Bandari haijakodishwa bali imeporwa

Bandari haijakodishwa bali imeporwa

Bandari haijakodishwa , bali imeporwa.

Kama ingekuwa imekodishwa tungeambiwa inakodishwa kuanzia lini mpaka lini, na malipo ya mwenye mali yatakuwa kiasi gani, na aliyekodi atabakia na nini wakati ikiwa imekodishwa.

Kuna yeyote ameona kwenye mkataba tumekodisha kwa kiasi gani? Hata kama una lorry lako, umeshindwa kununulia matairi, unamkodishia mtu afanyie biashara, na gharama zote za matengenezo ziwe kwa aliyekodi kipindi chote akiwa amekodi, ndiyo iwe mwenye lorry asiwe na sehemu yoyote kwenye mapato atakayopata aliyekodi?

Kwenye madini ambako hatujaweka hata shilingi, lakini kwa kuwa madini yapo katika nchi yetu, nchi inamiliki 16% kwenye kila mradi wa uchimbaji madini. Hapo zamani, hata tuliposema tunapunjwa, angalao tulikuwa tunamiliki 10% kwenye kila mgodi wa madini. Na hiyo haiondoi haki ya Serikali kukusanya kodi zote kwa mchimbaji ikiwa ni pamoja na corporate tax 30%, mrabaha 6%, inspection fee 1%, local levy 0.3%.

Huku kwenye bandari ambako bahari nibyetu na tumwekeza matrilioni ya pesa, haki ya umiliki 0%, kodi nyingine, eti DP wapewe punguzo maalum! Halafu amiliki kwa 100% kwa kipindi kisichojulikana!! Kuna mwenye akili timamu anaweza kuukubali uwendawazimu wa namna hii?

Aliyelikubali hili, natamka kwa dhamira njema kabisa, huyo ni hayawani mkubwa, ni mjinga wa kupindukia ambaye anazidiwa akili hata na mtu ambaye hajawahi kuona hata mlango wa darasa.

Wapo wanavijiji huko vijijini, wana ardhi kubwa, hawana uwezo wa kuitumia yote, huwa wanakodisha washamba yao, hawakupi bure, lazima utalipa. Sisi, bandari ambayo mara ya mwisho tumefanya uwekezaji wa zaidi ya trillion 1, eti tunampa mwarabu bure, halafu tunadanganywa kuwa tutanufaika kupitia kodi, ajira na huduma zilizoboreshwa, lakini hakuna chochote tunachogusa kwenye yale mapato ya mwekezaji. Kwani huko kwenye madini ambako hatujaweka pesa yetu, huwa hawalipi kodi, hawatoi ajira? Mbona tuna umiliki wa bure wa 16%.

Kwenye bandari kwa sababu zaidi ya kuwa bahari ni yetu, pia tumewekeza pesa nyingi, mkataba licha ya kulazimika kuwa na muda, tunastahili kumiliki zaidi ya 16% kwa kuangalia yeye mwekezaji anawekeza kiasi gani. Kama anawekeza trillion 10, sisi tumewekeza trillion 5, ina maana sisi tunatakiwa kumiliki 25% kutokana na uwekezaji wetu, plus 16% free carried ownership kwa sababu rasilimali ni yetu. Hivyo sisi tutastahili kuwa 41%, mwendeshaji 59%.

DP hawa hawa, bandari mojawapo wanayoiendesha kule UK hawana umiliki wa 100% kwa sababu tayari Serikali ilikwishafanya uwekezaji kabla ya wao kuanza kutoa huduma. Kwa hiyo kule kwenye bandari ya Uingereza ni partnership ila huku wanataka umiliki wa 100% kama vile hakuna chochote tulichowekeza, hivi hawa waarabu mbonu wanatufanya sisi watanzania wote hamnazo?

Sisi lazima tuwadhihirishie kuwa kama kuna watu hamnazo basi ni hao waliosaini nao mkataba, na makuwadi wao waliopo bungeni, lakini huku nje kwa Watanzania, kuna watu wenye akili timamu ambao hawawezi kuukubali uhayawani wa namna hiyo.

Mkataba huu kama ni mzuri sana, tunaomba uanze na bandari ya Zanzibar na Pemba, maana wenzetu wameuona ni mzuri sana. Kilicho chema sana, ni busara kukipeleka kwanza nyumbani kwako kabla hujapeleka ugenini. Mbalawa, tunamwomba azungumze na Serikali ya nyumbani kwake kule Zanzibar, ili watanganyika tujifunze kutoka kwao, maana wamekwishakataa kuwa suala la bandari siyo la mwungano.
Ndivyo ulivyoelewa?
 
Wanaposema wanalinda mipaka ya nchi, ni mipaka ipi wanamaanisha, mbona huu mpaka kupitia bahari unaibwa?

Mipaka ya nchi iliyowekwa kisheria, kulinda haimaanish kila maamuzi ya serikali waingilie no, hilo ni jukumu la wananchi , wananchi wakiamua probably wata support until then
 
Unajua wizi na ubadhirifu uliopo pale bandarin kwa Sasa?mijitu inatunisha matumbo kwa wizi! Miaka ya 90,wakati tunabinafsisha TBL na TCC,watu walipiga kelele sana,kulikuwa na meneja Mmoja Mmoja pale TBL,yeye alikuwa anaweka ndugu zake TU,hata kama ni vilaza,kampuni ilikuwa haiingizi pesa serikalini,hata mishahara lazima itoke hazina,baada ya kubinafsishwa,TBL imekuwa kama TRA,mishahara ni minono,
Hao DP waje,wataongeza ajira,serikali itapata Kodi kupitia PAYE!!
Hizi kelele nyingi zingine zinaletwa na majizi ya huko bandarin,yanahofia michongo Yao Haram inaenda kulisha.
Hakuna anayekata ukodishwaji katika uendeshaji, lakini mkataba unatakiwa uwe wazi na wenye maslahi mapana.

Tunataka muda wa mkataba.
Tunataka tujue DP atawekeza kiasi gani?
Sisi mpaka sasa tumewekeza kiasi gani?
DP kutokana na kiwango cha uwekezaji wake vs uwekezaji wetu plus ni rasilimali yetu, yeye atakuwa anamiliki kiasi gani na sisi tutamiliki kiasi gani?
Yeye atapata asilimia ngapi ya faida, na sisi tutapata asilimia ngapi?

Tunataka tujue ni mambo gani DP akiyafanya au asipoyafanya itamaanisha amekiuka mkataba, na hivyo sisi kumfurusha bila ya kumlipa fidia yoyote?

Halikadhalika kwa upande wetu, ni mambo gani tukiyafanya au tusipoyafanya, itamaanisha tumekiuka mkataba, na hivyo mkataba kukoma, na sisi kulazimika kumlipa fidia?

Hatutaki tubadilishe aina ya wezi, yaani tutoke kwenye kuibiwa na waswahili wenzetu, tuanze kuibiwa na mwarabu. Tunataka kusiwepo na wizi.
 
Bandari haijakodishwa , bali imeporwa.

Kama ingekuwa imekodishwa tungeambiwa inakodishwa kuanzia lini mpaka lini, na malipo ya mwenye mali yatakuwa kiasi gani, na aliyekodi atabakia na nini wakati ikiwa imekodishwa.

Kuna yeyote ameona kwenye mkataba tumekodisha kwa kiasi gani? Hata kama una lorry lako, umeshindwa kununulia matairi, unamkodishia mtu afanyie biashara, na gharama zote za matengenezo ziwe kwa aliyekodi kipindi chote akiwa amekodi, ndiyo iwe mwenye lorry asiwe na sehemu yoyote kwenye mapato atakayopata aliyekodi?

Kwenye madini ambako hatujaweka hata shilingi, lakini kwa kuwa madini yapo katika nchi yetu, nchi inamiliki 16% kwenye kila mradi wa uchimbaji madini. Hapo zamani, hata tuliposema tunapunjwa, angalao tulikuwa tunamiliki 10% kwenye kila mgodi wa madini. Na hiyo haiondoi haki ya Serikali kukusanya kodi zote kwa mchimbaji ikiwa ni pamoja na corporate tax 30%, mrabaha 6%, inspection fee 1%, local levy 0.3%.

Huku kwenye bandari ambako bahari nibyetu na tumwekeza matrilioni ya pesa, haki ya umiliki 0%, kodi nyingine, eti DP wapewe punguzo maalum! Halafu amiliki kwa 100% kwa kipindi kisichojulikana!! Kuna mwenye akili timamu anaweza kuukubali uwendawazimu wa namna hii?

Aliyelikubali hili, natamka kwa dhamira njema kabisa, huyo ni hayawani mkubwa, ni mjinga wa kupindukia ambaye anazidiwa akili hata na mtu ambaye hajawahi kuona hata mlango wa darasa.

Wapo wanavijiji huko vijijini, wana ardhi kubwa, hawana uwezo wa kuitumia yote, huwa wanakodisha washamba yao, hawakupi bure, lazima utalipa. Sisi, bandari ambayo mara ya mwisho tumefanya uwekezaji wa zaidi ya trillion 1, eti tunampa mwarabu bure, halafu tunadanganywa kuwa tutanufaika kupitia kodi, ajira na huduma zilizoboreshwa, lakini hakuna chochote tunachogusa kwenye yale mapato ya mwekezaji. Kwani huko kwenye madini ambako hatujaweka pesa yetu, huwa hawalipi kodi, hawatoi ajira? Mbona tuna umiliki wa bure wa 16%.

Kwenye bandari kwa sababu zaidi ya kuwa bahari ni yetu, pia tumewekeza pesa nyingi, mkataba licha ya kulazimika kuwa na muda, tunastahili kumiliki zaidi ya 16% kwa kuangalia yeye mwekezaji anawekeza kiasi gani. Kama anawekeza trillion 10, sisi tumewekeza trillion 5, ina maana sisi tunatakiwa kumiliki 25% kutokana na uwekezaji wetu, plus 16% free carried ownership kwa sababu rasilimali ni yetu. Hivyo sisi tutastahili kuwa 41%, mwendeshaji 59%.

DP hawa hawa, bandari mojawapo wanayoiendesha kule UK hawana umiliki wa 100% kwa sababu tayari Serikali ilikwishafanya uwekezaji kabla ya wao kuanza kutoa huduma. Kwa hiyo kule kwenye bandari ya Uingereza ni partnership ila huku wanataka umiliki wa 100% kama vile hakuna chochote tulichowekeza, hivi hawa waarabu mbonu wanatufanya sisi watanzania wote hamnazo?

Sisi lazima tuwadhihirishie kuwa kama kuna watu hamnazo basi ni hao waliosaini nao mkataba, na makuwadi wao waliopo bungeni, lakini huku nje kwa Watanzania, kuna watu wenye akili timamu ambao hawawezi kuukubali uhayawani wa namna hiyo.

Mkataba huu kama ni mzuri sana, tunaomba uanze na bandari ya Zanzibar na Pemba, maana wenzetu wameuona ni mzuri sana. Kilicho chema sana, ni busara kukipeleka kwanza nyumbani kwako kabla hujapeleka ugenini. Mbalawa, tunamwomba azungumze na Serikali ya nyumbani kwake kule Zanzibar, ili watanganyika tujifunze kutoka kwao, maana wamekwishakataa kuwa suala la bandari siyo la mwungano.
Mnyonge mnyongeni haki yake tumpe JPM kwenye rasilimali alijitahidi sana kwenye madini aliongeza umiliki Wa govt kutoka %10 mpaka %16 na hapo hatujawekeza pesa zetu %100 uwekezaji Wa pesa ni wao but kwenye hili La bandari tayari govt imewekeza trillion of money anakuja mjinga mmoja anasema atamiliki yeye pekee kwa %100 na mashariti ya kijinga kibao!!JPM alikosea Ku deal na wapinzani wake tu ambacho pia sio kitu kidogo kushindwa Ku balance democrasia daah!!! Tunakwenda wapi jamani!!
 
Uzuri hili nalo litapita.
Kelele hz za bandari mwisho mwezi huu tu kuzisikia, ikifika July tutakuwa na habari zingine
Tayari tupo July, tunaelekea mwishoni, suala la uporwaji wa bandari bado tunalo. Na hatutakoma kulaani na kukemea mkataba ule wa kishenzi.
 
20141018_MAP004_0.jpg
 
Back
Top Bottom