Bandari ya Dar es Salaam yaboreshwa kwa Bilioni 24.08 kuongeza Ufanisi wa Mizigo

Bandari ya Dar es Salaam yaboreshwa kwa Bilioni 24.08 kuongeza Ufanisi wa Mizigo

Zack Abdul

JF-Expert Member
Joined
Mar 9, 2026
Posts
1,194
Reaction score
911
Serikali imeidhinisha Shilingi bilioni 24.08 kupitia mradi wa Dar es Salaam Maritime Gateway Project kwa mwaka wa fedha 2025/26 ili kuboresha miundombinu ya Port of Dar es Salaam na kuongeza ufanisi wa huduma za mizigo pamoja na usalama wa bandari.

Hadi Februari 2026, bilioni 11.31 zilikuwa zimetolewa na kuwezesha kukamilika kwa upembuzi yakinifu wa maboresho ya Gati Na. 8–11, maandalizi ya ujenzi wa Gati Na. 12–15, ujenzi wa matanki 15 ya mafuta yenye uwezo wa kuhifadhi mita za ujazo 378,000 ukiwa umefikia asilimia 42, pamoja na uboreshaji wa Gati la Malindi ambao umefikia asilimia 11 huku kazi za awali zikiendelea.
IMG-20260514-WA0047.jpg
 
Back
Top Bottom