SoC02 Bangi iwekwe huru

SoC02 Bangi iwekwe huru

Stories of Change - 2022 Competition
Joined
Sep 8, 2022
Posts
2
Reaction score
16
BANGI IHALALISHWE.

Kwa ulimwengu wa sasa siyo vyema kuendelea kudanganyana , baahi ya masuala hayawekwi wazi siyo kwa sababu gani? Hakuna cha maana zaidi ya danganya toto.

Sheria na kanuni nyingi zimewekwa ambazo zipo kwa maslahi mapana ya mamlaka zinazongoza raia . Vingi vimehalalishwa na vingine vitahalalishwe iwe leo au kesho lakini vipo kwenye mchakato huo wa uhalalishwaji .

Kati ya kitendo haramu Ulimwenguni , matumizi ya mmea wa Cannabis Sativa /Indica ni miongoni mwayo . Yaani ikijulikana ni mtumiaji wa mmea huo basi heshima itashuka kwa kiwango fulani .

Ijapokuwa kuna mengi yanayofanyika na kutendeka ya kiovu , yenye kukiuka kanuni na taratibu lakini walimwengu wamefumbia macho wapo kimya tuu .

Nawaona watetezi wa haki za wapenzi wa jinsia moja wametapakaa kila pembe ya Ulimwengu , wengine wakiwa viongozi wa madhehebu kabisa huku wengine wakiwa watu maarufu wenye kutoka kwenye kada tofauti tofauti .

Pamoja na kupata shida kwenye baadi ya mataifa lakini wanazidi kukua na kuonekana kwamba wanalao jambo na kwa baadhi ya mataifa Ulimwenguni umepitisha rasmi haki zao za kuoana wenyewe kwa wenywe .

Hebu tuliache hilo , kwa siku za hivi karibuni huko Ughaibuni kumekuwa na wimbi la ongezeko la wanaharakati wengine watetezi wa haki za kutoa mimba! Yaani wanaandamana mitaani kutetea uovu wa namna hiyo na mpaka wanagika mahakamani kutetea hoja zao za mauaji .

Eti wanasema ujauzito ukiwa chini ya miezi mitatu unaweza kutolewa bila tabuu , wanajisahaulisha yote hayo ni mauaji uwe na wiki mbili au miezi nane huo wote ni ujauzito na ni kiumbe hai kimebebwa siyo mfuko wa nylon .

Huwa napata wakati mgumu nionapo ama kusikia mpaka kuna mataifa yanamiliki silaha za maangamizi , mabomu ya atomic nyuklia na silaha nyinginezo za kikemikali ambazo huwa wanapata wasaa wakuzungumza endapo mmoja wao akimshambulia mwenzie ijapokuwa kutakuwa na vifo pamoja maafa kuripotiwa lakini wao watazungumza yao hakuna shida .

Harakati nyingine zinaenda sawa kabisa michakato inaonekana inaridisha kwa namna moja ama nyingine ila suala la harakati za uteteaji wa mmea wa Cannabis Sativa/Indica bado lipo nyuma sana na wanaharakati wake hawana nguvu yeyote ya kutetea hoja zao .

Leo hii tukizungumzia idadi ya vifo vitokanavyo na matumizi ya sigara ni makubwa sana na yanazidi kuongezeka kila mwaka , huku watumiaji nao wakiongezeka kila uchwao kutokana na matangazo yatangazayo bidhaa hizo za tumbaku .

Sigara zinavutwa , pombe zinanyweka na matangazo juu ya kukuza biashara zao na kuongeza watumiaji . Jamii zinazidi kupoteza wapendwa wao ila kwa kuwa ni bidhaa zilizo halalishwa hakuna pakwenda kushtaki na endapo ukiwafungulia mashtaka utaonekana akili hazikitoshi .

Haya magari yanayobeba sigara yanalindwa na mitutu kabisa , nakubali taifa letu kwa muda mrefu limekuwa chini ya mihimili miwili kwenye ukusanyaji kodi mihimili hiyo ambayo ni sigara na pombe imelibeba taifa letu la Tanzania kwa miongo nenda rudi leo hii tozo zimeletwa kuongeza kipato kwa serikali .

Wakati ule wa pombe za kwenye packet "viroba" zilipokuwa zipo kampuni husika walipiga pesa siyo mchezo na wao ndiyo walikuwa wanalipa kodi kuliko hata kampuni za madini pamoja na kuchangia vifo vya maelfu ya vijana ambao walikuwa ndiyo nguvu kazi ya taifa ila walipendwa na kuheshimika sana .

Sasa turudi kwenye Bangi mmea rafiki sana ambao hauhitaji mambo mengi unapooteshwa , sehemu nyinginezo unaota bila kuoteshwa yaani ni mmea wa asili kwa matumizi ya asili kabisa .

Kuna propaganda eti mvutaji akivuta basi itamkaa kichwani miaka saba , hii huwa inanichekesha sana yaani miaka saba kitu kipo kichwani tuu hakuna kuisha kama ni kitaaluna ni safari ya kutoka kidato cha kwanza hadi chuo mwaka wa kwanza inaisha ukiwa unaingia mwaka wa pili na hapo ni kwa mvuto wa mmoja je! Kwa mvutaji wa miaka kumi atakuwa na "stimu" kwa miaka mingapi??

Sehemu baadhi ya wanajamii wanapokwama ni pale wanapodhani mmea huu ni kwa ajili ya kuvutwa tuu! Hapo wanakosea sana tena sana kwakuwa Cannabis inaweza kutumika kwa kunyweka , kupakwa , kufukiza na hata kulika inategemeana na mapendeo yako .

Huko Ughaibuni kuna baadhi ya mataifa mmea huu umehalalishwa kwa matumizi ya tiba "Medical Marijuana" , huko Latin America kuna taifa la Uruguay kwao unatumika bila tabu .

Majuzi wakati wa kampeni za kugombea urais nchini Kenya miongoni mwa wagombea urais Ndugu Profesa George Wajackoyah kupitia chama cha Roots aliweka bayana kwamba endapo akishinda urais basi mmea huo ungehalalishwa nchini humo .

Wengi walimkebehi na kumuona mjinga ila kiukweli wao ndiyo walikiwa wajinga na siyo yeye , kwa mahesabu ya Profesa Wajackoyah mmea huo ungliingizia mapato taifa la Kenya ambalo kwa miaka mitatu wangelipa madeni yote wanayodaiwa lakini basi kura hazikutosha na kuambulia kukamata nafasi ya tatu kati ya wagombea wanne .

Leo hii soko la mmea huu lipo juu sana ulimwenguni kwa kuwa mali ghafi yake ina soko kubwa huko Ulaya na Marekani ambako wanatumia kwa matumizi ya dawa ambayo hutibu Saratani , glaucoma , matatizo ya kukosa usingizi na baadhi kutumia kwa kupunguza lehemu mwilini .

Kama sigara ambayo zao lake la tumbaku hulimwa pekee yake kutokana na ukweli kwamba endapo likilimwa na mazao mengineyo hupelekea mazao hayo kugeuka sumu endapo yakitumiwa kwa matumizi ya chakula , lakini Bangi inalimwa na mazao kedekede ambayo baadae huliwa na watu bila tabuu yeyote .

Ifikie wakati sasa mmea huu uhalalishwe taifa letu lijiingizie kipato na siyo kuendeleza propaganda za kikoloni ambazo zilitumika miaka ya 1950 huko ambapo wapiganiaji uhuru wengi walikuwa wavutaji nao wakapitisha maneno yao yasiyo faa kabisa .

Wakati huo Fidel Castro , Che Guevara , Dedan Kimathi na MAUMAU wenzie walikuwa watumiaji pamoja na wanaharakati wengi waliyopambana dhidi ya ukoloni walipachikwa maneno mabovu likiwemo la ukichaa kutokana na kutumia kwao mmea wa Cannabis .

Ifikie wakati sasa serikali ipitishe matumizi na ulimaji wa mmea huu ambao utatuletea faida na tija kubwa kwa maslahi mapana ya taifa letu vizazi vilivyopo na vijavyo . Bangi ihalalishwe , Ahsante Sana!

Cc.Video kwa hisani ya Mtandao .
 
Upvote 11
Ningekubaliana na wewe kama ungepambania pombe na sigara zipigwe vita kama bangi.
Bangi ni nzuri kimatibabu, inatumika kutengeneza dawa za binadamu. Ila bangi ikitumika kupita kiasi bila utaratibu wa wataalamu wa afya ina madhara makubwa sana kwa binadamu, ikiwemo kua kichocheo kikubwa cha uhalifu.
 
Jamaa umetiririka kwa mapana na kwa uwazi Sana nikupongeze lakini naomba ufahamu na kutufahamisha tutajueje kuwa kichwa gani kinafaa kuhimili hiyo ganja na Kipi hakifai kuhimili iyo ganja Mf. Ndugu yangu anarafiki yake ndugu yangu akajifunza kuvuta bangi kutoka kwa rafiki yake TUKAWA tunaona mabadiliko fulani mwisho alichizi lakini rafiki yake Hakuchizi mpaka nw bangi ni ya Wachache Sana kwa ushauri wangu MFUNDISHE MWANAO KUPIGA PAFU MOJA MBILI SAFI LAKINI KUSHAURI UMA NAMNA HII WEWE NI MPUMBAVU MKUBWA MJINGA MSHENZI KAMA HAWO ULIYOWATAJA HAPO JUU VUTA MWENYEWE USIHAURI WATU TUMEKUWA TUKIPOKEA WATU WENGI SANA WENGINE WANAHALI MBAYA KUHUSU HAYA MAMBO KAMA KICHWA CHAKO KINAHIMILI IT'S FINE
 
kiundani soma kitabu.
IMG-20220716-WA0002.jpg
 
Wewe pamoja na wanaharakati wanaotetea mapenzi ya jinsia moja Kuna tofauti gani?
 
Utakua uliandika topic hii ukiwa unavuta…. Kwa lugha nyingine uko haireee 🤣😊
 
Back
Top Bottom