Bangi ihalalishwe

Stroke

JF-Expert Member
Joined
Feb 17, 2012
Posts
37,630
Reaction score
47,434
Sijaona any criminality inayotokana na uvutaji wa bangi isipokua negative perception tuliyojijengea miaka mingi kuwa bangi sio nzuri.

Hili limenifanya nione kua bangi namsaada mkubwa ukiondoa ubaya unaosemwa juu yake.

Hivi majuzi nilibahatika kukukaa na rafiki yangu moja kwa wiki kama mbili hivi, huyu jamaa, kwa bahati mbaya aliwahi kupata ajali na akaumia sana maeneo ya kichwa, alifanyiwa operation kubwa tu, kwahiyo, kuna wakati anakua anasikia maumivu sana ya kichwa , wakati mwingine anashindwa pata usingizi, hivyo ili kupunguza maumivu , huwa anavuta bangi inampa uwezo wa kulala, kidogo.

Kama pombe yenye madhara lukuki imekubalika kwanini si bangi.
 
Sio bangi tuu pia gongo ihalalishwe maana inchi zingine gongo ni kinywaji well packed kama Malawi
 
naunga mkono hoja.....aisee
 
Wote waliounga mkono ni wavuta bangi..leo mnataka bangi ilalishwe kesho mmoja wenu akiliwa tgo mtataka ushoga ulallishwe..bangi ni mbaya msitualibie vijana wa kesho na mawazo yenu yakibangi bangi..nyambafu

Sent from my BlackBerry 9220 using JamiiForums
 
Kaka sio kupinga tu sababu uliambiwa bangi ni mbaya. Wenzio wameleta sababu. Mi naunga mkono hoja ila with reserves.
Naunga mkono bangi ihalalishwe sababu haina madhara kiafya kama ilivyo kwa sigara na pombe, pia inamafaa kwa magonjwa fulani fulani. Ikihalalishwa in a controlled environment inaweza kuzalisha ajira in the entire value chain: mkulima, mfanya biashara wa jumla na mfanyabiashara wa mwisho, yani yume merchant kabisa. Pia bangi ni natural pesticidde inaweza kusaidia katika kilimo, na hata kutuingizia kipato cha carbon credit kwa kupunguza usafirishaji wa pesticides zingine na pollution inayo tokana na hizo pesticide.
Reserve yangu ni kua some people may abuse. Just like pombe kuna watu wakinywa wanashindwa kujicontrol. Tatizo la bangi ni bei yake rahisi. Yani for 5000 worth of beer or bangi tofauti ni kubwa sana, hivo people prone to addiction WILL get addicted na itakua gharama kubwa kuwasaidia.
Hivo ikiwa serikali itaamua kuhalalisha bangi basi tufungue coffee shops, na only watu fulani (ambao criteria zao zitachaguliwa) wataruhusiwa kulima, kuuza, kununua.
 
Hakuna kuhalalishwa,mtuache...kwan Bila bhangi inawezekana tuu...

Sent from my BlackBerry 9780 using JamiiForums
 
Kwetu mbegu za bangi ni kiungo cha mboga kama zilivyo karanga na tetele.
 

mkuu mimi sio mtumiaji wa bangi, na nilikua na perception kama yako mkuu, lakini nilivyokutana na huyu bwana, nikabadili mawazo mkuu, the guy anateseka sana lakini akishapata hiyo kitu analala vizuri sana mkuu, utamuonea huruma kaka, usihukumu watu bila kujua chanzo mkuu, kaa kwanza na kujua the reason behind ndio utoe maoni yako na si hukumu
 
Kaka nasio kutetea kisa umesoma google..nakubaliana na ww bangi inatumika to some extent kama dawa..ila its effect ni dynamic kwa mtu na mtu haiko uniform kama vitu vingine kama sigara..na sisemi singara ni nzuri hapana ila economically ni nzuri more benefit than bangi..kwanza harufu yake mbaya..na medical assosiations hawajaja na conclusion as all persea

Sent from my BlackBerry 9220 using JamiiForums
 

this is reality mkuu, hakuna cha google hapa, nimeona ikanigusa..
 
Mkuu mkaliwakitaa Mkuu sio Bangi tu ihalalishwe na unga pia uhalalishwe unaonaje? Acha ujinga wako kwa kuwa wewe unavuta hiyo bangi unataka ihalalishwe? kwenda maneno yako ya pumba hayo Bangi haitahalalishwa kamwe nchini Tanzania labda wewe ndio uwe Rais wetu unaweza kuhalalisha vile vilivyoharamishwa.
 
Last edited by a moderator:

Na kuelekea 2015, vijana wa CDM wanaihitaji sana ili kuwapa mori wa kupigania haki ya kuingia ikulu, kulinda kura zao bila woga, n.k. Si unaona vijana hawatukani kwenye post hii bali wanashabikia?
 

wewe mpuuzi unaongea nini wewe, unafikiri kila anaetetea jambo analifanya, wewew ndie mjinga unaeleta mada zako za kipuuzi hapa za kugoogle na kijifanya bonge la mjanja mjinga ni wewe na ukoo wenu wote
 
Pamoja na kupigwa Marufuku inapatikana kwa kila sehem kuliko maji safi na salama, kama vipi tenda ya ku supply maji au pembejeo za kilimo wapewe wauza bhangi maana wanafika kila kichochoro na kila korongo!
 
wewe mpuuzi unaongea nini wewe, unafikiri kila anaetetea jambo analifanya, wewew ndie mjinga unaeleta mada zako za kipuuzi hapa za kugoogle na kijifanya bonge la mjanja mjinga ni wewe na ukoo wenu wote
Unasisitiza upuuzi wako hapa eti Bangi iruhusiwe kwenda thread yako ya kipuuzi hiyo unayo kweli akili wewe? Bangi inapigwa vita Dunia nzima wewe unakuja hapa kuleta utumbo wako eti ihalalishwe bangi hapa kwetu Tanzania? na wewe ukiweza ka google na wewe uweke pumba zako.
 
Mkuu Roulette Na wewe Moderator Mzima unaunga Mkono Bangi Serikali ihalalishe ahhh? Sikutegemea kama utakuwa hivyo ahhhhh

Utafiti: Madhara ya bangi yanaongezeka


BAADA ya kuwepo kwa baadhi ya tafiti zilizokuwa zikiruhusu uvutaji wa bangi kwa madai kwamba ilisaidia wagonjwa waliosumbuliwa na msongo wa mawazo, hali hiyo imesababisha baadhi ya nchi kuruhusu matumizi yake.

Pamoja na mawazo ya wengi kufikiria kuwa kutokana na nchi ya Jamaica ndiyo ilikuwa mstari wa mbele kwa watumiaji wengi ingekuwa ya kwanza kuruhusu bangi, lakini ukweli ni kwamba nchi ya Canada ndiyo ilikuwa ya kwanza kukubali bangi kutumiwa kama dawa ya maradhi.


Baada ya utafiti huo wa awali hivi karibuni watafiti wengine wamegundua kuwa matumizi ya bangi kwa muda mrefu yanasababisha kujiongezea madhara badala ya kutibu kama ilivyokuwa ikisemekana hapo awali.


Watafiti hao wamekwenda kinyume na wale wa kwanza kwa kusema kuwa matumizi yake yana uwezekano mkubwa wa kumletea mtumiaji magonjwa ya kupungua uzito mara kwa mara, magonjwa ya figo, ini na ugonjwa wa akili.


Watafiti waliogundua athari hizo ni wale wanaotokea nchini Australia ambao katika utafiti wao wamegundua kuwa zaidi ya vijana 3,100 walio katika umri wa miaka 20 ndio wamekuwa watumiaji wakubwa wa bangi.

Utafiti wao umekwenda mbali na kubaini kwamba asilimia 18 ya vijana hao ni wale waliojiingiza katika matumizi ya dawa hizo za kulevya kwa muda wa miaka miwili au mitatu.

Asilimia nyingine 16 ya vijana wa umri huo wamebainika kutumia kwa muda wa kati ya miaka minne hadi mitano.

65 kati ya watumiaji wamegundulika wameshaathirika na maradhi ya ugonjwa wa akili.

Wakati hao wakisumbuliwa na tatizo hilo wengine 233 wamebainika kuathirika kwa figo na ini.

Watafiti wamebaini vijana wengine kati yao wanasumbuliwa na tatizo la kupata uchizi (wehu).

Baada ya kubaini hayo watafiti wametoa ushauri kwa vijana kutotumia dawa hizo za kulevya kwa vijana kwa zaidi ya miaka sita au zaidi tangu pale siku ya kwanza alipoanza kutumia.


Wanasema kuwa kwa wale ambao sasa wamevuta kwa muda mrefu kati ya miaka 15 na zaidi wengi wao wamekumbwa na tatizo la kiakili.


Kwa mujibu wa Dk. John McGrath, wa kituo cha uchunguzi wa afya ya wagonjwa wenye mtindio wa ubongo cha Queensland, nchini Marekani, anasema: “Wengi wa wagonjwa ambao wamekumbwa na matatizo hayo tumegundua ni wale waliowahi kutumia bangi kwa muda mrefu na hatimaye kujikuta wakipata tatizo la akili.”


Daktari huyo anasema kuwa ni nadra sana kukutana na wagonjwa wa akili vijana halafu wakawa hawajawahi kutumia bangi, iwe mwaka mmoja au zaidi.


Anasema kuwa iwapo matumizi ya bangi yatakomeshwa tatizo la vijana kupata matatizo ya utaahira yatapungua kwa kiasi kikubwa duniani.


Bangi ni nini, inatumiwaje?


Kwa hapa nchini na baadhi ya nchi, bangi imetambulika kama dawa ya kulevya ambayo imekuwa na majina mengi kutokana na kutumiwa na kundi la vijana zaidi kuliko watu wazima.

Bangi imekuwa ikijulikana kwa majina mengi ikiwamo, dawa, ganja, hashish, kijiti, marijuana, kaya blunt na mengineyo, ilimradi kutegemeana na sehemu inapotoka.

Watumiaji wengi wamekuwa wakiitumia kwa kuvuta kama sigara au wengine hutumia kwenye kiko kwa kuvuta.

Bangi ni bidhaa iliyochanganyika na kemikali hatari ambazo ni sumu na huathiri afya.
Wapo baadhi ya watumiaji wa bangi ambao wamekuwa wakiitumia kwa kuiweka katika maji wakiifanya kama majani ya chai na wengine huchanganya kwenye chakula.

Bangi inaathiri vipi ubongo?


Wanasayansi wamebaini kuwa matatizo makubwa yanaanza kupatikana kutokana na bangi kuingia kwenye ubongo wa mtumiaji na huathiri mfumo mzima wa akili.

Tatizo kubwa linalomkumba mvuta bangi ni kunyemelewa na magonjwa ya ugonjwa wa shinikizo la damu (BP), kupoteza kumbukumbu, mawazo, anaridhika hata kama ana matatizo.

Pia mtumiaji wa kila siku anakuwa akikumbwa na mabadiliko ya mara kwa mara katika ubongo wake.

Imebainika kuwa bangi inachangia kuongeza mapigo ya moyo kutoka asilimia 20 hadi 100, muda mfupi tu wa saa tatu baada ya kuvuta.

Bangi huaribu mapafu, kwani ina zaidi ya asilimia 50–70 ya kemikali aina ya carcinogenic hydrocarbons kuliko mvutaji wa tumbaku.

Mtumiaji wa bangi hupumua kwa tabu sana kuliko yule anayevuta tumbaku ingawa wote wanaharibu mapafu, pamoja na kuwa na uwezekano mkubwa wa kukaribisha ugonjwa wa kansa.

Imebainika kuwa watu wanaovuta bangi wamekuwa wakisumbuliwa zaidi na matatizo mengi ya kiafya.

Watafiti wamegundua kuwa wavutaji wengi wa bangi wamekuwa hawana mahusiano mema na watu walionao karibu kwani wamekuwa chanzo cha matatizo kutokana na wao kuona kila wanachofanya ndiyo sahihi na cha wenzao si sahihi.

Chanzo.
Utafiti: Madhara ya bangi yanaongezeka

https://www.jamiiforums.com/jf-doctor/412059-marijuana-side-effects-madhara-ya-uvutaji-wa-bangi.html
 
Last edited by a moderator:
tukihalalisha bangi haitochukuwa muda mrefu tutaanza kuagiza kutoka ulaya kwa matatizo ya nchi hii
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…