Bandari ya Dar es Salaam na mpango wa eneo la Kurasini

Bandari ya Dar es Salaam na mpango wa eneo la Kurasini

KalamuTena

JF-Expert Member
Joined
Jul 7, 2018
Posts
13,187
Reaction score
17,167
Bagamoyo inafyreka tu, haitakuwa na simile na mtu!

Tuliwahi kusikia taarifa nyingi kuhusu mpango wa kuiboresha bandari ya Dar es Salaam ili iweze kutoa huduma nzuri kwa wateja wake, na kuvutia wateja wapya toka sehemu mbalimbali, hasa majirani zetu wasiokuwa na bandari, kama DRC, Zambia, Malawi, Uganda, n.k..

Bila shaka mipango ya kuikarabati na kuifanya iwe ya ufanisi zaidi inaendelea hata sasa chini ya ule mpango wa Benki ya Dunia kuiboresha bandari hii.

Jambo nisiloelewa vizuri ni hili: bandari kufanikiwa zaidi kwenye shughuli zake za kuingiza na kutoa mizigo, ni lazima iwe na eneo kubwa zaidi?

Ufanisi wake hauwezi kufana kwa kuhakikisha kwamba mizigo inayoingia haikai bandarini kwa kuimarisha njia za kuiingiza na kuiondoa mizigo hiyo haraka mara inapoingia bandarini?

Hayo ni maswali nitakayowaachia wataam katika eneo hili wayajibu.

Sehemu ya pili ya mada hii ni eneo la Kurasini.

Inakumbukwa eneo hilo liliwahi kupangwa kufanya kazi zilizoambatana na bandari ya Dar es Salaam. Watu waliokuwa wakiishi kwenye eneo lile walihamishwa ili kupisha shughuli za kuweka nadhani EPZ, na wachina walisemekana wangekuja kuwekeza, wakilenga biashara zao kuhudumia maeneo ya nchi jirani. Mpango huo hausikiki tena, kama ulivyo ule wa Bandari ya Mwambani, Tanga. Je, mpango huo nao ulimezwa na mipango ya Bandari ya Bagamoyo?

Bagamoyo - kwani ni lazima iwe Bandari, haliwezi likawa eneo la viwanda na shughuli zingine bila ya bandari? Hii itaifanya Bandari yetu ya Da es Salaam iepuke janga la kumezwa na Bagamoyo.

Bandari ya Mwambani - inaweza kuendelea kujengwa ili kuhudumia eneo lote la kaskazini mwa nchi yetu na nchi jirani bila ya kuathiri shughuli za Bandari ya Dar es Salaam.

Hii Bandari ya Bagamoyo inavyozungumziwa, ni wazi sasa kwamba sharti la kutoendeleza bandari zingine ni sharti zito zaidi na ni la lazima ili mradi huo wa Bandari uwepo.

Hili ni sharti la kipuuzi zaidi kuliko masharti mengine yote yaliyomo kwenye mradi huo.

Na kama ni maswala ya mameli makubwa makubwa tunayoyataka yaje hapa, Mwambani itakuwa ndiyo bandari inayoweza kuisimamisha Lamu isiende popote katika eneo hilo.

Kama huamini, tazama ramani ujionee mwenyewe.

Reli inayotoka Tanga kuelekea kaskazini na magharibi mwa nchi yetu na kuelekea nchi jirani haina ushindani wowote na Bandari ya Lamu wala Mombasa.

Bandari ya Lamu inajengwa taratibu, kwa nini na sisi tusianze juhudi hizo, kabla hata wawekezaji hawajaichangamkia?
 
Back
Top Bottom