Bandari zetu nazo ziwe chini ya Ofisi ya Rais kwa Usalama wa Taifa

Bado hawa washenzi watapata njia za kutuchezea tu mkuu. TISS wenyewe siku hizi ni njaa tupu! Hakuna uzalendo wala nini!
 

... acha nijaribu kuwa 'clear' zaidi, ... ni hivi: mimi napendekeza bandari ziwe monitored, remotely, by TISS operatives wakiwa ikulu ambapo wataona kila kitu na kusikia kila kitu na kusoma documents na takwimu zote kwa kutumia videos na data zitakazokuwa streamed kutoka maeneo/na ofisi zote nyeti ya bandari zetu kupitia mtandao wa computa zote nyeti za bandari ambazo zinaweza kabisa kuwa 'integrated'na zile za ikulu!
... YAANI NATAKA BANDARINI PAWE BIG BROTHER SHOW YA KIAINA, ... NA RAIS AWEZE KUFUATILIA KILA ANAPOKUWA NA UMUHIMU AU MUDA WA 'LEISURE' WA KUCHUNGULIA HUKO NA HATA KUMHOJI MHUSIKA WA KITENGO CHOCHOTE CHA BANDARI!
Just cheap technology and IT is required for this!
NB: RESIDENT TISS AGENTS GET EASILY COMPROMISED AND CORRUPTED AND CAN EVEN START TO SYMPATHIZE WITH THE CROOKS!
 
Hiyo sasa ni kitu haiwezekani labda nikufahamkshe tu, bandari kuna direct link na ikulu. Zile system zote za bandari zipo linked na ikulu yani Rais anaweza kuaccess kujua wiki hii tunaingiza meli ngapi bandarini na Zina mzigo gani au tunaondoa meli ngapi na ikitokea akiona meli imekaa muda huwa anaweza kumpigia simu DG kuuliza.

Sasa hivi kuna Intergrated Security System (ISS) ambayo inainchude cameras na fence za umeme na Mambo kibao ambayo yanakuwa recorded kwenye CCTV.

Nadhani haujui namna bandari ilivyo ni vema uulize tukuleweshe sisi ni wadau pale
 
Je hyo issue anayoizungumza waziri mkuu ya system kuwa down ni michezo ya watu kupiga au ebu fafanua kdogo mdau
 
Sasa hapo "mihemko" ni ipi, au ulikuwa na kisasi cha kulipiza ambacho ulikiweka moyoni kwa muda mrefu, na leo ukapata upenyo?
 
Nadhani haujui namna bandari ilivyo ni vema uulize tukuleweshe sisi ni wadau pale
Hii hapa ni nafasi nzuri sana kwako wewe kueleza yanayotokea bandarini, hakuna lazima aje akuulize ndipo utueleweshe wengi tusiojua kinachoendelea huko.
Pengine hata Waziri Mkuu atashukuru kwa maelezo yako hayo.
 
Shida kubwa yetu sisi watanzania ni mindset za kufanikiwa kupitia wizi. Kuanzia juu mpaka chini kila mtu akilala akiamka anawaza jinsi ya kupiga awe tajiri faster atambe mjini. Mimi nahisi mamlaka zipo nyingi ila akishajulikana tu nae anapozwa kidizaini ndio maana kila siku eti system haifanyikazi mara mtandao upo chini maana system zinawabana sana wapigaji hawazipendi hata kidgo
 
Kuna haja gani ya kuwa na Waziri mkuu, Waziri wa uchukuzi, Katibu mkuu, TPA na Mkuu wa mkoa kama mnataka Rais pia akafanye kazi bandarini??

TISS wapo sana bandarini na hizo taarifa zote zipo.
Tatizo pale ilikuwa huyu DG mmoja ambaye hakusikiliza mtu yoyote, bodi, PS, Waziri hata PM !! Yeye alikuwa na Jiwe tu..
Mfano huko katika mafuta, flowmeter imefungwa 2014 na ina vitu kibao. Hata Rais anytime akibonyeza anaona kila data, quality ya mafuta pesa nk..
BUT wapigaji wakiongozwa na huyu jamaa aliyekuwa DG walikongoroa kila kitu, vuruga softwares, ili kuharibu data na kila aina ya records....hujuma za wazi kabisa. Sasa unashangaa Jiwe kweli hakujua haya, hao TISS je,
kama reports waliandika nini na wapi !!
Kibaya hawa watu mtandao wao bado upo TPA...sasa bila kusafisha issues zitaendelea...
Bodi pia inabidi isafishwe nadhani Mama anajua hilo..
 
Jamaa anacheka mda wote wakati watu wanapiga hela na ujanja mwingi
Bandari ikishikiliwa vizuri ni mradi mkubwa sana
Majaliwa kategeshewa watu wa kuwahoji nae kaingia kingi mazima!! Majaliwa inabidi Sasa awe anatumia mbinu zake mwenyewe kupata information za kutosha! Hata ikibidi apenyeze watu wake nje ya wale walioko kwenye system!!
 
Kwani huyo DG hawezi kumpiga fix Rais,Kama anavyopigwa fix Majaliwa!?
 
TISS wanatoka sayari nyingine!!???
Ungejuaa....
 
Mipakani na kwenye makao makuu ya kila taasisi na wizara.
 
Utopolo mtupu. Badala utake uwajibikaji wa imara wa bunge kusimamia nchi na serikali unataka mambo yachimbiwe mafichoni kwenye dola.
Watu wa nchi hii wanalielewa neno uwajibikaji kweli? Kuna mambo yanaudhi sana. Kuna wakti bora hawa wakae wanajeshi tujue moja
 
Je hyo issue anayoizungumza waziri mkuu ya system kuwa down ni michezo ya watu kupiga au ebu fafanua kdogo mdau
System yoyote ikizidiwa na watu walio-log in huwa inakuwa down au ikitokea ishu za kiufundi either server mbovu at zimezidiwa au system ikiwa haijawa updated. Hayo ni Mambo ya watu wa IT. System zote hata mpesa, Airtel money, Tigo pesa, system za ATM, banking, system za TRA ni normal kuwa slow wakati mwingine. Haya ni Mambo ya kawaida sema kuna kasumba linalitokea bandari basi watu wanasema wizi tu.

Kuhusu system kuwa down sio kweli, Ile ilikuwa system ya TRA ambayo ipo linked na malipo ya bandari, Ila sababu watu wanafanya malipo ya bandari basi inasemwa ni bandari tu.

Hata malori yalipokuwa yamesongamana kukaibuka mixed views kuhusu hilo bila kujua ile ni ishu ya watu binafsi waliopangishwa maeneo kwa ajili ya mizigo yao.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…