Bandarini tulipaswa kutafuta waendeshaji na sio wawekezaji!

Bandarini tulipaswa kutafuta waendeshaji na sio wawekezaji!

fazili

JF-Expert Member
Joined
Jun 10, 2011
Posts
16,427
Reaction score
22,418
Serikali inapaswa kujua nini kinachotakiwa kufanyika ili kuongeza ufanisi wa mashirika yetu ya umma kama TANESCO, TTCL, ATCL, TRC, TPA, n.k. Ukichunguza sana utagundua kwa mashirika haya ambayo tayari tulishawekeza kama taifa kwenye miundombinu ya msingi hatuhitaji WAWEKEZAJI bali WAENDESHAJI. Kwa mfano hatuhitaji mwekezaji ATCL, TRC, BANDARI, au TANESCO, tunahitaji waendeshaji kwani hata sasa bado tunawekeza matrilioni kwenye mashirika haya ila ufanishi hakuna kwasababu ya uendeshaji mbovu.

Kwa ujumla hoja ya kushirikiana na wataalam kuendeleza bandari yetu sio mbaya, ubaya ni vipengele visivyokuwa na ufafanuzi wa kutosha kwa mfano katika mkataba wa bandari na DP World, ilipaswa kuweka wazi kwamba DP wanakuja kuendesha bandari na sio kuwekeza. Huu mkataba ni wa jumla jumla (vague) na hauna maelezo ya kina mfano ukomo wa muda na wigo. Siku zote ni hatari kuwa na mkataba usiokuwa bayana. Hili limenitia wasiwasi mkubwa kuhusu weledi na uzalendo wa viongozi wetu.

Ukweli ni kwamba bila kutafuta washirika wanatakaotusaidia KUENDESHA mashirika yetu ya umma, basi tutegemee hasara tu. Tukubali kuwa weledi wa uendeshaji wa mashirika makubwa hatuna na tunahitaji watu wa kushirikiano nao kwenye undeshaji. Sio lazima kufanya UBINAFSISHAJI, tunaweza kuruhusu wajuzi wakatusaidia kuendesha baadhi ya vitengo au hata shirika zima kwa ufanisi zaidi.

Ni suala la muda tu ila hayo mashirika niliyoyataja hapo juu yatatutia hasara kubwa kabla ya hayajafa! Serikali tafuteni management teams kutoka mataifa yenye uwezo mkubwa tuingie mikataba inayoeleweka ya KUENDESHA mashirika yetu kwa manufaa ya umma.
 
Ndio walivyofanya waarabu wakaendeleaa.
SISI tunahitaji waendeshaji kuanzia bunge, urais hadi chini tubakie tu kula gawio
 
Mwekezaji anaweza kuwa muendeshaji mzuri lakini muendeshaji ni ngumu kuwa mwekezaji.

Kutafuta mwekezaji ni kulenga ndege wawili kwa jiwe moja. Tutafaidisha kwa faida za uwekezaji na kwa kuwa mwekezaji naye anatafuta faida nzuri basi atasimia uendeshaji.
 
Back
Top Bottom