Bandari ya Tanzania wanatoa siku 7 bure kwa mzigo wa ndani kukaa pale kisha siku zinazofata utalipia storage charges.
Sidhani kama bandari wanaweza wakachelewesha mzigo uliochini ili wapate pesa ya storage. Kama ni ofisa fulani alikwamisha ni vyema ukaweka wazi kwa kumuuliza Wakala wako wa Forodha (Clearing Agent) wapi walimkwamisha.
Unaweza kuta agent alichelewa kufata release order, kuingiza documents, kufatilia na kulipia huduma ya verification.
TPA kwenye mfumo wa kuondoa mizigo saizi wamekuja na mfumo ambao hautaji sana paper work Kwenye kuingiza au kutoa mzigo.