kuna updates za aina mbili kwenye simu
-security updates
-updates za matoleo toka version moja kwenda nyengine.
hizi security updates ni muhimu sana zinatoka kila mwezi, zenyewe hazibadili muonekano au feature za os, kazi yake ni kukupa ulinzi kwenye simu na kukulinda na malware na threats mpya.
updates za matoleo, mfano kutoka android 8 kwenda 8.1. hizi hukuongezea features kwenye simu na kubadili muonekano. kama alivyoelezea mdau hapo juu.
umuhimu wa ku update ni kuwa na simu salama ambayo ni ngumu kushambuliwa, yenye mambo ya kisasa na mapya. kila toleo kunakuwa na kitu kinaitwa change log, hukuonesha ni mambo mangapi mapya yameongezwa.
hasara ya ku update ni kama alivyosema mdau mwengine hapo juu inaweza haribu mambo fulani, mfano unaweza update simu isikae na chaji kama zamani,
kama simu yako ni halali kabisa umeinunua na ina warranty usiogope update simu yako mara kwa mara, likitokea tatizo samsung wenyewe watawajibika kulitengeneza.