Bangi ni mbaya sana

yaan unamkera kwakweli hebu acha !umeshindwa fanya sekondar shost !muone
Huu mwaka wa mwisho, naacha!
Hapana demi, ni ulevi kama ilivyo kwa ulevi mwingine kama vile pombe, sigara, kahawa, chai n.k. kwakuwa ukiivuta unajiskia burudani we vuta tu sio kesi maisha yenyewe mafupi haya fundi wangu
 
Ntatumia vyote lakini bange hapana..mambo ya kua tajiri kifikra siyawezi kabisa.
 
Ni kichwa chako tu,ikikikupenda safi sana hii kitu! ...Kama ulikua na appointment na demu,ukipiga hii kitu unaweza mpigia simu asije cuz unataka utulie ufikirie mambo yako.
 
Hahahahahahahaha
 
Ofcoz nakumbuka hata pindi nipo chuo ilinisaidia sana ktk usomaji maake ilinipa uwezo wa kuelewa kitu mapema saana na nikisoma topic ina kaa fasta
Mwathilika tayar .....nilisha kaa na watu wa hiv
Hua Ukiwaona ni smart na mada wanachangia fresh tu...ila badae utagundua tu kama hapa nazungumza na bangi...
 
'Legalise it and i will advartise..'by Peter Tosh

Bange,ndumu,weed,kijiti,herbs, ganja,blunt,moshi,msokoto,cha Arusha,majani,Bob Marley,puli na nk.

Kete kitaani ni jero hadi buku,(ni chanzo cha mapato)
 
Miaka ya 90 wazazi wangu walikuwa na mpangaji wao anakaa chumba cha nje, jamaa alikuwa msela sana na tulizoeana kibahati kwani tulikuwa hatuonani mpaka niende kwa wazazi kuwatembelea. Siku ya siku jamaa akaniambia nitoke chumbani kwake kwa sababu anataka kulipuliza, sikumuelewa.....akaniambia kinaga ubaga kuwa anataka kuvuta bangi na hataki nimuone kwani hataki kunitia matatizo na wazee wangu. Nikamwambia isiwe noma, tuvute wote huku nikijipa ujasiri kwamba LAZIMA nimuonyeshe huyu jamaa kuwa mimi ni mvutaji pia wakati nilikuwa sijawahi kuvuta hata siku moja. Tukalipuliza la kwanza, sikusikia kitu....akawasha lingine, tukalipuliza...hapa ndipo nikaona naanza kupaa mle chumbani mwa yule yanki. Nikamuuliza...hivi tuliingia saa ngapi ndani ya hili daladala mbona sikumbuki, naye akaniuliza...daladala gani mbona bado tuko getoni? Ghafla akapita mende, wacha nikimbizane naye mpaka uwani huku nikimtukana matusi ya hajabu....yaani hapa nilikuwa sikumbuki kama niko home kwa wazee. Nikaitiwa chakula, ile tunaanza kula dingi akaniuliza kama nimelewa nikamkatalia. Tunaanza kula tu, nikajikatia tonge langu la ugali nikapamba kwenye maji tuliyonawia, dingi akashindwa kunivumilia. Akanipiga kofi la uso na kuniambia nitoke mara moja huku akiwa kasimama, nikajuwa hapa nakula mkong'oto, nikakimbilia uwani kujificha maana dingi alishajuwa nilikuwa under the influence. Huko uwani sasa, nikajisikia baridi kali inajaa mwilini....katika kumuepuka baba, nikaenda kujifungia ndani ya banda la mbwa usiku kucha. Kuhamka asubuhi mwili wote unanuka mimavi ya mbwa na mengine nilikuwa nimeyalalia kichwani. Jamani bangi si chezo haswa kwa wanaojifunza.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…