Bando za Intaneti kuangusha Serikali ya CCM

Bando za Intaneti kuangusha Serikali ya CCM

Justine Marack

JF-Expert Member
Joined
Jul 31, 2014
Posts
612
Reaction score
1,698
Kilio cha Wananchi kimepuuzwa na SERIKALI. Kwa Hali ilivyo ni wazi kwamba unyonyaji huu unabaraka za mamlaka za juu. Sasa imekua ni mashindano ya kukandakiza wanyonge.

Baada ya kauli ya waziri kuwa Bando za internet ni huruma ya ziada, Sasa Makampuni uameshusha viwango zaidi. Ni kama wamepewa maagizo ya kusanya pesa kwaajili ya mamlaka flani.

Ukweli ni kwamba, Dunia ya Sasa imehama kwenye sera zilipendwa za. Maji,elimu, afya na Barabara. Ni Aibu Kwa waziri kupuuza wakati wa digitali na kusema ni ziada.

Yaani Teknoama ni ziada na kwamba sio lazima. Huku ndiko kuvimbiwa Asali baada ya kulamba Kwa ulafi. Katika Uchaguzi ujao, sera ya Bando za simu itakua na mashiko kuliko hizo Barabara zenu, kuliko mazingaombwe yenu ya Milioni 50 Kila Kijiji.

Kwakua Waziri amamua kuwa mkwapuaji, ni wakati wa CCM kutafakari athali za maamuzi ya waziri huyu juu ya gharama atakazo sababisha.

CCM itaanguka sababu ya Bando za MB. Amin Amin Nawaambia.
 
Naomba namna ya kupata GB za bure za Vodacom, Tigo na Airtel. Au namna ya kupata sms na dakika za bure, Njoo PM unisaidie.Au naomba VPN ya tigo na Airtel.
 
Wape vyanzo vipya vya mapato ya kuweza kulipa serikali kubwa na ghali. Na wanaolipwa wanajiona special wanaenda kununua subwoofers,magari,flat tv na kila kitu kinatumia dollar.
 
Makampuni ya simu yanaikusanyia CCM fedha za uchaguzi 2025 ndiyo maana kelele za wateja zinapuuzwa.
 
Kilio Cha Wananchi kimepuuzwa na SERIKALI. Kwa Hali ilivyo ni wazi kwamba unyonyaji huu unabaraka za mamlaka za juu. Sasa imekua ni mashindano ya kukandakiza wanyonge.

Baada ya kauli ya waziri kuwa Bando za internet ni huruma ya ziada, Sasa Makampuni uameshusha viwango zaidi. Ni kama
Kuitoa CCM madarakani sio rahisi kihivyo. Kuitoa madarakani inatakiwa kiwepo chama cha majambazi wa kura....

Kile chema cha majizi ya kura kitabaki madarakani hata mabando, matozo, mauaji na chochote kile kinachoumiza wananchi kikiwepo....
 
Back
Top Bottom