Neema ya BWANA
Member
- Jun 25, 2023
- 45
- 32
NENO LA MUNGU LINASEMA: "Kila mtu na aitii MAMLAKA iliyo KUU; kwa maana HAKUNA MAMLAKA ISIYOTOKA KWA MUNGU; na ile iliyopo umeamriwa na MUNGU. Hivyo amwasiye mwenye MAMLAKA hushindana na AGIZO LA MUNGU; nao washindanao watajipatia hukumu. Kwa maana watawalao hawatishi watu kwa sababu ya matendo mema, bali kwa sababu ya matendo mabaya. Basi, wataka usimwogope mwenye MAMLAKA? Fanya mema, nawe utapata sifa kwake; kwa kuwa yeye ni MTUMISHI WA MUNGU kwako kwa ajili ya MEMA. Lakini ufanyapo mabaya, ogopa; kwa maana hauchukui upanga bure; kwa kuwa ni MTUMISHI WA MUNGU, amlipizaye kisasi mtenda mabaya kwa ajili ya ghadhabu." (Warumi 13:1-4)
Tafsiri yake ni kuwa, MAMLAKA ZOTE ZINATOKA KWA MUNGU.
SERIKALI ZA JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA kuanzia awamu ya kwanza (1) mpaka awamu ya sita (6) zimetoka kwa MUNGU; hivyo amwasiye mwenye MAMLAKA anashindana na AGIZO LA MUNGU. Kumbe basi kwa NENO HILI hata suala la Bandari ya Dar es Salaam nchini Tanzania la kusaini mkataba na DP WORLD NI AGIZO KUTOKA KWA MUNGU ambalo limekuja kwa kusudi maalum; hivyo anayepingana na agizo hili hayupo upande wa MUNGU wala upande wa Watanzania bali yupo upande wa adui nyoka mwenye sumu ya hasira kali na Taifa la Tanzania anayetaka tufarakane, tuvutane hatimaye Taifa letu ligawanyike vipande vipande; ili BARAKA Alizotuandalia MUNGU kama Taifa zigeuke kuwa laana na tuzikose. (Washindwe na walegee kwa JINA LA YESU)
NENO LA MUNGU LINASEMA; "Je! Wewe hukujua? Hukusikia? YEYE MUNGU wa milele, BWANA, Muumba miisho ya dunia, Hazimii, wala Hachoki; AKILI ZAKE Hazichunguziki. Huwapa NGUVU wazimiao, Humwongezea NGUVU yeye asiyekuwa na uwezo." (Isaya 40:28-29)
Tukumbuke kuwa enzi za utumwa nchini Tanzania na Afrika miaka ya 1990 mpaka miaka ya 1960 na nyuma zaidi ya miaka ya 1960, mataifa mbalimbali ambayo kwa sasa ni mataifa yaliyoendelea yalifanya biashara ya utumwa Barani Afrika. Waafrika walikuwa wakinunuliwa na Mataifa ya Uarabuni na watu mbalimbali kutoka Magharibi waliofanya biashara ya utumwa kisha Waafrika kwenda kuuzwa ili wakatumike kwenye shughuli za kuongeza nguvu na kujenga uchumi wa mataifa hayo na lengo lilitimia kwa 100%.
Swali ni je? Mnashangaa nini leo hii Taifa la Tanzania tukimpa Mwarabu huyu huyu nafasi ya kuja kufanya kazi Tanzania ili Kujenga uchumi wa Taifa letu na Afrika kwa ujumla na sisi tufanikiwe kama wao walivyofanikiwa na zaidi?
MUNGU Ameona udhaifu wa Watanzania, Tanzania na Bandari ya Tanzania ulipo, hivyo huenda kwa njia hii ya Tanzania na DP World; MUNGU Ameamua Kutuongezea NGUVU (Isaya 40:28-29) kutoka kwa walewale waliotumia nguvu za mababu zetu kipindi cha nyuma ili tufikie Maendeleo Makubwa ambayo tuliishia kuyaona kwenye mataifa mengine, tofauti ni kuwa; Tanzania KWA NEEMA YA MUNGU ni Taifa la Amani hivyo hatulipi WEMA KWA UBAYA ndiyo maana hatuwezi kumchukua Mwarabu kwa njia ya Ukoloni na Utumwa aje kutusaidia Kujenga Taifa letu bali kwa HEKIMA YA MUNGU, Serikali imeamua kumchukua Mwarabu kwa njia ya AMANI NA MARIDHIANO; kwa sababu AMANI NA MARIDHIANO ndiyo TABIA YA MUNGU Aliyetuumba.
Kosa la Serikali liko wapi? Kosa la Rais wetu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ni nini?
Tuiache HEKIMA YA MUNGU Iamue kupitia Serikali Yetu Pendwa ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania; Akisema Mwarabu sawa, Akisema Mjapan sawa, Akisema Mchina sawa, Akisema Mkorea sawa, Akisema Mmarekani sawa kikubwa tuiachie Serikali; kwa HEKIMA YA MUNGU ifanye kile inachoona ni sahihi, kwani kile ambacho NI SAHIHI MBELE ZA MUNGU Lazima kipite na kiwe haijalishi wanadamu wameongea, wamepiga kelele, wamepiga vuvuzela, wamepiga ukunga au wamenyamaza kimya na wametulia; vivyo hivyo kile ambacho SI SAHIHI MBELE ZA MUNGU hakiwezi kuwa haijalishi wananchi wamenyamaza kimya, wametulia, wamepoa, wamefunga midomo au wameamua kuongea na kupiga kelele.
Tatizo la baadhi ya wanadamu ambao pia ni baadhi ya wananchi wa Taifa la Tanzania tunajisahau kufanya yanayotuhusu kama watoto wa familia ya Tanzania tunaanza kuingilia mpaka mambo ya chumbani ya baba na mama (wazazi) bila kujua kuwa baba na mama Huongozwa na MUNGU kutulea sisi ipasavyo na sisi kama watoto wa familia ya Tanzania inatupasa kutimiza majukumu yetu kwa nafasi yetu kama watoto wa Familia na Taifa la Tanzania ili kwa nafasi yetu na sisi watoto tuongozwe na HEKIMA YA MUNGU kuleta Maendeleo nyumbani; kwani njia wanazotumia wazazi (Serikali) kuleta Maendeleo ya Taifa hayatuhusu kikubwa tunajua kuwa ni HEKIMA YA MUNGU ndiyo inayowaongoza. (Warumi 13:1-4)
Kupitia andiko langu nililotangulia kuliandika hapa JAMII FORUMS kipengele cha STORIES OF CHANGE liitwalo ASANTE MAGHARIBI, KARIBU MASHARIKI nimeelezea namna Mataifa ya Magharibi kwa kipindi kirefu yamekuwa wazazi kwa Bara la Afrika, hivyo sasa kama watoto tujiongeze tufanye kazi na Mataifa ya Mashariki tukatafute na kurudisha nyumbani. Andiko hili halimaanishi lazima tuhame na Serikali zetu ambazo pia ni wazazi kwetu; kwani huenda wazazi (Serikali Zetu) wanafurahi zaidi kuendelea kufanya kazi na wazazi wenzao (Mataifa ya Magharibi) kuliko mahali ambapo watoto tunatakiwa tufanye kazi na Marafiki zetu; yaani Mashariki (Mataifa ya Mashariki); kikubwa Wazazi (Serikali) na Watoto (Wananchi) wote tunajenga Familia Moja na Taifa Moja la Tanzania na Bara moja la Afrika.
Kiunganishi cha andiko hili ni;
www.jamiiforums.com
Ili Taifa la Tanzania na Bara la Afrika kwa ujumla tuweze kupata MAENDELEO MAKUBWA na kwa WAKATI SAHIHI; tunatakiwa mambo ya MUNGU Tumwachie MUNGU, Mambo ya Serikali tuiachie Serikali.
Tafsiri yake ni kuwa; ili Taifa la Tanzania na Bara la Afrika liweze kuwa na UTAWALA BORA NA UWAJIBIKAJI SAHIHI KATI YA SERIKALI NA WANANCHI KILA MMOJA KWA NAFASI YAKE, ni lazima Watanzania na Waafrika tujifunze kumpa Kaisari yaliyo ya Kaisari na KUMPA MUNGU YALIYO YA MUNGU. (Mathayo Mtakatifu 22:21) (Marko Mtakatifu 12:17); kwani Mwananchi ambaye ni mtoto kwa Taifa la Tanzania kuingilia masuala ya Bandari ambalo ni JUKUMU la Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ambaye ndiye mzazi wa Watanzania ni sawa na kuchukua ya Kaisari kumpa Mtume Paulo lazima UTAWALA BORA NA UWAJIBIKAJI WA SERIKALI KWA NAFASI YAKE NA WANANCHI KWA NAFASI YAO uyumbe hivyo kupelekea kuchelewesha MAENDELEO YA TAIFA LETU LA TANZANIA NA BARA LETU LA AFRIKA.
HITIMISHO
Swali ni je! Majukumu yetu watoto wa Taifa la Tanzania (Afrika) ni yapi?
Jibu ni; Majukumu yetu watoto wa Taifa la Tanzania ni kutoingilia masuala nyeti kama Bandari ambayo ni KAZI YA SERIKALI bali ni kujihusisha na majukumu yetu ambayo ni KAZI YA MUNGU; nayo ni JAMII, ELIMU, UBUNIFU, SANAA NA TEKNOLOJIA. (Mwanzo 1 na Mwanzo 2) (Mithali 4:13) (Kutoka 31:1-6) (Kutoka 35:30-35)
Kwa mfano katika wakati huu; 'TREND' yaani HABARI KUBWA Nchini Tanzania kwenye Mitandao, Vyombo vya Habari na midomo ya Wananchi; Watoto wa Tanzania, badala ya kuwa BANDARI ambayo haituhusu ni JUKUMU LA SERIKALI; ilipaswa kuwa JAPAN NA SIKU YA KISWAHILI DUNIANI; NI NJIA GANI ITUMIKE KUKIRASIMISHA KISWAHILI NCHINI JAPAN? Hii ni baada ya Ubalozi wa Tanzania nchini Japan Kuripoti kuhusu Maadhimisho ya Lugha ya KISWAHILI duniani kule nchini Japan jana tarehe 7 Julai 2023 yaliyoongozwa na BALOZI WA JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA NCHINI JAPAN MHESHIMIWA BALOZI BARAKA H. LUVANDA; kwani hili na mambo yanayofanana na hili ndiyo MAJUKUMU YETU YANAYOTUHUSU wananchi; watoto wa Tanzania.
Wajapan wako 'busy' kuitangaza TANZANIA, LUGHA YETU ADHIMU YA KISWAHILI, UTAMADUNI WETU NA KUHUSU MAENDELEO YA AFRIKA; cha ajabu baadhi ya watanzania tuko 'busy' na mambo yasiyotuhusu hata kupelekea wengine kutofahamu kama jana tarehe 7/7 ilikuwa ni siku ya maadhimisho ya LUGHA YA KISWAHILI duniani.
Picha kutoka kwenye Tovuti ya Ubalozi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Nchini Japan.
TUWE WAUNGWANA WAPENDWA WANGU, NDUGU ZANGU WATANZANIA NA MUNGU KWA NEEMA YAKE ATUSAIDIE KATIKA HILI; TAIFA LETU NI MOJA, MUNGU WETU NI MMOJA, RAIS WETU NI MMOJA; SISI SOTE NI NDUGU, TUPENDANE NA TUIPENDE SERIKALI YETU, VIONGOZI WETU, TAIFA LETU LA TANZANIA, BARA LETU LA AFRIKA NA MATAIFA YOTE DUNIANI KWANI UPENDO KWANZA. (Yohana Mtakatifu 13:34) (Wagalatia 5:13-14) (Mathayo 22:37-40) (Marko 12:30-33)

SoC03 - Asante Magharibi, karibu Mashariki
Kwa takriban karne 21 sasa Bara la Afrika limekuwa likitegemea Teknolojia kutoka Nchi za Magharibi ikiwemo Marekani, Ujerumani, Uingereza na baadhi ya Mataifa ya Asia Magharibi. Kwa hili naomba niseme asante sana kwa Mataifa ya Magharibi kwani mmeweza kulisaidia Bara la Afrika katika nyanja...
www.jamiiforums.com
Ili Taifa la Tanzania na Bara la Afrika kwa ujumla tuweze kupata MAENDELEO MAKUBWA na kwa WAKATI SAHIHI; tunatakiwa mambo ya MUNGU Tumwachie MUNGU, Mambo ya Serikali tuiachie Serikali.
Tafsiri yake ni kuwa; ili Taifa la Tanzania na Bara la Afrika liweze kuwa na UTAWALA BORA NA UWAJIBIKAJI SAHIHI KATI YA SERIKALI NA WANANCHI KILA MMOJA KWA NAFASI YAKE, ni lazima Watanzania na Waafrika tujifunze kumpa Kaisari yaliyo ya Kaisari na KUMPA MUNGU YALIYO YA MUNGU. (Mathayo Mtakatifu 22:21) (Marko Mtakatifu 12:17); kwani Mwananchi ambaye ni mtoto kwa Taifa la Tanzania kuingilia masuala ya Bandari ambalo ni JUKUMU la Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ambaye ndiye mzazi wa Watanzania ni sawa na kuchukua ya Kaisari kumpa Mtume Paulo lazima UTAWALA BORA NA UWAJIBIKAJI WA SERIKALI KWA NAFASI YAKE NA WANANCHI KWA NAFASI YAO uyumbe hivyo kupelekea kuchelewesha MAENDELEO YA TAIFA LETU LA TANZANIA NA BARA LETU LA AFRIKA.
HITIMISHO
Swali ni je! Majukumu yetu watoto wa Taifa la Tanzania (Afrika) ni yapi?
Jibu ni; Majukumu yetu watoto wa Taifa la Tanzania ni kutoingilia masuala nyeti kama Bandari ambayo ni KAZI YA SERIKALI bali ni kujihusisha na majukumu yetu ambayo ni KAZI YA MUNGU; nayo ni JAMII, ELIMU, UBUNIFU, SANAA NA TEKNOLOJIA. (Mwanzo 1 na Mwanzo 2) (Mithali 4:13) (Kutoka 31:1-6) (Kutoka 35:30-35)
Kwa mfano katika wakati huu; 'TREND' yaani HABARI KUBWA Nchini Tanzania kwenye Mitandao, Vyombo vya Habari na midomo ya Wananchi; Watoto wa Tanzania, badala ya kuwa BANDARI ambayo haituhusu ni JUKUMU LA SERIKALI; ilipaswa kuwa JAPAN NA SIKU YA KISWAHILI DUNIANI; NI NJIA GANI ITUMIKE KUKIRASIMISHA KISWAHILI NCHINI JAPAN? Hii ni baada ya Ubalozi wa Tanzania nchini Japan Kuripoti kuhusu Maadhimisho ya Lugha ya KISWAHILI duniani kule nchini Japan jana tarehe 7 Julai 2023 yaliyoongozwa na BALOZI WA JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA NCHINI JAPAN MHESHIMIWA BALOZI BARAKA H. LUVANDA; kwani hili na mambo yanayofanana na hili ndiyo MAJUKUMU YETU YANAYOTUHUSU wananchi; watoto wa Tanzania.
Wajapan wako 'busy' kuitangaza TANZANIA, LUGHA YETU ADHIMU YA KISWAHILI, UTAMADUNI WETU NA KUHUSU MAENDELEO YA AFRIKA; cha ajabu baadhi ya watanzania tuko 'busy' na mambo yasiyotuhusu hata kupelekea wengine kutofahamu kama jana tarehe 7/7 ilikuwa ni siku ya maadhimisho ya LUGHA YA KISWAHILI duniani.
Picha kutoka kwenye Tovuti ya Ubalozi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Nchini Japan.
TUWE WAUNGWANA WAPENDWA WANGU, NDUGU ZANGU WATANZANIA NA MUNGU KWA NEEMA YAKE ATUSAIDIE KATIKA HILI; TAIFA LETU NI MOJA, MUNGU WETU NI MMOJA, RAIS WETU NI MMOJA; SISI SOTE NI NDUGU, TUPENDANE NA TUIPENDE SERIKALI YETU, VIONGOZI WETU, TAIFA LETU LA TANZANIA, BARA LETU LA AFRIKA NA MATAIFA YOTE DUNIANI KWANI UPENDO KWANZA. (Yohana Mtakatifu 13:34) (Wagalatia 5:13-14) (Mathayo 22:37-40) (Marko 12:30-33)
Attachments
Upvote
1