elivina shambuni
JF-Expert Member
- May 31, 2018
- 461
- 295
kupokea na kufungua gati namba tatu baada ya siku 10 kuanzia sasa. Gati hilo ni sehemu ya magati saba yanayojengwa katika bandari hiyo na yanayotarajiwa kufunguliwa na mamlaka hiyo na hivyo kuwezesha kuhudumia tani za mizigo milioni 25 kutoka milioni 16.2 inayohudumia sasa kwa mwaka.
Gati hizo zitakuwa na uwezo wa kupokea meli kubwa na kushusha mizigo mikubwa ikiwamo makontena na magari. Aidha, baada ya ukarabati wa bandari mbalimbali nchini kuanza kukamilika, serikali imeanza kujiandaa kwa ajili ya kupokea mizigo inayokwenda nchi za Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC).
Hayo yalisemwa na Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Isack Kamwelwe, wakati akizungumza na waandishi wa habari Dar es Salaam jana, baada ya Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Bajeti kutembelea baadhi ya maeneo bandarini hapo.
Alisema kwa sasa gati namba sifuri au maarufu Roro, gati namba moja na namba mbili pia zimekamilika na kuanza kutumika, huku TPA baada ya siku 10 ikisubiri kukabidhiwa gati namba tatu. Alisema baada ya Bandari ya Dar es Salaam kufanyiwa ukarabati gati namba sifuri yenye uwezo wa kushusha na kuhifadhi hadi magari 600,000 kwa mwaka, tayari limeanza kushusha magari huku magati mengine namba moja na namba mbili yakipokea meli zinazoshusha mizigo ya kichele.
“Conveyor belt ni mtambo mzuri ambao tukiupata meli zinazotumia siku 12 kushusha mizigo hii ya kichele sasa zitatumia siku nne. Tayari tumeshapitishiwa fedha kwa ajili ya kununua mashine hizi na tunachosubiri ni kutangaza zabuni,” alisema Kamwelwe.