWAMBA WA KASKAZINI na akiswekwa ndani wote mikia katikati ya miguu mnabaki maandamano ya kwenye keybod ndio mabingwa hayo hata CHUKUA CHAKO MAPEMA mmewashinda na ndio mnayaweza na somo la matusi mmefuzu.
 
Back
Top Bottom