Bams
JF-Expert Member
- Oct 19, 2010
- 19,362
- 48,879
Bandari haijakodishwa , bali imeporwa.
Kama ingekuwa imekodishwa tungeambiwa inakodishwa kuanzia lini mpaka lini, na malipo ya mwenye mali yatakuwa kiasi gani, na aliyekodi atabakia na nini wakati ikiwa imekodishwa.
Kuna yeyote ameona kwenye mkataba tumekodisha kwa kiasi gani? Hata kama una lorry lako, umeshindwa kununulia matairi, unamkodishia mtu afanyie biashara, na gharama zote za matengenezo ziwe kwa aliyekodi kipindi chote akiwa amekodi, ndiyo iwe mwenye lorry asiwe na sehemu yoyote kwenye mapato atakayopata aliyekodi?
Kwenye madini ambako hatujaweka hata shilingi, lakini kwa kuwa madini yapo katika nchi yetu, nchi inamiliki 16% kwenye kila mradi wa uchimbaji madini. Hapo zamani, hata tuliposema tunapunjwa, angalao tulikuwa tunamiliki 10% kwenye kila mgodi wa madini. Na hiyo haiondoi haki ya Serikali kukusanya kodi zote kwa mchimbaji ikiwa ni pamoja na corporate tax 30%, mrabaha 6%, inspection fee 1%, local levy 0.3%.
Huku kwenye bandari ambako bahari nibyetu na tumwekeza matrilioni ya pesa, haki ya umiliki 0%, kodi nyingine, eti DP wapewe punguzo maalum! Halafu amiliki kwa 100% kwa kipindi kisichojulikana!! Kuna mwenye akili timamu anaweza kuukubali uwendawazimu wa namna hii?
Aliyelikubali hili, natamka kwa dhamira njema kabisa, huyo ni hayawani mkubwa, ni mjinga wa kupindukia ambaye anazidiwa akili hata na mtu ambaye hajawahi kuona hata mlango wa darasa.
Wapo wanavijiji huko vijijini, wana ardhi kubwa, hawana uwezo wa kuitumia yote, huwa wanakodisha washamba yao, hawakupi bure, lazima utalipa. Sisi, bandari ambayo mara ya mwisho tumefanya uwekezaji wa zaidi ya trillion 1, eti tunampa mwarabu bure, halafu tunadanganywa kuwa tutanufaika kupitia kodi, ajira na huduma zilizoboreshwa, lakini hakuna chochote tunachogusa kwenye yale mapato ya mwekezaji. Kwani huko kwenye madini ambako hatujaweka pesa yetu, huwa hawalipi kodi, hawatoi ajira? Mbona tuna umiliki wa bure wa 16%.
Kwenye bandari kwa sababu zaidi ya kuwa bahari ni yetu, pia tumewekeza pesa nyingi, mkataba licha ya kulazimika kuwa na muda, tunastahili kumiliki zaidi ya 16% kwa kuangalia yeye mwekezaji anawekeza kiasi gani. Kama anawekeza trillion 10, sisi tumewekeza trillion 5, ina maana sisi tunatakiwa kumiliki 25% kutokana na uwekezaji wetu, plus 16% free carried ownership kwa sababu rasilimali ni yetu. Hivyo sisi tutastahili kuwa 41%, mwendeshaji 59%.
DP hawa hawa, bandari mojawapo wanayoiendesha kule UK hawana umiliki wa 100% kwa sababu tayari Serikali ilikwishafanya uwekezaji kabla ya wao kuanza kutoa huduma. Kwa hiyo kule kwenye bandari ya Uingereza ni partnership ila huku wanataka umiliki wa 100% kama vile hakuna chochote tulichowekeza, hivi hawa waarabu mbonu wanatufanya sisi watanzania wote hamnazo?
Sisi lazima tuwadhihirishie kuwa kama kuna watu hamnazo basi ni hao waliosaini nao mkataba, na makuwadi wao waliopo bungeni, lakini huku nje kwa Watanzania, kuna watu wenye akili timamu ambao hawawezi kuukubali uhayawani wa namna hiyo.
Mkataba huu kama ni mzuri sana, tunaomba uanze na bandari ya Zanzibar na Pemba, maana wenzetu wameuona ni mzuri sana. Kilicho chema sana, ni busara kukipeleka kwanza nyumbani kwako kabla hujapeleka ugenini. Mbalawa, tunamwomba azungumze na Serikali ya nyumbani kwake kule Zanzibar, ili watanganyika tujifunze kutoka kwao, maana wamekwishakataa kuwa suala la bandari siyo la mwungano.