Bandari ya Mangapwani Zanzibar au Bagamoyo Bara? Ipi itaitoa nchi yetu kiuchumi?

Bandari ya Mangapwani Zanzibar au Bagamoyo Bara? Ipi itaitoa nchi yetu kiuchumi?

chiembe

JF-Expert Member
Joined
May 16, 2015
Posts
16,859
Reaction score
28,112
Nimemuona Rais Mwinyi akiwa Uchina akipigia debe, pamoja na mambo mengine, Bandari ya Mangapwani. Katika hotuba zake kadhaa, Rais Mwinyi ameonyesha nia ya dhati kuifanya bandari hiyo iwe kubwa kabisa Afrika Mashariki.

Upande wa pili, inaelezwa kwamba bandari ya Bagamoyo ikikamilika, itakuwa na uwezo wa kubeba kontena sawa na bandari zote kusini mwa jangwa la sahara. Inakadiriwa kuwa na uwezo wa kontena milioni ishirini.

Kama nchi, wapi panalipa? Bandari ya Bagamoyo inajiunga moja kwa moja na nchi kavu. Mangapwani? Itabidi uchukue kontena halafu ulibebe tena kulileta bara?

Wajuvi, mna maoni gani? Kqa nini tuliipiga vita bandari ya Bagamoyo enzi za jiwe, baadae tukamuona jiwe anajenga bandari ya nyamirembe huko chato, bandari ambayo sidhani ilishawahi kupokea hata meli moja, achilia mbali mtumbwi!
 
Ingewezekanaje Rais wa Zanzibar kupigia debe mambo ya Tanganyika? Kwani yeye hataki kura ya Wazanzibari?
 
Back
Top Bottom