Bandari ya Dar es Salaam

Bandari ya Dar es Salaam

gkileo

JF-Expert Member
Joined
Apr 16, 2010
Posts
1,096
Reaction score
487
Wadau Hongereni kwa majukum mbalimbali ya Ujenzi wa Taifa letu.
mimi ni mchuuzi wa spare za pikpiki kutoka China ,kwa hali ninayoona nina wasiwasi sana na biashara yangu kua itafikia mwisho muda sii mtefu. miezi miwili iliyopita niliingiza mzigo kutoka china , ambapo niliupata baada ya siku 22 baada ya meli kutia nanga. hivi ninavyoandika nina mzigo bandarini ambapo meli imefika mwanzoni mwa novemba, na sijajua mzigo nitaupata lini. Hali hii husababisha bidhaa kua ghali na sisi tunaoanza na wenye mitaji midogo kufilisika kwa kua tunakaa muda mrefu bila kazi tunaposubiria mizigo yetu bandarini. Ajabu kubwa kwa sasa baadhi ya wafanya biashara hasa mwanza huenda kununua spare za pikipiki kutoka uganda isiyo na bandari na kuweza kushindana na sie wenye Bandari!
Nilipofungua hii biashara nilivutiwa na bandari nikajua sio wateja kutoka tanzania tu bali watatoka uganda , burundi, Kongo , Zambia ,Malawi nk . Lakini ninaangalia sasa hata miundombinu inajengwa kutoka mombasa hadi kigali kuiwezesha Kenya kua mlango wa uchumi Afrika mashariki na kati .muda sii mrefu wageni watapungua sana hapa kwetu .
Juhudi za mh. Mwakiembe zinajulikana
lkn bado bandarini kuna shida ya mizigo kuchelewa. naomba tuchangie japo mawazo maana tunaelekea kubakia kama kisiwa licha ya majaaliwa makubwa tuliyojaaliwa.
(pamoja na maelezo yangu pia nimeona kwenye mtandao taarifa hii)
Ukosefu wa ufanisi katika bandari ya Dar es Salaam wagharimu mabilioni ya dola, Benki ya Dunia yasema - Sabahionline.com
 
Back
Top Bottom