Wakazi wa Tabata Banebane eneo la Katoma, kipande hicho hakina maji ya mgao wala maji ya aina yoyote kwa kipindi cha miezi 5 na zaidi.
Majibu ya wahusika ni kwamba ooh kuna merekebisho, wakanganya sasa wanasema kuna mradi wa bomba haitoshi.
Baada ya kadhia hiyo ya muda mrefu, ndio wanakuja site usiku au siku, masaa ambayo wanakwepa kukutana na wananchi.
Simu zao ni kikwazo mana wanatukwepa kiukweli ofisi ya Tabata DAWASA, Meneja na watu wake taarifa wanazo nashangaa kitengo cha emergency au mafundi hawajawahi hata kufika na kuchukua hatua za makusudi. Bado wanatuma bill hewa.
Mnatuchukuliaje ?